Picha: Membe na 'Mcheza Disko'!

Binafsi namuona membe kama kiongozi hasipima anasema nini. Nilimsikia siku hiyo akimtaja raisi huyu kijana wa madagasca kama mcheza disco bila kutambua huyu raisi analiongoza taifa huru. Binafsi namuona membe kama asiye na break ktk matamshi yake. Simuoni kama kiongozi makini hata kidogo. Hafai kuwa raisi nchi hii, hana staha!
 
Membe ni mbabaishaji sana,huwa hapimi uzito wa maneno anayotamka,kuna wakati aliwahi kuwakejeli waasi wa libya,ambao sasa ni watawala halali wa nchi ya libya!
 
Membe hana lolote ni mropokaji saana na hayupo systematic na mambo yake binafsi simkubali
 

Hivi kuna kazi/profession ambazo ukiwa nazo hustaili kuwa Rais? Vipi mcheza sinema Ronald Reagan kutawala Marekani?
 
Reactions: FJM
Anakurupuka sana afu baadae analamba matapishi yake, alisema hawezi kuwatambua waasi wa Libya eti hawawezi kuipindua serikali kwa pick up! leo hii yako wapi!@
 
Joka la mdimu ni mutu ya kutomboka maneno ya mingi mbofumbofu.
 
Nasikia ndio mteule 2015. hafai kabisa huyu jamaa
 
Hivi kuna kazi/profession ambazo ukiwa nazo hustaili kuwa Rais? Vipi mcheza sinema Ronald Reagan kutawala Marekani?

Hata ungekuwa makini namna gani, kitendo cha kujiunga na siasa za CCM ni lazima upoteze fikra na uwezo wa kupambanua mambo kwa uhalisia. Ili udumu ndani ya ccm ni lazima hujue kupiga propaganda, ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli bila kujali madhara yake kwani si vyombo vya dola vinawalinda.....!
 
Tatizo la Membe ni sawa na la Zitto kujiona wanajua kila kitu, na wengine hawajui
 
eti membe naye anautaka urais! Jk amefanya nafasi ya urais ionekane so cheap.
 
Hakuna katika ccm mwenye akili timamu, ukimlaumu membe pekee ni kosa, na kwakuwa viongozi wa ccm wana makamasi badala ya ubongo ndio maana nchi sasa ipo shaghalabaghala, mwisho wa yote 2015
 
Unakumbuka maneno yake juu ya waliokuwa wapinzani (waasi?) wa Muammar Ghadaf.
 
Anakurupuka sana afu baadae analamba matapishi yake, alisema hawezi kuwatambua waasi wa Libya eti hawawezi kuipindua serikali kwa pick up! leo hii yako wapi!@

Tanzania na watu wake wa ajabu kweli eti mtu kigeugeu kama membe naye anataka kumrithi kikwete!

Jamani kiti cha uraisi kinataka mtu makini sana sio ujanja ujanja kama watz wengi wanavyofikiria. Nafikiri kuna haja ya kuwata wale wote wanaofikiri kwa moyo wao wote kuwa na dhamira ya kuwania uraisi 2015 wajitokeze hadharani ili umma wa watz uwahoji ni kwanini wanafikiri wanaweza kumrithi mhe. Kikwete. Raisi wa nchi mbali na kuungwa na chama cha siasa husika ni kiongozi wa wote baada ya kutangazwa. Kwahiyo ni vema watu wenye nia njema na nafasi hii wajitokeze mapema ili tuweze kuwahoji ni namna gani wamewiwa kutaka kuwa kiongozi mkuu kabisa wa taifa hili lenye changamoto nyingi na namna gani wako tayari kuzitatua huku wakitakiwa kuonesha wazi mipango na mikakati ya kutufikisha huko kwenye nchi ya maziwa na asali....! Tz ya sasa hatuhitaji raisi ayetanguliza wapenda kumsemea kuwa fulani anafaa kuwa raisi wetu huku yeye ikiwa kimya. Yeyote bila kujali ni kutoka chama gani ajitokeze waziwazi mbele za watz aeleze nia yake njema na watz waanze kupima wenyewe mapema kabla ya uchaguzi mkuu 2015.
 
Membe alipinga pia kupandishwa kwa bendera ya waasi wa Libya katika ubalozi wao hapo Dar! Sasa sijui inapandishwa bendera gani?
 
Aliwakejeli na sasa wanamdai mipesa yao aliokomba wakati wa Gadafi!:huyo ni kinyonga na kigeugeu na hajui siasa za Kitanzania!amezoea ubabe na kutesa alipokuwa TISS!hawezi diplomasia wala siasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…