Pension za wastaafu za kila mwezi kutoka hazina mpaka leo tarehe 4 May hazijalipwa, je,zimepelekwa sikukuu ya wafanyakazi?

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
16,296
21,381
Pension za wastaafu za kila mwezi kutoka hazina mpaka leo tarehe 4 May hazijalipwa. Je,zimepelekwa sikukuu ya wafanyakazi Mei Mosi?

Hakuna asiyejua adha ya wastaafu,hasa wale wanayopata pension zao za kila mwezi kutoka Hazina.Pension yao ni kidogo mno,na kupigia kwenye bandiko hili,ningeshauri pension hizi ziongezwe, ili angalau zifikie Sh.450,000 kwa mwezi, kwa maana ya Sh.15,000 kila siku.Hela hiyo haitoshi kumuwezesha mstaafu kuishi,lakini angalau ikifika Sh.450,000, itamuwezesha kupata mahitaji ya msingi.Naomba niseme wazi ukweli huu kwamba,kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania,hii inawezekana kabisa na hata zaidi,shida ni wizi,matumizi mabaya ya fedha na kuifanya nchi yetu kuwa shamba la bibi.

Lakini naomba pia nizungumzie swala la malipo ya pension hizi za wastaafu kutoka Hazina.Pension hizi ni ndogo sana kama ambavyo nimeainisha,lakini malipo yanakumbwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kulipwa kwa pesion zenyewe.Inawezekana kabisa malipo ya pension hizi yanachelewa kwa sababu nilizokwisha zitaja hapo juu, yaani wizi,matumizi mabaya ya fedha na kuifanya Tanzania kuwa shamba la bibi,mambo ambayo hayana budi kudhibitiwa.

Vyovyote vile iwavyo,pension hizi zinapaswa kulipwa kwa wakati,hasa kwa vile ni ndogo sana.Unamlipa mstaafu kiduchu,halafu kama hiyo haitoshi, unamcheleweshea kumlipa,hapana ni mbaya,ni kukosa utu,unfair na lack of moral values.

Mwisho niseme hivi, tatizo hili limekuwa sugu hasa kunapokuwa na sherehe za kitaifa,hii si mara ya kwanza.Mbona mishahara ya wafanyakazi inalipwa kwa wakati,hata kukiwa na sherehe za kitaifa,kwa nini isiwe hivyo kwa wastaafu?Hii ni dharau kwa wastaafu,ambao wamelitumikia taifa letu kwa muda mrefu,na jambo hili halipaswi kuwa entertained.Wafanyakazi wa hazina wanaowafanyia wastaafu uovu huu, wakumbuke kwamba ipo siku nao watastaafu.
 
Pension za wastaafu za kila mwezi kutoka hazina mpaka leo tarehe 4 May hazijalipwa. Je,zimepelekwa sikukuu ya wafanyakazi Mei Mosi?

Hakuna asiyejua adha ya wastaafu,hasa wale wanayopata pension zao za kila mwezi kutoka Hazina.Pension yao ni kidogo mno,na kupigia kwenye bandiko hili,ningeshauri pension hizi ziongezwe, ili angalau zifikie Sh.450,000 kwa mwezi, kwa maana ya Sh.15,000 kila siku.Hela hiyo haitoshi kumuwezesha mstaafu kuishi,lakini angalau ikifika Sh.450,000, itamuwezesha kupata mahitaji ya msingi.Naomba niseme wazi ukweli huu kwamba,kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania,hii inawezekana kabisa na hata zaidi,shida ni wizi,matumizi mabaya ya fedha na kuifanya nchi yetu kuwa shamba la bibi.

Lakini naomba nizungumzie swala la malipo ya pension hizi za wastaafu kutoka Hazina.Pension hizi ni ndogo sana kama ambavyo nimeainisha,lakini malipo yanakumbwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kulipwa kwa pesion zenyewe.Inawezekana kabisa malipo ya pension hizi yanachelewa kwa sababu nilizokwisha zitaja hapo juu, yaani wizi,matumizi mabaya ya fedha na kuifanya Tanzania kuwa shamba la bibi,mambo ambayo hayana budi kudhibitiwa.

Vyovyote vile iwavyo,pension hizi zinapaswa kulipwa kwa wakati,hasa kwa vile ni ndogo sana.Unamlipa mstaafu kiduchu,halafu kama hiyo haitoshi, unamcheleweshea kumlipa,hapana ni mbaya,ni kukosa utu,unfair na lack of moral values.

Mwisho niseme hivi, tatizo hili limekuwa sugu hasa kunapokuwa na sherehe za kitaifa,hii si mara ya kwanza.Mbona mishahara ya wafanyakazi inalipwa kwa wakati,hata kukiwa na sherehe za kitaifa,kwa Nini isiwe hivyo kwa wastaafu?Hii ni dharau kwa wastaafu,ambao wamelitumikia taifa letu kwa muda mrefu,na jambo hili halipaswi kuwa entertained.Wafanyakazi wa hazina wanaowafanyia wastaafu uovu huu, wakumbuke kwamba ipo siku nao watastaafu.
Mkuu umetema madini matupu.

Kwanza ulishasikia hata mbunge mmoja akalisemea hilo Bungeni?

Mstaafu hana mtu wa kumsemea popote pale, ni kama condom iliyokwisha kutumika, maana hata mtumiaji aliyeitumia huionea kinyaa.

Ni utawala wa Kikwete pekee kwa wastaafu uliookoa 'jahazi' kwa kuwaondoa kutoka kwenye 'jinamizi' la kusubirishwa miezi 6, aliwaongezea na kuigeuza kusubirishwa miezi 3 then ikawa ya kila mwezi ilivyo sasa.

Tukija kwenye muktadha wa mada yako, aliyekuhabarisha kakupotosha kwa kukusudia ama kwa kutokukusudia kwa sababu zifuatazo:

Pensheni za hazina zililipwa trh 24/4/24 siku moja baada ya watumishi wa Serikali kulipwa mishahara yao, huo ndiyo ukweli.

Nikija kwenye: 'kuto kukusudia' ni kwamba pesa hizo wastaafu wengi waliingiziwa kwenye A/C zao kimya kimya bila notification za benki, hivyo kufanya wengine kukaa hadi siku 2 bila kujua hadi walipokuja kushituliwa na wenzao
.
Sielewi tatizo ni nini kwa mabenki kuingiza pesa kimya kimya kwa wastaafu kwa mtindo huo.
 
Alichoandika yupo sahihi,kuna Mini Pension inalipwa na hazina hadi jana tarehe 03/05 saa 12 jioni ilikuwa haijatoka mara nyingi huwa inapishana na hii ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa siku moja au mbili wakati mwingine inatoka siku moja.
 
Mkuu umetema madini matupu.

Kwanza ulishasikia hata mbunge mmoja akalisemea hilo Bungeni?

Mstaafu hana mtu wa kumsemea popote pale, ni kama condom iliyokwisha kutumika, maana hata mtumiaji aliyeitumia huionea kinyaa.

Ni utawala wa Kikwete pekee kwa wastaafu uliookoa 'jahazi' kwa kuwaondoa kutoka kwenye 'jinamizi' la kusubirishwa miezi 6, aliwaongezea na kuigeuza kusubirishwa miezi 3 then ikawa ya kila mwezi ilivyo sasa.

Tukija kwenye muktadha wa mada yako, aliyekuhabarisha kakupotosha kwa kukusudia ama kwa kutokukusudia kwa sababu zifuatazo:

Pensheni za hazina zililipwa trh 24/4/24 siku moja baada ya watumishi wa Serikali kulipwa mishahara yao, huo ndiyo ukweli.

Nikija kwenye: 'kuto kukusudia' ni kwamba pesa hizo wastaafu wengi waliingiziwa kwenye A/C zao kimya kimya bila notification za benki, hivyo kufanya wengine kukaa hadi siku 2 bila kujua hadi walipokuja kushituliwa na wenzao
.
Sielewi tatizo ni nini kwa mabenki kuingiza pesa kimya kimya kwa wastaafu kwa mtindo huo.
Mkuu hapa umechanganya kidogo.Ni kweli pension za mifuko ziliingizwa, hilo halina shida,kiasi ambacho hakikuingizwa ni pension kutoka hazina.Huwa serikali nayo inamchangia kiasi fulani mstaafu,hiki ndicho kiasi ambacho hakijaingizwa.
 
Alichoandika yupo sahihi,kuna Mini Pension inalipwa na hazina hadi jana tarehe 04/05 saa 12 jioni ilikuwa haijatoka mara nyingi huwa inapishana na hii ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa siku moja au mbili wakati mwingine inatoka siku moja.
Asante mkuu,hili ndilo tatizo hasa nililokuwa nalenga.Wasifanye hivi,it is wrong.Wastaafu nao ni watu,kwa hiyo kuwafanyia hivi si sahihi,it is wrong na ni dharau.

Ninalo wakumbusha watu wa hazina wanaohusika na swala hili ni kwamba, ipo siku nao watastaafu,sasa sidhani kama watajisikia vizuri waki-nyanyapaliwa namna hii.Ni vizuri wakajijengea mazingira ya kuja kujaliwa na kuheshimiwa watakapo-staafu.
 
Back
Top Bottom