Pesa za majini

baba stive

Member
Mar 10, 2016
11
10
Kumekuwa na watu wenye bahati ya kupata pesa nyigi sana kwa wakati mmoja kwa mfano pesa za migodini kwenye madini, pesa za kuokota, mirathi, pesa za zawadi, pesa za kilimo cha mazao ya biashara (pamba, tumbaku nk), pesa za warina asali, pesa za wachana mbao, pesa za kiinua mgongo na pesa mikopo na kwa ujumla hizi ni pesa zinazopatikana kwa bahati au kipindi maalumu au baada ya kusota sana. Toka ninakua nmekua nikisikia kuwa pesa hizi huwa haziwezi kukaa kwa mmiliki wake hata ukijengea nyumba lazima utaiuza na watu wengi wamekua wakiamini hivyo na kuigeuza kuwa ni pesa za kupita tu na kutanua kwa anasa.

Rafiki yangu mmoja Musa Anael mchimba madini huko Geita aliwahi niambia "pesa ya mgodini ni ya kula tu na kutanua kwa sababu haijengi wala haifanyi maendeleo" Lakini hata wanafunzi wa elimu ya juu wanaopata mikopo wanaamini pesa ile haiwezi kufanya chochote zaidi ya kuliwa na kuisha kwa kigezo kuwa haitoshi na jamii inaamini mambo haya kwa kiasi kikubwa.

Hapo maswali yanakuja, je hakuna watu waliofanikiwa kupitia njia hizo hizo? kama pesa za mirathi hazikai humfuata mwenye nazo mbona Akina Mohamed Dewji pesa hazijawafuata baba zao? nikakumbuka suala la viinua mgongo jinsi wazee wanavyokufa mapema baada ya kuzipata pesa hizo na kwisha ndani ya mda mfupi, sasa nkajiuliza mbona hapa kuna mkanganyiko? watu wengine wanasema pesa hizo hazikai lakini wapo wachache wanaofanya maendeleo kupitia pesa hizo za bonus.

UTAFITI

Katika kutafiti kupitia watu waliowahi pata pesa hizo na kuwaishia mikononi nikagundua kuwa watu wengi hatuna ELIMU YA PESA namaanisha kuwa kabla hatujaanza kutafuta pesa tulitakiwa kuwa tushapata elimu ya kukabiliana na homa ya kupata pesa nyingi kwa mda mchache ili kuepuka kutokuchanganyikiwa na kuja kukumbuka kupanga mipango pesa imekwisha.

Hii naiona kwa sasa makampuni mengi yanayotoa zawadi kwa wateja wao hutoa ELIMU YA UJASIRIAMALI kwa washindi na ndipo huwapa pesa hizo kwa mfano TMT na AIRTEL Hii yote ni kumwandaa muhusika kisaikolojia kuweza kukontrol pesa yake lakini huko America msanii Justine bieber kabla hajaanza kazi rasmi ili kukabiliana na changamoto kama hizi na zile za umaarufu familia yake na manejimenti yake kwa pamoja walimtafutia shule kupata elimu kuhusiana na kazi yake.

Tabu inakuja kwetu hapa kwamba hatuna mpango wa kujipa elimu hii au elimu ya suala lolote tunalotaka kulifanya na ndio maana tunapopata pesa nyingi huishia kuinywea pombe na kulala kwenye mahotel ya kifahari bila kujua kuwa hakuna chanzo kingine cha pesa hizo.

Mimi naamini kila mtu anaweza kukaa chini na kujipa elimu ya pesa kupitia mitandao na vitabu au kuhudhulia semina zinazohusiana na mambo haya na pia ni jukumu la mzazi kumwandaa mtoto kutokuamini kuwa kuna pesa haziwezi fanyiwa maendeleo badala yake watoto wafundishwe jinsi ya kuishi na pesa na kuibajeti wakiwa bado wanakua na ili waepuke homa ya pesa.

Lakini pia tuache kuiga waliofeli katika kufanyia maendeleo pesa hizo. Kushindwa kwao kumesababishwa na matatizo binafsi hivyo jiangalie wewe unaweza kufanya kipi na tuache kuamini kila tunachokisikia na watu hawa wengi wanaoamini hivi wanatoka tabaka letu hili hebu tuachane na mila hizi na imani potofu na tufanye kazi kufahamu kuwa pesa ni pesa inahitaji kuheshimiwa ili ikae sasa tujaribu tuone kama pesa hii haikai.

by
MELKIZEDECK BASHINGWA
MTANZANIA
19/03/2016
 
Back
Top Bottom