Pengo mfukuzeni kanisani Mizengo Pinda

Pengo mfukuzeni kanisani Mizengo Pinda

Status
Not open for further replies.
Hakika wapenda haki wote tumeumia kiongozi huyu alaanike na damu zote za wenye haki zimlilie kumbe ni chui ndani ya ngozi kondoo na watu wote waseme, amina
 
Hakuna haja ya kukimbilia kwa pengo, mbona mafisadi pengo hajawatenga?

"To know the enemy is half the victory"

Zaka na sadaka wanazotoa makanisani kwao wakiondolewa, mtazitoa ninyi??? Hapendwi mtu bali zaka na sadaka wanazotoa!!
 
Ambao wanapinda sheria waache washughulikiwe tena washughulikiwe ipasavyo. Vita ya panga haiamuliwi kwa panga unatakiwa uwe na silaha kubwa zaidi.
Wanaandamana wanafanya vurugu hadi mdogo wangu kaumizwa. Siendi kwenye mikutano.yoyote ya siasa na kitambulisho.cha kura nimechoma. Tumbafuuuu!
Wacha wapewe kipondo wote wanaofanya vurugu.
Tumbafuuuu
 
Wewe ndiye kiazi mviringo kweli,ulitegemea atengwe na shehe?
sababu CHADEMA NDIO WENYE HAKI MILIKI NA UKATOLIKI SIO!!!hadi mmefikia kuchagua nani aingie kanisani na nani asiingie. then mkiambiwa chadema ni chama cha kanisa mnabisha.
 
sababu chadema ndio wenye haki miliki na ukatoliki sio!!!hadi mmefikia kuchagua nani aingie kanisani na nani asiingie. Then mkiambiwa chadema ni chama cha kanisa mnabisha.
kuippenda ccm inabidi uwe na mashusiano na shetani
 
Imani yangu ndogo iliyokuwa imebaki kwa baadhi ya viongozi wa CCM ilikuwa imebaki kwa Pinda. kama leo ameweza kutoa kauli ya namna hiyo basi nimeamini kwamba viongozi wa CCM hawamwamini Mungu, hukumu ya milele wala maisha baada ya kifo. Kuja kwenye makanisa ni kujipotezea muda bure.

Watu waliokusanyika kwa ajili ya mkutano wa kampeni wanauawa kwa bomu, wakikusanyika tena kwa majonzi ya kuwaaga wenzao waliouawa wanasema kuwa wanakaidi amri ya polisi. Hivi hawa polisi walikuwa wameandaa bomu la kuua na hapo hapo wameandaa amri ya kukataza watu wasikusanyike? Tangu lini watu wanaalikwa kwa ajili ya msiba na kuomba kibali cha polisi?

Pinda kama hajalogwa, alikuwa anazungumzia amri ipi ambayo wananchi walikuwa wamekaidi? Mwangosi alipouawa alikuwa akifanya kazi ya kupata habari, alikuwa amekiuka amri ipi? Dr. Ulimboka alikuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari alikuwa amekaidi amri ipi? Hivi siku hizi mtu akikaidi amri ya polisi anahukumiwa na hao hao polisi bila kufika kwenye mahakama yoyote?

Pinda aelewe kuwa serikali imewekwa madarakani na wananchi na wananchi ndiyo wanaoweza kuiamuru itekeleze maagizo yao na siyo wananchi watekelezi upumbavu wa serikali. Wananchi wameiagiza muda mrefu kwamba iwapeleke mahakamani mafisadi, lakini serikali imekaidi amri hiyo. Huyo huyo Pinda alipobanwa kuhusu kuwafungulia mashtaka mafisadi aliwatetea kuwa kuwashtaki mafasadi kutaiyumbisha nchi.

Wananchi wameiagiza Serikali ya CCM kwamba katika uchaguzi hawapo tayari kuwachagua wale wanaogombea uongozi kupitia CCM, lakini CCM wanalazimisha kutumia rushwa na polisi kulazimisha kuingia madarakani. Wanasahau kuwa wananchi ndio wenye uamuzi wa nani awe kiongozi?

CCM kumbukeni jambo moja, hakuna dola yoyote duniani iliyowahi kushindana na raia wake( kinyume chake hakiwezekani). Ninachoona ni kuwa Pinda anafikiri kuwa wananchi hawawezi kupingana na serikali. Ni uwendawazimu kuwatisha wananchi kuwa wasishindane na serikali. Huo ni ugonjwa wa upungufu wa akili kichwani.

Madaraka ya wananchi dhidi ya serikali hayana kikomo lakini madaraka ya serikali yana kikomo. Dola zote zinazoongozwa na viongozi ambao hawajaathirika kiakili daima wamekomea pale ambapo utashi wa wananchi haukubaliani na yale yanayofanywa na serikali. Ninachoona hapa kwetu Tanzania ni kuwa serikali ipo juu ya wananchi badala ya wananchi kuwa juu ya serikali. Viongozi gani hawa hawasomi katiba ambayo imetaja wazi wazi kwamba madaraka ya serkali yanatoka kwa wananchi?

Viongozi mkome kabisa kuwatisha wananchi. Wananchi wana sauti ya mwisho juu ya uendeshaji wa nchi siyo serkali iliyopo madarakani.Nukta.

Safi sana mkuu. Yaani serikali imejisahau kabisa kuwa imezaliwa na wananchi na sio serikali imezaa wananchi. (serikali ni chombo cha kutumikia wananchi.)
 
kwa uchungu kabisa kauli ya mizengwe punda si ya kibinadamu,na kama kardinali pengo ungewashauri mumtenge dikteta huyo wameshinndwa kuongoza sasa wanatisha na kutumia mabavu.Watu wasio na hatia wameuwawa na polosi wenu bado mnatutisha,hatutatishika na porojo zenu tutawonesha mkanda jinsi polisi wako walivyouwa mwanamke na mtoto wa miaka 7 hii nilaana ambayo hamtakwepa popote.Mizengwe una muda usiopunguwa miska 2 madarakani,tutakushitaki kwa kauli hii uliyoitoa bungeni.2016 hautakuwa pm hivyo utaturleza aliyekutuma ni nani.
Miongozi yetu imelewa midaraka na mipesa ya bwerere sasa lazima icheuwe kwa mijineno yakukifu; Ila tu mjue wanamtolea sadaka aliyewapa madaraka na mifedha kwa damu na kutia vilema. Wenzio wanafanya ibada yao tu manake sioni hata upinzani uliopo hapa nchini wa kuwatia mteru kiasi hicho
 
Kwa kweli tuache ushabiki wa kisiasa, kauli ya Pinda Bungeni si ya kiungwana wala ya Kiongozi ya ngazi yake. Nashauri aikanushe kwa kulia kama ili ya kuua wanaoua Albino au akatubu kanisani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom