aliekwenda magazetini ni Pengo sio polisi
Lile gari ni mali ya kanisa ndugu usipende kukurupuka ukadhani unaongea jambo la maana mbele za watu. Ni kama yale magari ya ikulu, ukiondoka unayaacha pale unless tuamue kukuzawadia. Hata chakula anachokula pale kinalipiwa na kanisa, njoo na lingine hilo la gari ni la jikoni.
Hakwenda magazetini, alikuwa anaongea na vijana kwenye misa ya ufukweni.
Na umekimbilia kujibu kasentensi kamoja ili tu kuukimbia ukweli kuwa CCM ina lake katika hili. Mimi nilikupa na mfano wa Lowassa kukuonesha kuwa hakuna uhakika wa mambo yanayozungumzwa na CCM na vibaraka wake. Nikukumbushe jambo: Katika uchaguzi wa mwaka kama sio 1995 basi ni ule wa 2000, Kamanda Mahita alitoa tuhuma nzito dhidi ya CUF kuwa wameingiza nchini kontena la majambia ambayo yatagawiwa misikitini ili kufanyia vita. Unaweza kunipa muendelezo wa jambo hili?
Tusiwe wepesi wa kuwa fooled namna hii. Kama Askofu anatuhuma basi haikuwa sahihi kuzieneza, la muhimu lilikuwa kumuweka ndani kama wahalifu wengine. Huu ni uhuni tu ambao watu wenye akili zetu tumeshaubaini. Na wanaongea uhuni huu kwa kujua kiwango chetu cha kufikiri ni kidogo na ndio maana wengine wameanza hata kuona gari analotembelea Askofu kalinunua kwa pesa ya madawa, wakati lile ni mali ya kanisa. Tuwe wenye kufikiria ili tuweze kutoka hapa tulipo.
Waliothibitika kuwa wameiba kina Jairo wapo pale tunatend kuwasahau, huku akili zetu tunazielekeza kwenye uzushi. Walituambia Lowassa ni fisadi, mpk leo yupo uraiani kazi kubweka bweka kama mbwa koko, sitawaamini kwa maneno. Nitaamini nikiona Askofu kakamatwa na kufikishwa mahakamni kwa hilo. Tunaangamia kwa kukosa akili
Haswaa,wala hujakosea! Wangapi wanamkumbuka Leonard Bhonke mhubiri wa kimataifa? Alikuwa anakusanya maelfu ya watu viwanja vya wazi,pia alihubiri live kwenye radio na tv akiwa uwanjani,lakini akanaswa na shehena ya madawa ya kulevya. Kikwete kwenda kuwaambia maaskofu kuwa viongozi wa dini waache kuuza madawa ya kulevya we unadhani alikurupuka? Na alipopewa masiku ili akanushe au adhibitishe na yeye kukaa kimya ulidhani yeye *****? Alijua akiwasema hadharani kuwa ni fulani na fulani hali ya nchi itakuwa hatarini kwani watu wa madawa hujipanga kwa njia zote. Mfano ikipangwa JK auwawe,na mpango ukafanikiwa basi ujue yale ya Rwanda yatakuja Tanzania lakini itakuwa baina ya Waislam na Wakristo.
Kwanini anatajwa tajwa kwamba anauza unga??
Don't be pathetic. Suala la madawa ya kulevya si swala la wakristo na waislamu ni swala la MUHALIFU na DOLA. Ukianzisha ujinga wa kidini ktk ishu inayoweza kuangamiza jamii ni upuuzi. Hakuna mkristo wa kumtetea askofu ikiwa anauza madawa ya kulevya. Kama hilo ni kweli ni wajibu wa serikali kutuepusha nalo. Rais kusimama majukwaani kuongea utumbo wa namna ile si dalili za utendaji.
Ngoja nikuulize swali wewe unayetaka kuleta udini usio na mpango hapa: Ukigundua kuwa Imam wa msikiti wenu anajihusisha na vikundi vya ugaidi utanyamaza Watanzania wafe kwa kuwa huyo ni muislamu mwenzio au utaripoti tukio ili kuepusha maafa kwa jamii yako?
Nani kakurupuka? Mimi au wewe? Soma uelewe nini kimendikwa siyo kukurupuka tu. Mimi wala gari analotumia Mhashamu Policarp Kadinali Pengo silijui. Mantiki ya post yangu ilikuwa kumdhihaki jamaa aliyejibu post yangu kuwa Vague. Mimi nikasema gari la kifahari? Nikiwa na maana hiyo vague alikuwa akimaanisha Vogue? Najue vague ni kwamba haieleweki nami nikajifanya sielewi! Wapi nimesema anatumia gari la kifahari? Acha kukurupuka na kujifanya wewe ndio mkatoliki namba one. Mimi mwenzio ni mwenyekiti wa baraza la walei parokiani kwangu.Lile gari ni mali ya kanisa ndugu usipende kukurupuka ukadhani unaongea jambo la maana mbele za watu. Ni kama yale magari ya ikulu, ukiondoka unayaacha pale unless tuamue kukuzawadia. Hata chakula anachokula pale kinalipiwa na kanisa, njoo na lingine hilo la gari ni la jikoni.
Tusiende kanisani, hili ni suala la kisiasa. Wakati mahita anasema CUF wameleta kontena la majambia ili wagawe misikitini, uliuliza kwa nini CUF? Ilikuwa ni kweli? Tumia akili yako vyema kaka, sio kila kitu tukielekeze kwenye udini. Tukiwa wenye kusahau yaliyotupata jana, kesho yatatupata tena. Mtuhumiwa hatajwi tajwi, anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mimi (kwa akili yangu) niliona kwamba, kama CUF walishukiwa kufanya vile, basi polisi wasingesema jambo hilo hadharani. Wangeweka mtego wamkamate huyo mwenye kontena wakati anaanza kugawa kwenye misikiti. Lkn kwa kuwa ni propaganda, ilitangazwa nia na madhumuni kuteka akili za watu. Leo hii kama askofu anauza madawa, haikuwa kazi ya Rais kumshtua ili apate muda wa kuficha ushahidi. Ilikuwa ni kazi ya polisi kufanya uchunguzi kimya kimya na kumtia mbaroni na kumfikisha mahakamani na afungwe kama wahalifu wengine. Sasa huu tunaoonge ahapa ni ujinga unaoletwa na elimu ndogo ya siasa. We are happy to be fooled
Kanisa lina hela nyingi sana hadi za anasa? wakati waumini wake kule sumbawanga wanakanisa la makuti
Pengo ana issues zake nyingi sana, ya madawa sidhani ila kiimani kama umetenda yasiyofaa lazima uweweseke, na kama ameiona na haikua public notice au hakuwa contacted formally je haoni kwamba tayari ameingia kwenye magam??
aisee
Mufti anafilisi
Pengo anabwabwaja
ndinaliyooo
kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, sasa kama mtu anasimama kutetea drug dealers wanaotumia jina la kanisa kwa nini na yeye asiwemo kwenye list? wewe wadhani alihamishiwa kagera kwa mazuri? ni mengi yangelipuka kama angeendelea kaa hapa dsm. all in all, pengo aache unafiki, urafiki wake wa karibu na drug dealers watia mashaka. may be wote wanachonga michongo pamoja....who knows....? watu hawawezi just list him without knowing his involvement.
Wewe ulimuamini Mahita au uliamini maelezo ya CUF at that time??
Ukweli ni kwamba leo unajidai kwamba una sympathazy na CUF kumbe ulikuwa upande wa Mahita;
Kibao kilipoanza kugeuza kwenu....
Unatakiwa uwe consistent
Kanisa lina hela nyingi sana hadi za anasa? wakati waumini wake kule sumbawanga wanakanisa la makuti
asante aisee
hata mimi siamini kama anaweza husika na madawa
but najua he is not as innocent as he wants people to believe
yupo kama mwanasiasa hivi...
anachokifanya sasa ni 'kuchochea hisia za kuwa serikali ya Kikwete ina ugomvi na makanisa'
ndo maana 'anaropoka kwa makusudi'
yeye anajua kazi ya polisi ni kukusanya taarifa za kweli na za uwongo
kabla ya kuchambua na kuzifanyia kazi..
kama hujakamatwa....unaweweseka ili iweje?
mbona Mama Rwakatare licha ya jina lake kuwemo na kutangazwa sana
kiasi cha yeye kwenda polisi kuuliza kama ni kweli yupo kwenye ubunge still????
Kama nilikuwa upande wa Mahita, basi nilikuwa mjinga na nilikosea. Sasa niambie ni busara gani zinazokuongoza kutumia ujinga wangu wa jana kuhalalisha ujinga wako wa leo? Mtu mwenye busara hutumia makosa ya wengine kurekebisha mienendo yake. Sioni unachotaka tubishanie hapa. Nini ni muhimu kwako kama Mtanzania, mawazo yangu au uhalisia wa mambo katika lililopo mbele yetu?