Pesa si chochote, si lolote

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Dunia imejaa pilika pilika za usiku na mchana, watu hatulali, hatuli tukashiba, tunauana, Tunafungana, Tunajeruhiana, Tunachukiana, hakuna kabisa Upendo baina yetu.
Ukiuliza ni Kwa nini yote hayo yanatokea? jibu ni Kwa Sababu ya pesa, pesa ni hatari Sana, Wanadamu tunaamini kuwa ukiwa na pesa ndo umemaliza maisha yote, Tumemsahau Mungu wetu, akili zetu na nguvu zetu zote zipo ktk kutafuta pesa kuliko kumtafuta MUNGU, yaani kufanya ibada.
Sisi wanadamu ni wajinga, ni wapuuzi kabisa, huwa tunajiona tuna akili sana na tunaona mbali sana kumbe ni zero brain kabisa.
Muda mwingi tunatafuta pesa ambazo mwisho wa Siku tunakufa na kuziacha, na huko tuendako baada ya kifo kuna maisha tofauti na ya hapa duniani.
Tunapenda pesa wakati pesa haiwezi ku.....
1.Kuzuia kifo
2.kununua Upendo /amani na furaha
3.kukuepusha na magonjwa pamoja na majanga mengine
4.kukupatia miaka mingi ya kuishi duniani
5.kukufanya uwe karibu na MUNGU

Hayo ni machache Kati Ya mengi sana ambayo pesa haiwezi kukufanyia.
Kwa mantiki hiyo, pesa ina thamani gani zaidi ya kuwa mtego wa Shetani?
Tujitathimini Sana na tumtafute MUNGU kuliko pesa.
 
Mkuu Ciprofloxacin

Hakika umeandika mada nzuri sana. Yaani sisi wanadamu tumejikuta tupo kwenye mtego wa shetani "pesa"

Utakuta mtu amebarikiwa kuwa na nyumba zake mbili, lakini roho ya kipepo inamuingia na kuanza kuiba pesa, na anajenga Nyumba zingine 10.

Mungu kwa kumfundisha, hiyo Kazi anafukuzwa, kesi juu, Nyumba zinafilisiwa na kufungwa anafungwa.

Wanadamu tujifunzi kuwa na kiasi na kushukuru na zaidi ya yote tutumie muda wetu mwingi kuwa karibu na Mungu. Na tusiwe watumwa wa pesa.
 
Ndiyo maana bwana wetu Yesu Kristo katika maandiko kwenye Biblia alinukuliwa akiwaambia wanafunzi wake kuwa tajiri kuuona ufalme wa mbinguni, nafasi yake ni finyu mno, sawasawa na uwezekano wa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!

Matajiri walio wengi ni maajenti wa shetani, kwa kuwa wanatumikia na kuabudu mali badala ya kumtumikia na kumwabudu Mungu aliyewaumba na kuwapa hiyo neema ya kupata utajiri.

Matajiri walio wengi hawazifuati amri kuu 2 za Mungu, ambazo ni zile zinazosema mpende Mungu wako kuliko kitu chochote na ya pili ambayo inafanana nayo ni ile inayosema mpende jirani yako kama nafsi yako .
 
Tafuta vyote pesa na Mungu......Mungu alikua na maana kusema mtakula kwa jasho lenu. Kumtafuta Mungu pekee bila pesa inaweza ukafikia kipindi ukamkufulu hata huyo Mungu. Hebu pata picha u mgonjwa waumwa mfano malaria unadhani ukiamini kwa Mungu unapona? Ni lazima uende hospital umpatie dokta pesa ndipo akutibu.....Wachungaji na makanisa wanakusanya pesa kwa ajili ya sadaka kwanini na wakati wao wanamtegemea na kumuhubiri Mungu? Tusidanganywe na kuwa vipofu kwa jina la Mungu maisha bila ya kuwa na pesa hayaendi.....fanya kazi upate pesa na at the same time unaomba na kusali....."Asiefanya kazi na asile"
 
Nilipokuwa mdogo naamkia wakubwa zangu na kupewa pesa. Sasahivi wale wakubwa zangu wananiamkia mimi na kuwagaiya pesa. Bila ya Pesa heshima hakuna. Hivi ukipata mualiko kwa Sheikh au Pastor na kwa Bakhresa wapi utakwenda?
 
Dunia imejaa pilika pilika za usiku na mchana, watu hatulali, hatuli tukashiba, tunauana, Tunafungana, Tunajeruhiana, Tunachukiana, hakuna kabisa Upendo baina yetu.
Ukiuliza ni Kwa nini yote hayo yanatokea? jibu ni Kwa Sababu ya pesa, pesa ni hatari Sana, Wanadamu tunaamini kuwa ukiwa na pesa ndo umemaliza maisha yote, Tumemsahau Mungu wetu, akili zetu na nguvu zetu zote zipo ktk kutafuta pesa kuliko kumtafuta MUNGU, yaani kufanya ibada.
Sisi wanadamu ni wajinga, ni wapuuzi kabisa, huwa tunajiona tuna akili sana na tunaona mbali sana kumbe ni zero brain kabisa.
Muda mwingi tunatafuta pesa ambazo mwisho wa Siku tunakufa na kuziacha, na huko tuendako baada ya kifo kuna maisha tofauti na ya hapa duniani.
Tunapenda pesa wakati pesa haiwezi ku.....
1.Kuzuia kifo
2.kununua Upendo /amani na furaha
3.kukuepusha na magonjwa pamoja na majanga mengine
4.kukupatia miaka mingi ya kuishi duniani
5.kukufanya uwe karibu na MUNGU

Hayo ni machache Kati Ya mengi sana ambayo pesa haiwezi kukufanyia.
Kwa mantiki hiyo, pesa ina thamani gani zaidi ya kuwa mtego wa Shetani?
Tujitathimini Sana na tumtafute MUNGU kuliko pesa.
Amina
 
Tafuta vyote pesa na Mungu......Mungu alikua na maana kusema mtakula kwa jasho lenu. Kumtafuta Mungu pekee bila pesa inaweza ukafikia kipindi ukamkufulu hata huyo Mungu. Hebu pata picha u mgonjwa waumwa mfano malaria unadhani ukiamini kwa Mungu unapona? Ni lazima uende hospital umpatie dokta pesa ndipo akutibu.....Wachungaji na makanisa wanakusanya pesa kwa ajili ya sadaka kwanini na wakati wao wanamtegemea na kumuhubiri Mungu? Tusidanganywe na kuwa vipofu kwa jina la Mungu maisha bila ya kuwa na pesa hayaendi.....fanya kazi upate pesa na at the same time unaomba na kusali....."Asiefanya kazi na asile"
Anamaanisha tusibase Sana kwenye pesa tukamsahau Muumba wetu . Ndo manake
 
Mungu anapenda watu wake tuwe na pesa wala usidanganyike ila anataka uzipate kutoka kwake maana anasema "utajiri na heshima viko mikononi mwake" na ukimtii atakupa utajiri wa mataifa.
Pesa si shida ila unavyozipata na kuzitumia ndo inaweza ikawa shida.
Watu wa Mungu mtafute pesa jaman la sivyo mtajikuta mnashindwa kukemea dhambi kwa watu wenye pesa.
 
We
Dunia imejaa pilika pilika za usiku na mchana, watu hatulali, hatuli tukashiba, tunauana, Tunafungana, Tunajeruhiana, Tunachukiana, hakuna kabisa Upendo baina yetu.
Ukiuliza ni Kwa nini yote hayo yanatokea? jibu ni Kwa Sababu ya pesa, pesa ni hatari Sana, Wanadamu tunaamini kuwa ukiwa na pesa ndo umemaliza maisha yote, Tumemsahau Mungu wetu, akili zetu na nguvu zetu zote zipo ktk kutafuta pesa kuliko kumtafuta MUNGU, yaani kufanya ibada.
Sisi wanadamu ni wajinga, ni wapuuzi kabisa, huwa tunajiona tuna akili sana na tunaona mbali sana kumbe ni zero brain kabisa.
Muda mwingi tunatafuta pesa ambazo mwisho wa Siku tunakufa na kuziacha, na huko tuendako baada ya kifo kuna maisha tofauti na ya hapa duniani.
Tunapenda pesa wakati pesa haiwezi ku.....
1.Kuzuia kifo
2.kununua Upendo /amani na furaha
3.kukuepusha na magonjwa pamoja na majanga mengine
4.kukupatia miaka mingi ya kuishi duniani
5.kukufanya uwe karibu na MUNGU

Hayo ni machache Kati Ya mengi sana ambayo pesa haiwezi kukufanyia.
Kwa mantiki hiyo, pesa ina thamani gani zaidi ya kuwa mtego wa Shetani?
Tujitathimini Sana na tumtafute MUNGU kuliko pesa.
ll said mdau watu wanaitolea macho pesa kuliko hata kuangalia kuwa maisha yanamwisho
 
Back
Top Bottom