Neno La Leo: Hata Maisha Tunayoishi Ni Ya Ku-Chakachua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Hata Maisha Tunayoishi Ni Ya Ku-Chakachua!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jul 23, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,
  ZAMANI sana kulikuwa na bendi ya muziki wa dansi ya Kiwanda Cha Urafiki. Iliitwa Urafiki Jazz Band, wana Chakachua. Naam. Wanamuziki wale waliweza ‘ kuchakachua’ ala za muziki, wakaimba na watu wakachakachuka ukumbini. Siku hizi ukisikia ‘ Chakachua’ unafikiri juu ya mafuta ya diseli yanayochakachuliwa. Ina maana yanachanganywa na mafuta ya taa, oil chafu, petroli na viviminika vingine unavyovijua!
  Basi, alimradi tunaendeleza maisha yetu ya ovyo ovyo. Anayekaanga chipsi anachakachua mafuta ya kukaangia. Tumefika mahali hata mafuta makali ya transfoma za umeme yanatumika kukaangia chipsi!
  Ah! Na majumbani nako kuna wanandoa wanaochakachua mahusiano yao. Na hata utamaduni wetu haujanusurika. Naam. Hata maisha tunayoishi nayo ni ya Ku-Chakachua. Na hilo ni Neno La Leo.
  Kwa kazi zaidi za Maggid, tembelea; mjengwa / http://www.kwanzajamii.com
   
 2. F

  FM JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red hapo!!!
   
 3. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Nimepapenda hapo kwenye le blee!
  hiyo ndo haswaa ian leta chakachua zoote ulotaja mkuu.
   
Loading...