barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,870
Hisia nyingi za wengi zilielekezwa kwa Associate Profesa Peter Kopoka,Mkuu wa zamani wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala UDOM.
Wakati huo Prof Kopoka alikuwa upande wa Edward Lowassa na hakuficha hisia zake juu ya kuwa upande wa Lowassa "die hard".Hata baada ya kujulikana,kesi hiyo ilipelekwa kwa Makamu Mkuu wa Chuo ambaye alitakiwa kumchukulia hatua kwa kujihusisha na siasa wakati ni "mtumishi wa umma".
Hata alipoulizwa,Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alisema kwa kuwa jambo hilo lilionekana kukiwakilisha chuo katika masuala ya siasa, uongozi ulilazimika kumhoji mhadhiri huyo.
“Ametuandikia barua ya kujieleza na kubainisha kuwa alikwenda yeye binafsi na siyo kama mwakilishi wa chuo. Lakini mambo haya ni magumu sana kutofautisha. Mimi kwa mfano, siwezi kwenda sehemu halafu nikasema sikwenda kama mkuu wa chuo kwa sababu siwezi kutofautisha hilo. Lakini tumechukua maelezo yake na tumeyahifadhi,” alisema Profesa Kikula
Ajabu ni kuwa,juzi kati wakati CCM inatimiza miaka 40 ya uhai wake,Prof Idris Kikula,mhadhiri wa zamani wa UCLAS/Ardhi (AU) na mwanachama wa chama cha Mapinduzi,akiwa kama mtumishi wa umma alijumuika na sisi wanachama wenzake kuhudhuria sherehe hizo ndani ya ukumbi mpya wa CCM eneo la Ntyuka-Dodoma.
Katika picha hii ndani ya ukumbi,ambayo haina tofauti na kitendo kile alichokifanya Prof Kopoka,huyu Prof Kikula anaonekana akiwa amekaa katikati ya wanachama wa CCM na si kwa wageni waalikwa.Mbele ya Nape Nnauye na jirani na Prof Kabudi,VC Prof Kikula anaonekana akifuatilia kwa makini sherehe hizo akiwa ndani ya sare za chama cha mapinduzi.
Sasa kwa hali hii ya Prof Kikula,kuvaa chati la chama,kukaa ukumbini na kusherekea kama mwanachama wa CCM,kuna tofauti gani na Prof Kopoka wakati ule?Je na yeye Prof Kikula alipokuwa pale ukumbi wa chama,alienda kama yeye au kama mkuu wa chuo?Kama ilikuwa ngumu kwa Prof Kikula kupata "ugumu" uwakilishi wa Kopoka kama ulikuwa binafsi au wa chuo,Yeye uwakilishi wake pale ulikuwa binafsi au wa chuo?Ukizingatia yeye kwa nafasi ya Makamu Mkuu wa chuo,popote anapoonekana,basi "UDOM" imewakilishwa.
Aina hii ya siasa za visasi,upendeleo,ghiliba,chuki na kukomoana,zinaweza kujenga hisia hasi miongoni mwa wananchi,hata kama linalofanyika lima nia njema.Hii inatukumbusha enzi za Prof Baregu kusitishiwa mkataba sababu za itikadi zake,Prof Abdallah Safari kuondolewa chuo cha Diplomasia Kurasini na kupokwa gari lenye namba za kidiplomasia sababu ya mtazamo wake kisiasa.
Ni wakati wa wasomi wa Tanzania,kuchagua ama kuwa baridi au kuwa moto.Hii tabia ya kuwa vuguvugu ni dalili ya unafiki na utumwa kwa wanasiasa.