Philipo Mwakibinga: Nitagombea uenyekiti BAVICHA

Philipo Mwakibinga: Nitagombea uenyekiti BAVICHA

Dj-kobo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
458
Reaction score
193
Habari zenu wana-JF.

Bwana Mwakibinga kupitia ukuta wake wa fesi buku ametangaza rasmi kuwa atachukua fomu ya kugombea uenyekiti BAVICHA taifa.

Ikumbukwe huyu bwana alifukuzwa chuo kikuu cha UDOM kufuatia mgomo aliouitisha 2011 akiwa rais.

Kwa maoni yangu huyu kijana anafaa.
 
Namie nachukua fomu nagombea.

Ni haki ya kila mwanachama.

Kwa maoni yangu, nafaa
 
Ooh! nafahamu huyu jamaa bwana ana misimamo yake ambayo haiyumbi na anasimama kwenye haki...ni mwaka wetu 2011 ambapo ndo alifukuzwa chuo lakini ilikuwa sababu ya wengine wapate haki yao..na haki yetu kweli ilipatikana japo jamaa walimtosa chuo sijui yupo wapi kwa sasa na anafanya nini?....
 
Ni haki yake,nimtakie tu kila la kheri katika kutimiza ndoto yake ya kutuongoza vijana kupitia bavicha
 
alifungua kesi mahakamani na akashinda kwani alifukuzwa kinyume cha utaratubu,na pia inasemekana chuo kikuu cha dodoma kimemlipa pesa nyingi kama fidia.Hivi sasa karudishwa chuo na ni waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi katika kitivo cha sayansi ya jamii na sanaa udom..
Jamaa mkali
 
Namkubali sana huyu kamanda mkombozi wa UDOM lakini Ben Saanane anatosha.
 
Last edited by a moderator:
anafaa sana uzuri wake anajiamini na hagopi mtu . lkn kuhusu chuo mwaka huu karudi na amemaliza tayari
 
Ooh! nafahamu huyu jamaa bwana ana misimamo yake ambayo haiyumbi na anasimama kwenye haki...ni mwaka wetu 2011 ambapo ndo alifukuzwa chuo lakini ilikuwa sababu ya wengine wapate haki yao..na haki yetu kweli ilipatikana japo jamaa walimtosa chuo sijui yupo wapi kwa sasa na anafanya nini?....

mwaka jana karudi na amemaliza chuo na yupo katika harakati
 
Katika wote wanaogombea bavicha,Anaetakiwa ni mmoja tu ammbaye co mnafiki,usaliti ni mwiko katika kundi lenye lengo moja.(Ushauri ktk chama viongozi waendelee kuisimamia katiba mtu anaevunja katiba kwa maslai binafs chama kisisite kumchukulia hatua kali za kikanuni,ikiwa pamoja na kufukuzwa,kujitoa kwenye chama ,Na waende huko kwenye chama (Godauni) la wasaliti.yani ACT
 
Namkumbuka huyu mkaka kwa misimamo yake yani hayumbishwi hata kidogo
 
Back
Top Bottom