Picha: Mafundi wasio waaminifu huwapa ramani ya Nyumba Majambazi

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,855
1,530
Picha zilizopigwa location tofauti zikionyesha tukio la wizi uliotokea Dar es salaam, kongowe.

Tukio lilikuwa hivi:

Majira ya asubuhi 3.00 alioneka jamaa mmoja akiruka ukuta na kuingia ndani ya nyumba. Baada ya majirani kuona jamaa akiruka ukuta majirani walitoka na kuzunguka upande wa main gate na kuanza kugonga geti la gari mwizi akatoka na kwenda kufungua mlango, jamaa wakahuhoji yule mwizi, mwizi akasema nimetumwa kufanya usafi. Mmoja kati ya majirani akazunguka dirishani na kumgongea jamaa aliyekua amelala ndani baada ya kupuliziwa dawa, jamaa alipostuka kutoka usingizini wakaanza kumtembezea kipigo kikali mwizi alipoona kipogo kikali akakurupuka na kujifungia ndani mwenyewe. Jamaa alipogoma kufungua mlango simu ikapigwa polisi na raia wakisubiria kwa hamu ya kutaka kuua.

Taarifa za Kiintelijensia

-Inavyosadikika mwizi alikuwa na ramani ya nyumba iliyo na michoro ya vyumba,choo, sebule, idadi ya taa,rangi ya geti n.k

-Taarifa zinaonyesha kuwa baada ya kujifungia ndani alisikika sauti ikiongea na simu ikisema "issue imefeli"

-Mpaka polisi walipofika mwizi alikuwa akipiga mlango kwa mikwala, polisi walipoingia ndani ilisadikika kuwa walimwambia ajifanye amekufa na kumbeba kwenye kitanda.

-Hakuna mlio wa risasi uliosikika
-Raia walipohoji kuhusu ramani iliyo contain ramani ya nyumba zote zilizopo eneo hilo ikiwemo na simu aliyokuwa akifanya mawasiliano alipokuwa chumbani, hakuna mtu aliyejua nani kachukua hata polisi wenyewe, inavyosadikika vilitiwa chooni au vinginevyo.

-Raia walipoomba wabakishiwe mwizi wao polisi walisema mwizi amesha kufa.

Angalizo:

wizi wa kuibiwa vitu vya samani, maarufu kama kusafisha varanda umedouble sana miaka hii na hii inatokana na hali mbalimbali za kimaisha. Taarifa za ki intel ndizo zinazosaidia wizi huu kufanikisha ambazo nyingi huanzia kwa mara ya kwanza nyumba inapojengwa msingi (foundation) na mafundi wasio waaminifu ndio wanao uza ramani za nyumba hizo kwa wahusika.
Screenshot_20161-08-03-11-28-50.png
20160803_100655.jpg
20160803_095516.jpg
20160803_101852.jpg
 
Aiseeeee
Ila inashangaza...kwanini polisi wamuambie alale kama amekufa?Hivi raia wanaweza kumpiga muhalifu aliyeko chini ya ulinzi wa polisi?
Chumba alichojifungia jamaa kilikuwa na choo?
Hata kama...nyumba inaonekana ya kisasa hiyo.Haiwezekani kuwe na choo cha shimo ndani kiasi hadi mwizi atupe simu humo chooni.
Huu ni mtandao mkubwa,ushahidi umepotezwa kinyemela.
 
Wizi unasiri nzito sana.
 
Nilishakutaarifu kuwa, mimi marukufu kupeleka issue yangu polisi, iyo ni sawa na kuwapelekea dili, mimi huwa natafuta nauli baada ya tukio, nikishindwa TANGA naenda Bagamoyo, huwa wanaisoma namba!

Back
Top Bottom