Kwa yaliyotokea Mwanza,naona kama CHADEMA kwa sasa hivi kina sifa zote za kuwa de facto Chama Tawala kwa sababu:-
(1) kina watu makini kwa hoja na mitazamo ya kubadili hali ya wananchi kama
chama tawala kinavyopaswa kuwa.
(2) kinajali kwa dhati matatizo ya watu na kina hoja madhubuti za kuondoa ma
tatizo hayo.
(3) kinasikilizwa sana na watu wengi kila kinapotoa miito yoyote ile kama maa
ndamano.
(4) Kiko upande mmoja kikipingwa na vyama vingine vingi. Kwa kawaida
chama tawala kinakuwa upande wa peke yake kikipingwa na vingine kama
hali ilivyo kwa "Chama Tawala" CHADEMA sasa hivi kinavyoshambuliwa na
"Vyama vya Upinzani" vya CCM,CUF,NCCR Mageuzi,UDP,TLP nk.
Kutokana na nguvu ya ushawishi ya CHADEMA kwa wananchi,CCM inapaswa ikichukulie chama hicho kama taasisi kubwa na nyeti katika mustakabali wa maendeleo na amani ya nchi yetu. Wawe wanazitafakari kwa utekelezaji agenda mbali mbali zinazotekelezeka za chama hicho zinazolenga maslahi ya umma. Wasiichukulie CHADEMA kama kichama fulani hivi cha wababbaishaji kama kile cha jimbo moja na mbunge mmoja! CCM wakitangaza vita na CHADEMA kupinga hoja za maslahi ya umma, kuna hatari kubwa inaweza kutokea kama CHADEMA kitatumia nguvu yake ya ushawishi dhidi ya serikali ya CCM. Ni ushauri tu.