Phiri, uongozi Simba watofautiana

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SIKU chache baada ya kocha wa Simba, Patrick Phiri kuondoka klabuni hapo akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa madai ya kuuguliwa kwao, Zambia imebainika kuwa kocha huyo amechoshwa na vitendo anavyofanyiwa na uongozi wa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuingiliwa katika upangaji wa timu.

Phiri aliondoka kimya kimya mjini Lubumbashi, Jumapili wakati timu hiyo ikikabiliwa na mechi ngumu ya marudiano dhidi ya TP Mazembe kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuuguliwa.Lakini, habari ambazo Mwananchi imezipata jana zinaeleza kuwa ni kutokana na kufautina na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange 'Kaburu'.

Habari za kuaminika toka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa kocha huyo alianza kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kuambiwa kuwa baadhi ya wachezaji hawatakuwemo kwenye kikosi chake kwa madai kuwa nafasi ni ya wachezaji 18.

"Unajua Phiri alikuwa anataka Banka (Mohamed) aende, lakini uongozi ulimkatalia kwa madai kuwa kiungo huyo aliingia kambini wiki moja tu, Phiri alikuwa tayari hata kwenda na ndege tofauti mradi Banka apate nafasi kwa maelezo kuwa atasaidia timu, lakini uongozi ulimkatalia.

"Kitendo kile kilimuudhi kocha, uongozi wa sasa hivi siyo kabisa, unakuta unampangia timu, anaelezwa mara mchezaji huyu acheze dakika 20, mwingine asicheze, kuna wachezaji kama Mgosi (Mussa Hassan), Nyoso (Juma), Kaseja (Juma) na Banka kuna viongozi hawawakubali kabisa, yaani inawakatisha tamaa hata wachezaji wenyewe,"kilieleza chanzo hicho

"Kwa upande wake, Phiri amekuwa akitofautina nao katika hilo, yeye anaamini hao ni wachezaji wazuri na mwaka jana alikuwa nao mpaka wakachukua ubingwa iweje viongozi leo hii wampangie timu.

"Kocha (Phiri) alikasirika kule Lubumbashi alipofokewa kwa nini amempanga Kaseja badala ya Barthez (Ally Mustapher), unajua kuna viongozi pale wanatumia fedha zao kutaka kunyanyasa wengine, wana wachezaji wao sasa wanaona kama hao wengine wanawabania, inakatisha tamaa sana,"kiliongeza chanzo hicho.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kaburu alisema, "Hakuna kitu kama hicho Phiri ni mwajiriwa na mimi ni mwajiri wake yeye ni mwalimu wa ufundi mimi sijui kitu kama tungekuwa tunajua tusingemwajiri, tumefanya hivyo kutokana na taaluma yake sasa kwa nini tumuingilie?"

"Timu ipo kambini na Phiri anarudi leo (jana), suala lake la kwenda kwao aliomba ruhusa toka tupo Arusha na tulimkubalia, hakuna mtu ambaye anampangia timu kama kuna kiongozi anamuingilia mwalimu majukumu yake basi hafai kuwa kiongozi, sisi Kibaden (Abdallah) tumetaka kumwongezea Phiri nguvu ili amsaidie, na hakuna kiongozi yoyote aliyegombana na kocha wala kumwingilia katika majukumu yake,"alisisitiza.

Juzi, uongozi wa Simba ulikaririwa ukimtangaza Kibaden kuchukua mikoba ya Phiri ambaye walidai amekwenda Zambia kumuuguza mke wake. Timu hiyo itarudiana na TP Mazemba Aprili 2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kwenye mechi yao ya awali mwishoni mwa wiki iliyopita walifungwa mabao 3-1
 
Timu ipo kambini na Phiri anarudi leo (jana), suala lake la kwenda kwao aliomba ruhusa toka tupo Arusha na tulimkubalia, hakuna mtu ambaye anampangia timu kama kuna kiongozi anamuingilia mwalimu majukumu yake basi hafai kuwa kiongozi, sisi Kibaden (Abdallah) tumetaka kumwongezea Phiri nguvu ili amsaidie, na hakuna kiongozi yoyote aliyegombana na kocha wala kumwingilia katika majukumu yake,"
 
timu ipo kambini na phiri anarudi leo (jana), suala lake la kwenda kwao aliomba ruhusa toka tupo arusha na tulimkubalia, hakuna mtu ambaye anampangia timu kama kuna kiongozi anamuingilia mwalimu majukumu yake basi hafai kuwa kiongozi, sisi kibaden (abdallah) tumetaka kumwongezea phiri nguvu ili amsaidie, na hakuna kiongozi yoyote aliyegombana na kocha wala kumwingilia katika majukumu yake,"

asante kwa hiyo post: Umeleweka kiongozi.
 
Back
Top Bottom