Pettiness

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,493
Reaction score
145,853
Marehemu Senator McCain alikuwa anaheshimiwa sana na watu wengi.

Lakini naona kama vile amekufa na vinyongo moyoni mwake.

Kabla hajafa alisema wazi kuwa hataki rais Trump ahudhurie msiba wake.

Ni wazi yeye McCain na Trump zilikuwa haziivi.

Ila kwa nini afe na kinyongo namna hiyo? Hiyo kwa kweli ni weakness kubwa sana.

Kafa Jumamosi iliyopita. Trump akatoa tamko la kawaida tu.

Bendera ikashushwa nusu mlingoti White House. Jumapili jioni ikarudishwa juu.

Watu wakalalamika, licha ya kwamba sheria ilifuatwa kama ilivyo.

Jumatatu jioni ikashushwa tena nusu mlingoti baada ya watu kulalamika na kumshutumu Trump.

Si vizuri kumlaumu marehemu ila McCain naye alichangia huo mkanganyiko.

Mtu unajua unakaribia kufa halafu unasema hutaki rais wa nchi ahudhurie msiba wako Halafu watu wategemee rais akupe heshima ambazo watu wanadhani unastahili?

Kama hiyo haitoshi, McCain huyo huyo hakutaka hata Sarah Palin, mgombea mwenza wake, ahudhurie msiba wake!

Huyo mzee alikuwa na kinyongo sana na amekufa nacho. Sad

Palin not invited to McCain's funeral: report
 
Wewe ndo huwa unasemaga USA baby? ahahahhaha. Jenga nchi yako hachana na hayo mashetani mkuu
 
Hapo kwa McCain hata mimi nafikiri alikosea sana hasa tukizingatia kuwa alikuwa ni mwanasiasa na kiongozi, mtu ambaye anapaswa awe mfano wa kuigwa katika kuleta umoja katika jamii licha ya mafarakano yaliyomo. Ila kwa sababu naye ni binadamu tukubali tu hiyo ilikuwa weakness yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Twaib!
 
Kumbe iyoo kansa niya kutengeneza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahaaa haaa haaa
Mbona naye Trump alisema ANAPENDA KUONGEA NA WATU AMBAO HAWAJAWAHI TEKWA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…