Picha: Daktari FAKE MBARONI!

GAMBLER

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2009
Messages
303
Likes
0
Points
0

GAMBLER

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2009
303 0 0
MKAZI wa Ukonga Mombasa, Charles David Shauritanga (31) leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Samora pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kusomewa mashtaka tofauti likiwemo kosa la kujifanya daktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutaka kumfanyia upasuaji mtoto wa Bi. Fatuma Mathayo kwa gharama ya 80, 000/=.
Mtuhumiwa huyo awali alipelekwa Mahakama ya Mwanzo ya Samora na kusomewa mashtaka mawili na Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo, Musa Gumbo, mbele ya Hakimu Janeth Kinyage.
Akiwa mahakamani hapo alisomewa kosa la kwanza la kujifanya daktari na kosa la pili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Baadaye mtuhumiwa alipandishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kusomewa kosa moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo Musa Gumbo mbele ya Hakimu Benjamini Mwakasonda.
Mtuhumiwa alikana makosa yote na kutakiwa kuwekewa dhamana ya 40,000/= na mtu mmoja kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwekewa dhamana na watu wawili kila mmoja mil. 3/= kwa kosa la kujifanya daktari.
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Januari 28 mwaka huu.


‘ARRRROOO SONGA MBERE’
1263474700_1.jpg

Daktari feki (katikati) akisindikizwa na askari polisi kwenda Mahakama ya Mwanzo Samora kusomewa mashtaka yake.
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
7,930
Likes
134
Points
160

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
7,930 134 160
duuh hii mbona inatisha sana.inamana hapo muhimbili usalama wa wagonjwa ni mdogo kiasi cha kwamba mtu yoyote anaweza kujifanya daktari bila wafanyakazi wa hapo hospitali kumgundua? ndio mambo yale yale ya mgonjwa wa mguu kafanyiwa operation ya kichwa na wa kichwa kafanyiwa ya mguu.
 

FM

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2009
Messages
202
Likes
1
Points
0

FM

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2009
202 1 0
Huyu jamaaa inaonekana ndo dili yake. Mwaka jana alikamatwa kwa kosa kujifanya daktari katika hospitali ya Wilaya Mufindi (Mafinga). Mzee alikuwa na digrii fake, cheti cha kumaliza internship fake, barua ya ajira fake, na nyarakanyingine za serikali zote za kugushi. Mpaka sasa sijajua ni mazingira gani yaliyomfanya kuachiwa huru.
 

Forum statistics

Threads 1,190,668
Members 451,284
Posts 27,679,920