Picha Bora kabisa ya wiki.

Tuwe wakweli tuso wanafiki, Huyu Mzee kiukweli alifanya mengi tuliyoyaona na kuyasikia. Alitoa misaada mingi sana kwa walemavu,yatima,masikini,na kwenye sekta ya elimu. Siyo yule mwingine hadi msiba ulifanyika kwa promo na hakuna cha maana alichofanya zaidi ya kuwa Mungu mtu! R. I. P Mzee R.A. Mengi!
 
Picha sharti iseme maneno mengi. Hongera alieinasa. View attachment 1090204

Nadhani Sifa nyingi sana ziende kwa Dereva wa hilo Gari kwani kwa jinsi muda ulivyokuwa umeenda na ratiba ilivyokuwa angeweza kuendesha kwa Kasi hilo Gari ila Dereva alijawa na Hekima kubwa na ya Ajabu mno kiasi kwamba hata alipokuwa akipigiwa ' Honi ' na Gari za nyuma bado alisimama hadi huyu Mlemavu alipojitokeza na Kuligusa hilo Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Mzee Dkt. Reginald Abraham Mengi. Ukimsifia Mwizi kwa Kukimbia sana basi Msifie pia na Yule anayemkimbiza mno.
 
Usitumie nguvu sana kuwaaminisha watu kuwa wewe una fikra kubwa sana au upo tofauti na wengine katika kufikiri. Sometimes chukulia vitu katika uhalisia na urahisi wake maana vitu vingine havihitaji fikra pevu kuliko hisia.
 
Una jicho la tatu mkuu.si rahisi dereva kusimamisha hivyo ukizingatia hao jamaa wenye gari za mbele ndio waongoza msafara.dereva aliguswa pia ndio maana akaona "isiwe tabu..".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…