Pendekezo: Wallace Karia atimuliwe TFF, analeta siasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,117
Hakuna mahali popote katika dunia hii ambako siasa ilichanganywa na mpira wa miguu na kukapatikana mafanikio, ndio maana kuna uongozi wa kisiasa unaopiganiwa majukwaani kama kinyang'anyiro cha ubunge wa Kinondoni na Siha, tofauti kabisa na uchaguzi wa TFF.

Kitendo cha Karia kuwaelekeza waandishi maswali ya kumuuliza Rais wa FIFA ni usaliti uliochanganyika na ubabe wa kishamba sana, amelenga kumlinda nani?

Rais wa FIFA si mtoto mdogo na anaijua Zanzibar pengine kuliko Mzamiaji Karia, aachwe ajibu maswali yote yatakayoletwa kwake kwa kadri ya waandishi watavyoulizwa.

Inafahamika kwamba Karia ni Team Malinzi (bado sijaelewa aliponaje kwenye ule msala) sasa huku anakoenda anataka kutuletea ubabe wa Ndolanga enzi za FAT, inabidi wembe uliotumika kumnyoa Malinzi ugeuzwe kwa Karia, ili aende kuungana na chama chake kwenye siasa.

Poor Karia !
 
Watanzania sisi ni watu wa ovyo. Tumekubali Msomali awe Rais TFF.
....Mkuu huyu alikuwa DED Mvomero na kwa hakika ameleta maendeleo makubwa sana kwenye kipindi chake hapo Mvomero, ina maana hilo halikufahamika?
 
....Mkuu huyu alikuwa DED Mvomero na kwa hakika ameleta maendeleo makubwa sana kwenye kipindi chake hapo Mvomero, ina maana hilo halikufahamika?
Mkuu, usishangae hii Bongo yetu. Hadi jeshini walikuwepo foreigners kwenye nafasi nyeti za intelligence. Sasa wapo kwao Rwanda. Just imagine!
 
hamna kitu wadanganyika na nyinyiem hawakipendi kukisikia ni Zenjibar kupewa uanachama wa Fifa na hicho ndo kimempeleka kagera man lupango
 
Mkuu, usishangae hii Bongo yetu. Hadi jeshini walikuwepo foreigners kwenye nafasi nyeti za intelligence. Sasa wapo kwao Rwanda. Just imagine!
Kagame hana ubaguzi hata wazawa wa kiTZ anawachukua mfano lipumba alimchukua awe mshauri wake na pia wabongo wengine wengi tumeona kagame akiwachukua kupata skills na juzi alichukua walimu wa kiswahili toka TZ..ndio maana namuona genius kagane

Kuna wa south nk paul anawachukua ndio maana Rwanda imepiga hatua kubwa sana chini ya kagame laiti angekuwa na mentality kama yako huenda Rwanda ya Leo tusingeiona..Paul anachukua diasporas na foreigners hata kwa kuwalipa pesa nyingi ndio maana Rwanda leo hii ina wenye ujuzi kibao

Huko NASA 30% ni wahindi na ni idara nyeti ya USA .

Magu naye amekuwa na akili kachukua it's wa Rwanda ili sisi tulioendekeza siasa tunolewe ..good mr president
 
Ni sawa lakini tusichanganye issues.

Kagame anawachukua na passport zao akijua ni Watanzania lakini kwa sababu ya upungufu wa Watalaam wanaenda kufanya kazi na kurudi. Hata Wakenya wapo wengi.

Kuna cases za Wanyarwanda walioishi hapa kwetu Tanganyika kama Watanzania lakini wamerudi kwao kwa njia za panya na ku claim unyarwanda wao. Mmoja maarufu alikuwa jeshini!

Tofautisha hivyo vitu viwili.
 
Back
Top Bottom