Watanzania wenzangu Tunda linalo itwa Nanasi kwa Tanzania linastawi sana tatizo kubwa la zao hili ni soko nadhani wtz ni mashahidi juu ya hili, Kikwete rais wetu sio lazima akashangae huko Accra juu kilimo hicho cha Mananasi labda akashangae mashine za kutunza hayo matunda. Labda kinachomponza Rais wetu ni kutojipa muda wa kuwatembelea wakulima wa nchi yake na kusikiliza shida zilizopo, Tanzania ina matunda mengi Machungwa, Embe,Mapasheni, Maepols, na mengine mengi yote yanapatikana hapa Tanzania lakini yote haya yanaachwa yaoze wafanyabiashara au serikali wanaagiza Juice toka nchi za Oman,Dubai,South Afrika Maleysia,na nchi nyingine yote haya Ni uwezo mdogo wa kufikiri wa Viongozi wetu wa Tanzania tunalalamika uchumi wa nchi hii unayumba kumbe viongozi wetu kazi yao ni kutalii tu kiongozi wa nchi alienda kuangalia shamba la Nyanya Nje ya nchi akatoka na sifa kemkem juu ya kilimo cha Nyanya amesahau ya kwamba Miaka yote nyanya inalimwa hapa Tz mikoa ya Iringa, Morogoro,Tanga,Mbeya na mikoa hii yote haina soko la kuuzia zao lao hata kujenga kiwanda cha kusindika hili zao la nyanya kiongozi anakaa kulia lia tu, kiongozi ambaye sio mbunifu ni hatari kwa maisha ya wengine angepunguza Safari zake za nje fedha yetu tukanunua mtambo mmoja wa kusindika matunda pengine nchi ingepiga hatua kubwa na pengine shida za wtz zingepungua.