Mkuu pete gani hiyo ya elfu ishirini? nakumbuka mimi nilinunua pete mwaka 2010 na gram moja ya gold ilikuwa inauzwa elfu 60, sasa utahitaji japo gram tatu na kwa sasa nadhani itakuwa bei iko juu zaidi, andaa angalau kuanzia laki mbili ndo unaweza kupata pete ya maana kidogo.