Picha:Tajiri namba moja lakini anaishi kawaida kabisa

8434958c50a742f8aaa1c18337011fa2.jpg


a53e3cd8603021581f7a051d6b2a90d7.jpg


29dc2360ff4a26a4b8facb4cfeccab9d.jpg


Steve Jobs CEO wa Apple.
Billionaire lakini ukimtizama au kukutana naye utadhani ni mzee anayeshinda kwenye vijiwe vya kahawa yupo simple .

Sasa ww ukipata vi laki 3,5 zako kila mtu atajua utajishebedua,gari ulikimbize ututimulie mivumbi
hebu tuonesheni na matajiri ambao wanaishi maisha ya kitajiri basi

maana mi hapa naona kama mnatakakupotosha kitu fulani na hoja zenu zenye upande mmoja wa shilingi...!!
 
Masharti ya mganga unaambiwa utajiri tunakupa ila ufanye hivi.
-usipake pafyum
-usivae viatu
-usilale juu ya kitanda
-usivae nguo ya thamani wala vito (dhahabu)
-usilale zaidi ya masaa kadhaa ukilala lazma uchome ubani(ufukize dawa)
-usifanye mapenzi hata siku 1
-usizae mtoto
Pesa unazo lakini huna uhuru nazo.
 
*Iko hivi*

“Maskini na tajiri wana mawazo tofauti.

Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo.

Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo.

Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya.

Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.

Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi.

Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.

Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa.

Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.

Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda.

Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.

Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana.

Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.

Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita.

Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja.

Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani.

Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.

Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa.

Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa.

Maskini ana woga.

Tajiri hana woga.

Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha.

Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri.

Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi.

Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.

Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa.

Tajiri hutumia pesa kupata pesa.

Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake.

Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.

Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa.

Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine.

Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.

Fikiri kama anavyofikiri tajiri.

Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.”

Chanyata Ubongo wako sasa!
...!!!
 
Huyu jamaa anaishi kawaida kabisa japokuwa ndie tajiri namba moja Africa. Hebu ktk hiyo picha tazama
1,Kalamu
2,Mapete vidoleni (hana)
3,Simu ya kawaida kabisa

Sisi ukipata hela za mkopo tu utavaa Mapete vidole vyote,utaning'iniza funguo za kavits ka mkopo hadi za mageti yote ya nyumbani kwako,utajifanya kuzungusha round wakati hela yenyewe ndio hiyohiyo, nk nk Tunaishi kimaigizo sana.
Tuna kiburi,jeuri,tu wavivu wengi wetu,hatuheshimu kazi,tunapenda sana siasa kuliko uchumi,si ajabu tutasalia hivihivi.
Tubadilike watanzania wenzangu.
6cd7bbf8e0f5f153db999ae0378ea684.jpg

FREEMAXENCE.
N'yadikwa
Mkia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom