Mbandika picha ni vizuri ungeelezea na hali halisi ya alichozungumza Rais wetu na jinsi ya huo umati ulivyofika hapo na ni % ngapi ya watu wa mjini Igunga wamehudhuria
1. Mapokezi yake yalikuwa jana na alipokelewa na wananchi wachache na vijana wa bodaboda na bajaji walichukuliwa kwa ahadi ya kupewa Tsh.5,000/= jambo ambalo ni aibu na pia hata hiyo fedha yenyewe hawakupewa.
2. Juhudi za kusomba watu zimeanza tangu jana na watu walifikishwa ma maloli kama 5 hivi na wote walilazwa chini katika ofisi za CCM chakula cjui kama walipata. Aibu ya pili hiyo.
3. Leo siku ya mkutano watu wamesombwa na malori yasiyopungua 20 kutoka maeneo yote ya vijijini.
Aliyoongea mengi yalikuwa yamejaa ushabiki wa kisiasa na sio ya kujenga umoja na mshikamano kwa Watanzania.
kuna kauli ambayo niliona haikufaa kwa kiongozi wa nchi kuizungumza.
** Alisema ujenzi wa Daraja ni ahadi ya serikali ya chama cha CCM na ipo katika ilani ya CCM sasa anashangaa imekuwa ni kigezo cha kuvuliwa ubunge kwa Kafumu, itabidi sasa tuwe tunafanya kampeni za Kibubu kwani ukiongea tu inakuwa kosa na hapo mbeleni itabidi tutafute namna ya kuepukana na hili(namna gani anajua yeye) kwa kauli hii naona anapingana moja kwa moja na sheria za nchi hii. Pia alisema Dr. kafumu amekata Rufaa wanachosubiri ni uamuzi wa mahakama kama watashinda au la lakini wakishindwa wataingia kwenye uchaguzi na watashinda kwa kishindo kuliko uchaguzi uliopita. HAPA WATU WENGI WALIGUNA. hapa inaonyesha CCM kazi wanayo.
Labda kitu kinachonishangaza kwa nchi yetu inatakiwa tutenganishe Ziara za Serikali na Chama Rais anapofanya ziara za Serikali na kuingiza mambo ya Chama yanaleta sintofahamu kwa watu wengine. wenzetu USA Rais akishachaguliwa iwe ndani au nje ya nchi anapeperusha bendela ya Taifa huku kwetu nimeshangaa kuona mitaa yote ikiwa imetapakaa bendera za kijani (CCM) nimeshindwa kuelewa hii ni ziara ya serikali au Chama.