Pete ya dhahabu yenye kidani chekundu

Pete ya dhahabu yenye kidani chekundu

Heisenberg

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2017
Posts
1,688
Reaction score
2,981
DISCLAIMER: Nianze kwa kusema hii story sio ya kwangu, ni ya member fyddell ambae amesimulia hii story ndani ya story

👇👇👇👇👇

Hivyo nimeona nisaidie kuweka hapa iwe peke yake ili irahisishe usomaji na ufuatiliaji maana imeleta shida sana kwa wasomaji mbalimbali. Kwa ruhusa yako mkuu fyddell naomba niandike hii story kwa hapa kama itakupendeza
Ukwaju Citizen B Naki 12 Joannah na wengine wote karibuni

Naamini kuwa uchimbaji wa madini ya dhahabu unaendana na majini coz mdogo wangu aliokota pete ya dhahabu ina kidani chekundu juu yake baada ya dada wa kiarabu kufungua pochi yake ili atoe nauli na ile pete ikadondoka kwenye siti akiwa anaongea na konda huku akichokonoa chokonoa pochi yake. Dogo baada ya kuichukua alishuka kituo kinachofuata na break ya kwanza kwa bro wake ambaye ni mimi.

Sijui nami niseme nitaendelea Kama mkuu Kitoabu? Basi bhana, baada ya kunieleza nikatoka nae mpaka kwa sonara wa kihindi. Yule sonara baada ya kumuonesha tu alipandisha mashetani, eh alipoanza kupiga kelele kwa maneno ya kiarabu na kutimua mbio na watu wengine wote waliokuwepo pale jumlisha na sisi wote mbio huku nimeishikilia mkononi.

Tukakaa sehemu na mdogo wangu nikimhoji maswali huku nami nikianza kuiogopa ile pete. To cut the story short tukaenda kwa sonara mwingine Kariakoo naye ni muhindi ofisi yake ikiwa inanuka ubani tupu, alipoiangalia akatuuliza mmeipata wapi huku akitukazia macho.

Hapa nikaona yasijeyakatokea yaleyale ya kule Ila imani yakupata pesa ilikuwa imenijaa nikamkazia kwa kumdanganya kuwa mama ametupa tuje kuiuza kwasababu anaumwa. Akatuangaliaa Sana huku akiiangalia Ile pete, bila kuipima wala nini akasema nawapa laki 5 na elfu alobaini. Aisee sikutegemea, mi nilijua tutauza laki ikizidi sana laki moja na nusu, Sasa kusema laki tano nikakubali fastaa...

Mchezo uliishia wapi?
Basi nikazigawanya zile hela mule mule dukani, nikampa dogo laki mbili zingine nikabaki nazo Mimi. Nikamwambia we pita njia yako nami njia yangu hata Kama tunafuatiliwa tusipokonywe yote na usinunue chochote nikukute home. Baada ya makubaliano mi nikashika njia yangu na dogo nae yake, nikaenda duka flani kununua carpet ya manyoya, nikanunua na subwoofer na vitu vingine vidogo dogo vya kupendezesha chumba na nikabakiwa na chenji kazaa nikarudi home.

Usiku tumelala dogo akashtuka kelele mtindo mmoja huku akining'ang'ania mimi, tukakimbia mpaka sebureni. Nyumba nzima watu wakaamka, nami nimejawa na hofu tele huku sijui nini kimempata dogo. Akawa anaulizwa anaweweseka huku akisema kuna mwarabu mzee amekuja akakaa kitandani anataka, hasemi anaogopa.

Mama na mzee wakasema ameota huyu rudini mkalale. Baada ya kukazimishwa na kuingia room tukapanda kitandani yaani nilikuwa mpaka nausikia moyo wa mdogo wangu ulivyokuwa ukimdunda huku akitetemeka nami nikajawa na hofu kuwa hapa Kuna kitu na si ndoto kama wazazi walivyosema. Dakika kumi nyingi, nikashangaa gafra mdogo wangu kaniruka kuja mwisho wa kitanda ukutani. Ile kuangalia tunapopandia kwenye kitanda kwa macho yangu tena kukiwa na giza nikamwona mtu amevaa kanzu nyeupe akiwa na mandevu kibao akifunua neti like naye apande kitandani.

Aisee kelele nilizopiga hazikuwa na mfano

Basi yule mtu akapotea, hapo niko juu ya mdogo wangu wote tunang'ang'ania kule mwisho ukutani mbali na pale tilipomuona yule mtu akifunua neti. Watu wakaja chumbani, awamu hii baba alikuja na silaha mama na majirani wanaume watatu wakatukuta tunalia mbaya.

Waliingiwa na imani ya uwepo wa hali si ya kawaida kwasababu mara ya kwanza mdogo wangu ndio alipiga kelele, mara ya pili na ukubwa wote wa kuwa mwaka wa kwanza chuo Udsm nipige kelele vile?! Kingine kilichowashangaza wazazi ni kutokuwepo kwa huyo mtu ndani na wao ndio wamefungua mlango, pili mabadiriko ya chumba ya vile vitu ambacho nilivinunua kupitia Ile hela ya pete bila wao kujua maana hatukuwaambia (kwa vitu hawakujari sana kwasababu nilikuwa na boom though nilikuwa nakaa main campus ila week end narudi home coz sio mbali na chuo)

Wote tukaenda sebureni na kusimulia nilichokiona, walipokonekti na aliyoyasema dogo mara ya kwanza wakaona hapa kuna jambo. Majirani zetu ni waislamu, mmoja akasuggest wasome dua kufukuza kitu kibaya alafu asubuhi tupelekwe sehemu. Kwa kipindi like sikujua wanamaanisha sehemu gani, nilikuwa kujua baadae. Wamemaliza kusoma wanatuambia turudi chumbani tukalale hakuna kitakachotokea tena...weee nani akubali? Mi nikapinga nakusema bora nikae macho hapa hapa sebureni mpaka asubuhi kule chumbani sirudi, hiyo ni mida ya saa tisa kasoro usiku.

Nifupishe. Ilipofika asubuhi pamoja na ukristo wao wazazi wetu lakini walikubaliana na mzee mmoja jirani yetu watupeleke kwa shekhe mmoja hivi. I can't differentiate him with mganga ila ye anachora chora kwenye karatasi alafu anawaambia nini hasa kilichotokea, kilichopo na nini chakufanya.

Yule shekhe ndio akaanza kusema, aisee over alikuwepo na mdogo wangu kwa jinsi alivyokuwa anasimulia mpaka sonara wa kwanza kupandisha majini maana alikutana na jini lenye nguvu kuliko yeye likamuonya. Kumbe kile kidani chekundu juu ya pete ni jini lilikuwa limewekwa kwenye mfumo wa kidani kwenye Pete ya dhahabu kwaajili ya kazi za yule mwanamke (Hapa sitaingia into details maana hayahusu hii simulizi). Akamtaja mpaka jina la hilo jini kuwa hatatuacha kwasababu tumempeleka sehemu (kwa sonara yule wa pili) amefukuzwa so anatufuata sisi tumrudishe sijui wapi yule shekhe alisema.

Sisi tukaombewa ombewa pale na yule shekhe alafu tukapewa dawa ya kuoga kwa siku saba yaani unaichanganya kwenye maji ya kuoga. Sisi tukatolewa nje ndani wakabaki baba, yule mzee aliyemshauri baba twende kwa huyo shekhe na shekhe mwenyewe wakijadili jambo.

Tuliambiwa ile dawa tuoge asubuhi na usiku kabla ya kulala na kunuia maneno flani ya kumfukuzia yule kiumbe. Ile laki mbili alivyokuwa nayo dogo baba aliamua kumpa yule shekhe (sijui aliitumia au aliichoma moto kama alivyodai? Vile vitu vingine shekhe alivifuata nyumbani ili akavichome Moto pia). Sasa ilipofika usiku wa ile siku mimi na mdogo wangu wote tunaogopa kwenda kulala chumbani. Hiyo ni j'tatu na chuo sikwenda kwa hofu ya lile dude kunitokea chuoni nikiwa peke yangu, pamoja na kupewa Ile dawa na kile kisomo bado nilikuwa nimejawa na hofu so nilitaka kuwa karibu na baba maana yeye ndio alikuwa anaonekana jasiri kuliko wote.

Mama yeye baada ya kusimuliwa na mzee aliyosema yule shekhe alibaki kulia na kuomba tu huku akimwomba (kumlazimisha mzee atupeleke kwa Kakobe). Usiku ilipofika baba akaamua kulala na sisi chumbani, kwakweli usingizi haukuja, mapigo ya moyo yapo juu, nikimwangalia dogo nae dogo ananikodolea macho tukiwa kitandani mzee kalala chini, pembeni ya kitanda. Mida ya Kama saa saba sijui saa sita (sikumbuki muda sahihi) usingizi ukatupitia, nakuja kushtuka.

Baada ya kushtuka usiku nilihisi baridi sana likitambaa kwenye mwili, kuangalia chini alipolala baba hayupo. Hofu iliongezeka ndani yangu nikifikiria yule mzee anaweza akaja tena na tuliyokuwa tunamtegemea ni baba kuwepo pale. Nikamuamsha mdogo wangu ili kujipa moyo wa uwepo wa pamoja katika hali niliyoihisi.

Nikawa nasikia sauti mtu akilia na kusema "siondoki mpaka mnipe (Kuna neno lilitajwa ambalo sikulijua) vinginevyo nitaendelea kuwafuatilia mpaka wanirudishe kwa (akataja jina jingine la kike, nadhani ni jina la yule mwanamke aliyedondosha Pete). Nikamuuliza dogo unamsikia huyo mtu anayelia? Sauti inatokea wapi? Hakuna aliyekuwa na jibu kwasababu sauti ilikuwa inajaa madikioni mwangu bila kudhihirisha sehemu inayotokea, yaani ni Kama vile nimevaa earphone alafu mtu aongee.

Yule shekhe Kuna maneno alituambia kuwa tukiona Hali ambayo hatuielewi tuyatamke hayo maneno. Nayakumbuka lakini hapa sitayataja. Basi nikaanza kuyatamka yake maneno huku nikitetemeka mdogo wangu akilia kwa kwikwi. Bila kujielewa tulipitiwa na usingizi na kushtuka asubuhi kumeshakucha. Ile Hali haikujirudia kwa muda wa siku tano yaani it was like nothing happened before.

Sasa nilikuwa nimesharudi kwenye hali ya kawaida na chuo nilikuwa nikienda na kufurahi na washkaji kama kawaida bila kuwaambia kwanini siku tatu sikuwepo mazingira ya chuo. Ile siku ya sita nilisahau kuoga Ile dawa kuanzia asubuhi mpaka jioni, kilichokuja kutokea usiku wakati natoka seminar room kujisomea haaa.

Itaendelea kadili jamaa atakavyopost
 
Uwiii...nipo kusubiri muendelezo...@fyddell ankoli usinisahau please
 
Samahani naomba kuuliza tofauti kati ya kidani na kito? Inaniwia vigumu kuelewa pete ya dhahabu na kidani chekundu.

Kito ni kitu chochote kitokanacho na madini yenye thamani.

Kidani kimsingi hutumia kutambulisha kitu cha kuning'niza shingoni.

hapa imetumika kimakosa. ilitakuwa iwe pete ya dhahabu yenye kito chekundu.

ambacho ni Obvious Rubi
 
Kito ni kitu chochote kitokanacho na madini yenye thamani.

Kidani kimsingi hutumia kutambulisha kitu cha kuning'niza shingoni.

hapa imetumika kimakosa. ilitakuwa iwe pete ya dhahabu yenye kito chekundu.

ambacho ni Obvious Rubi
Shukran kwa ufafanuzi.
 
Hahah aise unatakiwa ututengeneezee fiction character kama shelecko Holmes maana izi stori za uganga uwaga ndo zile zile

Tunaitaji character alie na uwezo wa kufikiri sio uwezo wakichawi

Tumechoka sasa....
 
Samahani naomba kuuliza tofauti kati ya kidani na kito? Inaniwia vigumu kuelewa pete ya dhahabu na kidani chekundu.
Bado nawasifu waliotuletea habari hii inaeleweka hata kwa mtoto mdogo, kuwa pete ya dhahabu ina jiwe jekundu (Ruby) katikati
1605521769487.png
1605521798370.png
 
Kito ni kitu chochote kitokanacho na madini yenye thamani.

Kidani kimsingi hutumia kutambulisha kitu cha kuning'niza shingoni.

hapa imetumika kimakosa. ilitakuwa iwe pete ya dhahabu yenye kito chekundu.

ambacho ni Obvious Rubi
Shukran kwa ufafanuzi.
Bado nawasifu waliotuletea habari hii inaeleweka hata kwa mtoto mdogo, kuwa pete ya dhahabu ina jiwe jekundu (Ruby) katikati
View attachment 1627597 View attachment 1627598

Ni hadithi nzuri, nami nimeona nifahamishwe kuwa kinachokaa juu ya pete ya dhahabu mara nyingi huwa ni kito cha madini chenye thamani, sasa kusoma kuhusu pete ya dhahabu yenye kidani chekundu, nikaona labda ndiyo miongoni mwa maajabu ya kijini ya hiyo pete. Lakini kwa ujumla wake ni hadithi nzuri na inamafundisho ndani yake.
Hakuna mkamilifu.
 
Kito ni kitu chochote kitokanacho na madini yenye thamani.

Kidani kimsingi hutumia kutambulisha kitu cha kuning'niza shingoni.

hapa imetumika kimakosa. ilitakuwa iwe pete ya dhahabu yenye kito chekundu.

ambacho ni Obvious Rubi
Oh ok ni kito na si kidani. Asante kwakunielewesha mkuu
 
Shukran kwa ufafanuzi.

Ni hadithi nzuri, nami nimeona nifahamishwe kuwa kinachokaa juu ya pete ya dhahabu mara nyingi huwa ni kito cha madini chenye thamani, sasa kusoma kuhusu pete ya dhahabu yenye kidani chekundu, nikaona labda ndiyo miongoni mwa maajabu ya kijini ya hiyo pete. Lakini kwa ujumla wake ni hadithi nzuri na inamafundisho ndani yake.
Hakuna mkamilifu.
Asante kwa kunielewesha. Nilishindwa kung'amua kuwa kile ni kito zaidi ya kuita kidani.
 
Back
Top Bottom