People's power ni hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

People's power ni hatari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Wasema hata watoto wao wamegeuka
  [​IMG] Chadema waanza rasmi kutumia chopa  [​IMG]
  Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, Siyoi Sumari


  Siasa za kushutumiana, kupakana matope zimeendelea kutawala kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha na safari hii, wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Akeri, wakiwalalamikia walimu wa shule za msingi na sekondari kwamba wamekigeuka chama hicho na kushabikia Chama cha

  Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwafundisha wanafunzi wao kutumia msemo unaotumiwa na Chadema wa

  'people’s power'

  Kadhalika, wazee hao wamelaani wafuasi wa Chadema, kwa kupiga yowe kwenye mikutano ya kampeni na kila wanapoona wafuasi wa CCM waliovalia sare za chama.

  Wakizungumza na waandishi wa habari katika tawi la CCM la Patandi lililopo eneo la Tengeru, wazee hao walisema jana kuwa mila na desturi za Kimeru zinazua yowe kupigwa bila sababu hasa kama hakuna msiba, lakini inashangaza kuona

  kwamba hata watoto wadogo wanapiga yowe na kuonyesha alama ya vidole viwili pindi wanapoona wafuasi wa CCM.
  Mweyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM Kata ya Akeri, Ndewariyo Kaaya, alisema: “Inasikitisha kwamba hadi watoto

  wadogo wa shule wakiona mtu amevaa nguo zetu (CCM) wanapiga yowe kitu ambacho ni kibaya kwani ni uchuro na ni laana mbaya sana, labda pengine serikali yetu itusaidie.”

  “Tunatukanwa hadi na watoto wadogo kabisa, ukipita wanasema ‘people’s power’ na kuonyesha vidole viwili,” aliongeza mzee huyo.

  Mzee Benard Kaaya, mjumbe wa Kamati ya Siasa katika kata hiyo, alisema sehemu kubwa ya watu wanaopiga yowe ni vijana pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kuwataka wazazi wawakanye watoto wao kushiriki jambo hilo.

  “Walimu tena hapa sekondari ya Akeri, badala ya kuwafundisha watoto wetu masomo, wanawafundisha ‘people’s power’, wanawafundisha siasa, hebu tukemee vitendo hivi jamani, nawaomba mabalozi mliopo hapa tusiruhusu yowe tena kwenye kata yetu,” alisema Mzee Kaaya na kuongeza: “Hata leo asubuhi watoto wadogo wamenionyesha alama ya Chadema.”

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) tawi la Akeri, Luyana Sikawa, alisema: “Hawa walimu wamesahau kwamba wapo kwenye ajira ya CCM, wametugeuka na hawapo kabisa na sisi, hili ni jambo baya sana.”

  Alimlaani mgombea wa Chadema, Joshua Nassari, kwa kutangaza kwamba atafuta ushuru unaolipwa mara mbili mbili kwenye soko la Tengeru akieleza kwamba tangazo lake limeibua vurugu sokoni hapo.

  “Mgombea wa Chadema asilete vita pale sokoni, amekuwa akitangaza kufuta ushuru kitu ambacho hakiwezekani, yeye ametamka pale sokoni matokeo yake nimekuwa nikizomewa kila mahali ninapopita, watu wananipigia yowe kila wanaponiona,” alisema Sikawa, ambaye pia ni mwenyekiti wa soko hilo.

  LEMA AONYWA TENA


  Mzee Kaaya alimwonya mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, akimtaka asikanyage Arumeru Mashariki kwa kuwa wazee watawaamuru vijana wa CCM wampige. “Lema aache tabia yake ya kuchochea vita na tunamwambia asije hapa, maana atapata janga na tunasema kabisa akija hapa atapigwa kweli,” alisema.

  CHADEMA YAANZA KUTUMIA HELIKOPTA


  Chadema kimeanza rasmi kutumia helikopta katika mikutano kampeni huku Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, akiendelea kuishutumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kudai kuwa Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ameanza vibaya kwa kuchakachua daftari la wapiga kura.

  Hayo aliyasema jana alipokuwa akihutumbia mikutano wa hadhara katika vijiji vya Ngurudoto, Ngarananyuki na Sakila, huku umati mkubwa wa watu ukiwa umezunguka eneo hilo wakiangalia helikopta iliyoanza kutumika jana.

  Alisema kuwa Nec imeanza mtihani huo vibaya kwa kutoa daftari jipya la wapiga kura, ambalo limechakachuliwa na kuongezwa vituo hewa zaidi ya 50.

  “Kama hawatarekebisha hili, safari hii hatutakubaliana na hili suala la kuibeba CCM kwa wazi, mtageuza Arumeru kuwa chanzo cha machafuko kama ilivyo Tunisia,” alisema.

  Dk. Slaa aliongeza kuwa mbali na kuchakachua daftari hilo, pia Nec iliwapatika CCM barua ya orodha ya wapiga kura siku saba kabla, lakini wao na vyama vingine hawajapata wakati wako katika orodha moja ya kucheza mpira wa uchaguzi.

  “Hivi inawezekanaje mpira unachezwa pamoja wa Simba na Yanga, halafu timu moja inapendelewa na refa, alafu wengine wakaangaia tu, lazima itatokeo vurugu, kuepuka hili Tume iangalie maana tumewashitukia,” alisema Dk. Slaa.

  Aidha, alisema ni vema kama serikali walitaka CCM ishinde uchaguzi huo na nyingine, vema wasingeleta uchaguzi kiini macho kwani wanavifunika mablanketi vyama vingine kwa lengo la kuipa ushindi CCM.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alimjibu Mkuu wa Operasheni ya Uchaguzi wa Jeshi la Polisi, Isaya Mngulu, kuwa yeye amesomea sheria na hajasomea siasa na hakuna shule ya kusomea siasa.

  “Huyu Mngulu anasema eti kama tunataka Polisi tuachie wenyewe waliosomea sababu sisi tumesomea siasa, mimi namwambia siasa haisomewi bali nilichosomea sheria na nikachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama, ila mimi kilio changu Polisi watende haki na sio kuibeba CCM,” alisema.

  NASSARI AJINADI


  Mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari, aliomba kupigiwa kura, ili awe mbunge wa wananchi atakayetatua kero zao zilizoshindikana kwa miaka 50 ya Uhuru.

  Nassari pia aliwaambia wapiga kura wake kuwa hawahitaji uchawi Arumeru wala muujiza wowote, bali wanahitaji mkombozi wa kweli, ambaye ni yeye mwenye dhamira madhubuti ya kuwatoa wananchi kwenye hatua moja kwenda nyingine.

  SIOI AOMBA KURA


  Mgombea wa CCM, Sioi Sumari, ameahidi kutatua kero mbalimbali, ikiwemo ya kuiboresha shule ya sekondari ya wasichana ya Songoro.

  Sioi alitoa ahadi hiyo wakati akiomba kura katika vijiji vya Mulala, Songoro, na Sura. Alisema kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwemo upungufu wa vifaa vya maabara na kwamba wamchague ili kusimamia uboreshaji wa shule hiyo kwenda kwa wakati.

  “Mkinipa ridhaa ya kuwa mbunge wenu nitahakikisha nasimamia uboreshaji wa shule ya Songoro na mradi huu unakamilika kwa wakati,” alisema.
  Alisema pia atahakikisha anasimamia ukamilishaji wa ujenzi ya zahanati iliyopo kijiji cha Mulala kwa kuwa tayari fedha zimetengwa kwa ajili ya kumalizia zahanati hiyo.

  NEC: FANYENI KAMPENI KWA UTULIVU

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imevitaka vyama katika jimbo la Arumeru Mashariki kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu na kufuata maadili na kanuni za uchaguzi.

  Nec pia imesisitiza kutofanya uandikishaji upya wa wapiga kura katika jimbo hilo badala yake litatumika daftari lililotumika mwaka 2010.

  Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lubuva alisema kampeni za uchaguzi zikiendeshwa kwa amani na utulivu hata siku ya kupiga kura wananchi nao watakuwa huru kwa kumchagua kiongozi wamtakaye.

  “Vyama vyote tuliwekeana saini ya kuendesha kampeni kwa amani na utulivu na watafuata maadili ya Tume ya Uchaguzi, pasipo kuwa na matusi yoyote, hivyo navitaka vyama vyote kulizingatia hilo,” alisema Jaji Lubuva.

  Lubuva aliongeza kuwa Tume imebaini kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika daftari la uandikishwaji katika uchaguzi wa 2010 hivyo kutafanyika marekebisho kwa ajili ya uchaguzi wa sasa Arumeru Mashariki, lakini hakutakuwa na uandikishaji upya.

  Alisema Tume imeshafanya marekebisho hayo na kuwaingiza wapiga kura 54 ambao taarifa zao haziwepo katika daftari la wapiga kura na kubaini wapiga kura 28 waliojiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  WANAHARAKATI WATUMA WAANGALIZI


  Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) kimepeleka timu ya waangalizi wa katika Jimbo la Arumeru Mashariki kama utafanyika katika mazingira huru na haki bila ukiukwaji wa haki za binaadamu.

  Mratibu wa Uchaguzi kituo cha Sheria wa LHRC, Merick Luvinga, aliliambia NIPASHE kuwa timu hiyo iliondoka jana kwenda Arusha.
  Alisema leo atatoa idadi kamili ya wamaharakati waliokwenda sambamba na maeneo ambayo watasambazwa.

  Imeandikwa na Restuta James, Charles Ole Ngereza, Cynthia Mwilolezi, Arusha, Gwamaka Alipipi na Emmanuel Kimweri, Dar.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. paty

  paty JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  wazee wanaona wao pekee ndo wana haki ya kushabikia siasa , vijana wakishabikia etii oooh wanatuttukana kwa kutuonyesha alama ya Y
   
 3. O

  Original JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuoneshwa vidole viwili imekuwa tusi?, Gadaffi alitiwa vijiti matakoni.
   
 4. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani wanatukanwa au wanapewa ukweli? Maana kuishabikia ccm kwa sasa inakupasa uwe na akili ya maiti.
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  hawa wazee hawajawaona wale wazee wa EAST AFRICA COMMUNITY walivyoteswa? Hawajui hata baba wa taifa walimuua?
   
 6. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vidole viwili ni alama ya amani na ushindi....kama wazee hawataki mabadiliko basi ni bora wawe waathirika wa mabadiliko....peoples power ni sauti na Nguvu kubwa ya Umma...
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye Avata yako nzuri naomba useme NCHI HII IMEUZWA NA CCM. PLEASE

   
 8. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...mwendo mdundo vijana wa Arumeru,shikilieni hapo hapo na ikiwezekana ongezeni spidi ya kuvizomea hivyo vizee vya m.a.g.a.m.b.a mpaka kieleweke aka mpaka m.a.g.a.m.b.a yavuke..."WAACHENI WATOTO/VIJANA WAJE CHADEMA MAANA HILI TAIFA NILAO"...
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mama yangu alijivua gamba kutokana na kitendo cha mwanangu (mjukuu wake) kupiga mayowe kila amwonapo amevaa nguo za ccm,
   
 10. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wazee wanatakiwa kujua kwamba kumbe wamebaki CCM kwa sababu ya mazoea.
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 521
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Leo nimeamini kweli kuwa mtaji wa CCM ni wazee na wajinga
   
 12. m

  maramojatu Senior Member

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ikiwezekana na akina mama watembee na vijiko na sufuria kila wakikutana na mafisadi wavigonganishe. Tufanye hivyo mpaka ufisadi uishe. Hawa magamba hawana maana. Kwanza wazee wa meru wote wanapenda cdm
   
 13. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hao wazee sioni kama kuna jambo hata moja walilolalamikia lenye mantiki,watoto kuonyesha alama ya V si kua walimu ndio wamewafundisha,kuna vyombo vya habari n.k lazima wajue kua watoto wa leo wako faster kupambanua jambo kias kua si rahisi kuchotwa akili na ujinga wa c.c.m,pili zee zima tena kiongozi wa jumuia mojawapo ya chama linawalaumu walimu kua wamewageuka eti walimu wamesahau wako hapo kwa ajili ya c.c.m!what a shame,sasa mzee kama huyo ukimuita i**** utakosea?mwngne anakuja anasema ushuru sokoni hauwezi punguzwa,what a shame,ni masoko mangapi ambayo wafanyabiashara wamepga kelele na ushuru kupunguzwa,mfano soko la mwenge,makumbusho,kilombero n.k,hawa wazee wa c.c.m sijui uwa wanawazaga nini kabla ya kutoa kauli zao!
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  People power inakua kwa kasi ya ajabu, hata mimi nashangaa. Nafikiri wenye makosa ni CCM.
   
 15. t

  tweve JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 696
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ukiwa mshabiki ama mwanachama wa ccm ni lazima akili iwe imechanganyikana na kinyesi
   
 16. k

  kinyambani Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.(peooples power.....)
   
 17. h

  hans79 JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Hao wazee wanazuzuka na vijisenti vya uchaguzi wanajisahau uchaguzi ukiisha hakuna tena wa kuwajali ndo panakuwa kilio cha kusaga meo,mara nilirubuniwa mara najutua kuchagua ccm.waache njaa zao waungane na ukweli utawale,maisha bila ufisadi wa ccm + magamba yao yawezekana.
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  mtoto wangu wa Miaka mitano amesema haipendi CcM baada ya kumwona Wassira
   
 19. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Ukiichunguza picha vizuri, utagundua huyu mwenye shati la kijani anafurahi mwenyewe, lakini waliomzunguka karibu wote wamenuna. Hii ni hatari sana kwa huyo mwenye shati la kijani
   
 20. d

  dada jane JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndo kazi pekee tulichoamua walimu ni kukomboa fikra za haya makinda ya njiwa hakuna cha TUCTA wala CWT. Uwiiiii.
   
Loading...