Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Na Maggid Mjengwa,
ZAMANI sana kulikuwa na bendi ya muziki wa dansi ya Kiwanda Cha Urafiki.
Iliitwa Urafiki Jazz Band, wana Chakachua. Naam. Wanamuziki wale waliweza
kuchakachua ala za muziki, wakaimba na watu wakachakachuka ukumbini. Siku
hizi ukisikia Chakachua unafikiri juu ya mafuta ya diseli
yanayochakachuliwa. Ina maana yanachanganywa na mafuta ya taa, oil chafu,
petroli na viviminika vingine unavyovijua!
Basi, alimradi tunaendeleza maisha yetu ya ovyo ovyo. Anayekaanga chipsi
anachakachua mafuta ya kukaangia. Tumefika mahali hata mafuta makali ya
transfoma za umeme yanatumika kukaangia chipsi!
Ah! Na majumbani nako kuna wanandoa wanaochakachua mahusiano yao. Na hata
utamaduni wetu haujanusurika. Naam. Hata maisha tunayoishi nayo ni ya
Ku-Chakachua. Na hilo ni Neno La Leo.