Pendekezo la Mdahalo wa Katiba Mpya

Pendekezo la Mdahalo wa Katiba Mpya

ethink

Member
Joined
Mar 5, 2009
Posts
11
Reaction score
5
Ndg. wanajamii kutokana na hali ya mkanganyiko wa sasa wa mchakato wa Katiba, napendekeza kuwe na mdahalo ambao wazungumzaji wakuu wawe:
1. Jaji Joseph Warioba
2. Prof. Kabudi
3. Mh. Samweli Sita
4. Mh. Andrew Chenge

Mdahalo huu utangazwe na vyombo vyote vya habari binafsi na vya serikali.

Washiriki wawe wahariri vyombo vya habari ili kupunguza zomea zomea na kutupa fursa wananchi kuchambua mbivu na mbichi.

Nawakilisha.
Raia wa kawaida nisiye na upande.
 
Kila kitu Warioba tu, tunahitaji na wengine waseme!
 
Kila kitu Warioba tu, tunahitaji na wengine waseme!

Hayo ni mawazo yangu finyu, si vibaya ukipendekeza wasemaji wengine natumaini taasisi zitakazojitokeza kuandaa mdahalo huu watawafikiria.
 
Hayo ni mawazo yangu finyu, si vibaya ukipendekeza wasemaji wengine natumaini taasisi zitakazojitokeza kuandaa mdahalo huu watawafikiria.
Napemdekeza pia awepo Prof Issah G. Shivji!
 
Wazo zuri ila hao namba 3 na 4 hawawezi kukubali. Na upande wa Zanzibar nako kuna wataalamu wa katiba wawepo wawili, mmoja toka kwenye tume na mmoja toka BMK masalia.
 
Ahsante si wazo baya cha msingi, wananchi tupate ukweli toka kila upande ili tufanye maamuzi sahihi,

Freedom of speech is perhaps one of the most abused freedoms we have
 
Wazo zuri ila hao namba 3 na 4 hawawezi kukubali. Na upande wa Zanzibar nako kuna wataalamu wa katiba wawepo wawili, mmoja toka kwenye tume na mmoja toka BMK masalia.
Iliyokiwa Tume iko biased sana, wajumbe wake wakiwa wengi tutapata mawazo ya upande mmoja!
 
Hatutaki sita wala vijisenti tunataka Warioba na Kabudi pamoja na Polepole ndo wawe wasemaji.
ITV tunaomba utaratibu jinsi ya kupata mdahalo ule wa Warioba,Butiku na wengine kabla ya upuuzi kuanza Dodoma.Me nitaununua plz
 
Back
Top Bottom