Pic: MPENDAZOE, LEMBELI, KATAMBI WAITEKA SHINYANGA MJINI

Pic: MPENDAZOE, LEMBELI, KATAMBI WAITEKA SHINYANGA MJINI

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
MONDAY, AUGUST 31, 2015




Mheshimiwa James Lembeli akimwombea kura mgombea urais wa Ukawa mheshimiwa Edward Lowassa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa wakazi wa Shinyanga



Mgombea ubunge jimbo la Kishapu kupitia Ukawa ndugu Fred Mpendazoe akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watanzania kukubali mabadiliko kwani CCM imechoka huku akisisitiza kuwa mgombea urais wa CCM John Magufuli hana kabila zaidi ya kabila la CCM ambayo kamwe haiwezi kutoa rais bora


Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema pamoja na hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa CCM akiwemo mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo Stephen Masele hatakata tamaa kuwapigania haki wananchi na kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya wananchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uenezi kanda ya ziwa Chadema Juma Protas akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ambapo aliwasisitiza wananchi kuchagua viongozi wa Ukawa ambayo ndiyo mwarobaini wa maendeleo ya watanzania
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Msalala Paul Malaika akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema hata kama kuna mgombea mwenye sifa nzuri ndani ya CCM wananchi wasimchague kutokana na kwamba mfumo mzima wa CCM ni mbovu hivyo wafanye mabadiliko kwa kuiweka Ukawa madarakani
Mheshimiwa James Lembeli na fimbo yake ya kimila akimsikiliza kwa umakini zaidi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la Shinyanga
Makamanda wa Ukawa wakiwa meza kuu
Wagombea udiwani kupitia Ukawa katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga wakitambulishwa wakati wa mkutano huo
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano





Posted by Chadema Blogtz at 3:31 AM










 
Ha ha ha steven masele kichwa chini miguu juu
 
safi sana makamanda mwaka huu ni wamabadiliko hakuna kulala
 
Hongera makamanda.

Twendeni bungeni tukaifumue mikataba ya kijinga ya CCM.
 
Hii inaletq Furaha ndani ya moyo, viva UKAWA VIVA CHADEMA
 
Mgombea badala ya kueleza ataifanyia nini Shy iwapo watampa kura yeye muda wote wa hotuba yake anatua adithi za pingamizi. CDM zuzu kabisa
 
Ndio mana walitaka kuchana fomu original wakaambulia feki..hahahaaah
 
Nikimuangalia mtu kama Masha ni aibu sana kwake kusema aliyoyasema wakati akirejea ccm. Mawazo (attitude) ya binadamu ni kama rangi au kimo chake ambapo hakitakiwi kubadilika hadi anapofikia mwisho wake. Mfano Mwalimu Nyerere alipenda haki na aliipigania hadi mwisho wa maisha yake.
Sasa unapomuona mtu ambaye aliwahi kushika nafasi ya waziri nyeti alafu anatoka hadharani na kutuaminisha kuwa baada ya kukaa na kutafakari sana na kushauriana na washauri wake miaka miwili iliyopita na kujiunga na CHADEMA hakuwa na vision ya kilichokuwa mbele miaka miwili mbele!!! Sasa leo tunaweza kumuamini akisema anajua lililo mbele yake miaka mingine miwili ijayo!?
Kweli mtu akivaa suti inaongeza umaridadi na kuficha udhaifu wetu huku vichwa vyetu vikiwa na utata mkubwa.

Taratibu naanza kutilia mashaka na watu waliopewa elimu ya mkoloni kwa wale walioipata.
 
Back
Top Bottom