Picha: Matumizi ya bilioni 10 kwa UDSM kama yanavyoonekana kwa sasa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
Suala kubwa nililojifunza katika siasa za Tanzania ni kuwa na kiongozi shupavu anayesimamia kile anachokiamini na kukiamua.

Tanzania ina wanasiasa wengi wenye ujuzi mkubwa katika kuongea lakini ni zero katika kutenda.

Unamsikia mwanasiasa anakutengenezea kwa maneno bila vitendo Tanzania inayofanana na nchi zilizoendelea.

Tatizo la Tanzania sio ukosefu wa sheria bali ni usimamizi na utekelezaji wa sheria.

Wakati akitoa hotuba yake baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump alisikika akisema, "We will no longer accept politicians who are all talk and no action — constantly complaining but never doing anything about it".

Haya ndio maneno ya Rais Magufuli ambayo kwa sasa yanavyoonekana katika Matendo kwenye viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Haya ni majengo 20 yenye ghorofa nne kila jengo na yana uwezo wa kuhudumia wanafunzi 4,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa haya majengo yameanza kujengwa mwezi Agosti 2016.

C3LEVPIWIAEfzhg.jpg:large
 
Safi sana nategemea zizundiliwe na waziri wa elimu sio Rais kutafuta publicity..............

Rais ni taasisi...........
Unafiki mbaya.....Kwani akizifungua yeye kuna UBAYA gani??hili hali ni yeye aliyeweka JIWE LA MSINGI....tatzo lako ni chuki tu.....na bado msipoangalia TERM HII MAGUFULI mtaugua ugonjwa wa MOYO.......

Mzee wa watu anatekeleza AHADI ZAKE kwa kasi ya ajabu balaa......BILA SHAKA KABSA after two years under him TANZANIA itakuwa mbali mno.....

He is the MAN we have been waiting for..............
 
Mkuu hzo pesa zitakuwa audited na CAG maana tunaweza kuambiwa majukwaani kuwa zimetumika 10b kumbe kiuhalisia zimetumika kama Mara tano yake...si unajua tena mkuu awamu hii tunatafuta kiki kwa kila namna..

Halafu si unajua tena mukulu haojiwi kwa hyo itakuwa ngumu kujua gharama halisi.

Kule simiyu jengo lilitikiwa lijengwe kwa 46b mukulu aliamuru eti lijengwe kwa only 10b nayo nadhani ilikuwa ni kutafuta kiki jukwaani ila kiuhalisia haitakuwa hvo.
 
Mkuu hzo pesa zitakuwa audited maana tunaweza kuambiwa majukwaani kuwa zimetumika 10b kumbe kiuhalisia zimetumika kama Mara tano yake...si unajua tena mkuu awamu hii tunatafuta kiki kwa kila namna..

Kule simiyu jengo lilitikiwa lijengwe kwa 46b mukulu aliamuru eti lijengwe kwa only 10b nayo nadhani ilikuwa ni kutafuta kiki jukwaani ila kiuhalisia haitakuwa hvo.
Mkuu;
Kwa kukusaidia unaweza kuangalia na kusoma kwenye hii tovuti ambayo utakupa majibu ya maswali yako.

National Audit Office
 
Kuna Fundi aliniambia eti kujenga nyumba ya kuishi yenye ghorofa moja ni TZS.300ml.Nikamuambia nasimamia mwenye kila kitu na kununua hadi Sasa tunajiandaa kuezeka imetumika milioni Tshs.90ml. Wabongo tubadilike tuache hesabu za kufikirika na tuache uvivu wa kufikiri.Mheshimiwa Rais namkubali is more practical and critical thinker
 
Kuna Fundi aliniambia eti kujenga nyumba ya kuishi yenye ghorofa moja ni TZS.300ml.Nikamuambia nasimamia mwenye kila kitu na kununua hadi Sasa tunajiandaa kuezeka imetumika milioni Tshs.90ml. Wabongo tubadilike tuache hesabu za kufikirika na tuache uvivu wa kufikiri.Mheshimiwa Rais namkubali is more practical and critical thinker
Hii ni kweli kabsa......maana ndicho ninachokiona kwa upande wangu kwenye hii nyumba yangu.....
 
Kwa kweli anahitaji pongezi!
sisi tunaotoa maoni ktk kupinga yale tunayaona hayako sawa, tulipaswa kuwa wa kwanza kusifia haya mazuri yake!
maana wapo watu wao wanachangia threads za kuponda tu!
Ni jambo zuri sana mh amefanya, nadhani gharama alizotumia sio shida provided hakuna upigaji, maana kwa wazo husika hasa hili la kuboresha elimu, uwekezaji wake inapaswa uwe ndio kipaumbele cha taifa!
BIG UP Mh. Raisi J.p. Magufuli
 
Back
Top Bottom