Pendekezo: John Heche amrithi Zitto Kabwe

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF,

Kiongozi wa Bavicha Taifa John Heche ni kati ya wanamapinduzi waliojitolea na kufanya kazi kubwa sana ya kupigiwa mfano.

Kila tunaposoma vyombo vya habari John Heche anaripotiwa yuko vijijini kufungua mashina, ofisi na kuingiza wanachama wapya. Ni mwezi uliopita tu alikuwa mikoa ya nyanda za juu kusini na kuingiza maelfu ya wanachama.

Wiki hii mwanzoni alikuwa Morogoro na leo yuko vijijini Kagera akifanya kazi kubwa ajabu. Hata anapokuwa mapumzikoni Dar John Heche hatulii ofisini bali anazunguka kila kona ya Dar akifanya mikutano na kuzindua mashina.

Ni wazi kabisa kwamba kiongozi anayependwa na nyota wa chama hicho kwa sasa Katibu Mkuu Dr Willibrod Slaa amekuwa na majukumu mengi kiasi kwamba pengo la Naibu katibu mkuu Bara linaonekana wazi.

Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe amekuwa na majukumu mengi ya kibunge kiasi kwamba anashindwa kumsaidia Katibu mkuu majukumu yake.Zitto awe tu mjumbe wa Kamati kuu ambaye atakuwa hana majukumu ya kila siku ndani ya Sekretariati.

Ninatoa mapendekezo kwa viongozi wa chama kwamba ikiwezekana katika uchaguzi wa sekretariati mpya mwakani John Heche akabidhiwe mikoba ya Zitto Kabwe kwa ufanisi zaidi.Ikumbukwe kutokana na majukumu mengi ya kibunge ya Zitto ameshindwa karibu mara 4 mfululizo kuhudhuria vikao muhimu vya chama hicho vilivyotoa maamuzi mazito.

John Heche ni Jasiri, mpambanaji, anayefanya kazi usiku na mchana na aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya CHADEMA.

Hakika John Heche ni jembe kwelikweli anayepaswa kupandishwa daraja zaidi.

Nawasilisha.


 
Kazi anayoifanya Zitto kwa CDM inafananishwa na matap tap ya Heche?? Dah, kweli hapo hamna chama!

Umerudi? CCM wakimsikia Heche/Dr Slaa au Mbowe wanapata presha.
 
Kazi anayoifanya Zitto kwa CDM inafananishwa na matap tap ya Heche?? Dah, kweli hapo hamna chama!

Mbona umeishiwa sera kiasi hiki? Kama asubuhi unachangia kwa mtindo huu,itakapofika mchana si utatukana matusi humu.
Comment with smile, epuka jazba!
 
Zito atabaki kua Zito 2 hao watoto wanajaribu kuinga nyenendo zake hamna cha Heche wala Mnyika

Hajasema Zitto na Heche nani zaidi. You should read between the lines, Mtoa mada katoa hoja yenye mashiko.sijui wewe hujamuelewa wapi ili atoe ufafanuzi kwa maana namuona bado yupo humu.
 
Hajasema Zitto na Heche nani zaidi. You should read between the lines, Mtoa mada katoa hoja yenye mashiko.sijui wewe hujamuelewa wapi ili atoe ufafanuzi kwa maana namuona bado yupo humu.

Nakushukuru sana mkuu kunisaidia kunyoosha maelezo.Wala sijasema Zitto hafai bali amezidiwa na majukumu ya kibunge.Nafasi ya Naibu Katibu mkuu inapaswa kukabidhiwa kwa mtu asiye na majukumu zaidi ya hilo moja tu la kukisambaza chama kila kona ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…