- Tunachokijua
- Uhakiki na uthibitishaji wa picha ni muhimu ili kudhibiti upotoshaji unaoweza kufanyika kupitia maudhui ya picha. Hivyo ni muhimu kujifunza namna ya kutumia nyenzo za kidijitali zinazotuwezesha kubaini uhalisia wa picha.
Uthibitishaji Picha kwa kutumia Google Reverse Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.
Tutumie picha hii ambayo mdau ametaka kufahamu ilipigwa wapi. Picha hiyo inaonesha mandhari ya barabara iliyopita katika mlima mrefu. Je, ilipigwa wapi na lini?
Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini picha hiyo ilichapishwa katika mtandao wa Facebook na kuelezwa kuwa ni kutoka Bujumbura nchini Burundi.
Kadhalika gari inayoonekana barabarani ikiwa upande wa kulia wa barabara inaonesha uhalisia wa madhari ya barabara kutoka nchini Burundi.