ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 658
Mshikaji akiwa safarini kapoteza Pete ya ndoa. Anasema aliingia chooni kujisaidia. Akaivua akaitundika kwenye bomba ili wakati wa usafi isichafuke. Sasa alipotoka akaisahau, alipokumbuka akarush msalani hakuikuta. Kitu carrat tatu za gold hata mimi ningechukua. Sasa kaniuliza utaratibu wa kuvaa nyingine siufahamu. Eti, anunue nyingine avae tu? Anunue akavalishwe tena mbele ya padri? Anunue avalishiwe chumbani tu na wife huku akitoa ahadi ya kuvumiliana mpaka kifo kiwatenganishe? Au afanyeje? Serious!!!