Pep Guardiola rasmi Man City

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mhispania Pep Guardiola ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja mpya wa Manchester City.

Guardiola, atachukua majukumu hayo kuanzia Julai, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imetangaza.

Manuel Pellegrini ataondoka klabu hiyo Juni 30.

"Kutokana na heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kufanya wazi uamuzi wake ili kuondoa nafasi ya uvumi,” City wamesema kupitia taarifa kwenye tovuti yao.


Chanzo: BBC
 
...aende tuone kama atawapeleka nusu fainali ya champions league,thn awape na ubingwa wa Epl.
 
What if Pellegrini joins Man Unite after Van Gaal?
 
Mwisho wa Pep, sioni kama atakutana na watu wenye vipaji kama clubs alizotoka!

Huyu jamaa ni master wa kukusanya mishiko...!
 
Hawa City wamemkosea heshima sana Pellegrin. Imagine bila aibu wamekiri ati walianza mazungumzo na Pep tangu mwaka 2012. Japo siwapendi City, natamani sasa Pellegrin afanikiwe kuchukua EPL na Champions League ili Pep aje na challenges za kuachive hayo makitu.
 
Pep sasa umaarufu wake utashuka so fast
EPL ni ngumu sana
vitimu vidogo tu vinakuumbua
 
Ndipo ataelewa kwamba uingereza wanacheza watu au ng'ombe

Pep mbio za sakafuni mwisho ukongoni

Karibu uingereza karibu kucheza rugby
 
Pep hawezi kufanikiwa EPL angetuliza kipago kama mwenzake Lonely Mess...
 
Pep hawezi kufanikiwa EPL angetuliza kipago kama mwenzake Lonely Mess...


Kwanini Pep kachagua City? Kwasababu they can buy any player he wants. Mafanikio ya Pep always yanachangiwa na timu anazofundisha. Full squad ni wachezaji mahili. Pep anakuja kubadilisha mpira wa Uingereza.
 
hahahahahahahahaha aiseee i cant wait for this,the special one angekuepo epl ingenoga hatari sana.....goood news the best coaches wapo sehemu moja sasa
 
Haiwezi kuondoa motisha ya Pellegreni katika kipindi hiki muhimu? City wako nyuma ya Leicester kwa point 3 kwenye EPL, wako 16 bora ya UCL, wako fainali ya Capital one cup, wako 16 bora ya FA Cup.

Naona City wamechemka vibaya kutoa taarifa hii muda huu. Itawacost sana; Pep alijiandaa kuondoka Baryen kitambo ila Manuel hajaandaliwa, hivyo hii taarifa ni mshtuko kwake & pigo kwa City. Time will tell!
 
Hawa City wamemkosea heshima sana Pellegrin. Imagine bila aibu wamekiri ati walianza mazungumzo na Pep tangu mwaka 2012. Japo siwapendi City, natamani sasa Pellegrin afanikiwe kuchukua EPL na Champions League ili Pep aje na challenges za kuachive hayo makitu.
utaishia kutamani ila haitawezekana labda epl
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom