Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,179
- 7,330
Nimekuwa nikitoa nyuzi mbali mbali kuishauri serikali iweke taa za barabarani za kutosha katika miji yetu kupunguza ajali... naomba nisichoke kufanya hivyo...
Kwa takwimu zilizopo Tanzania kuna zaidi ya pikipiki laki 5 zinazohudumu kama boda boda kwa sasa
Pia imeonyeshwa kuwa ushuru wa boda boda mwaka huu umepanda hadi takribani Tsh 95,000/= kwa mwaka
Hii ni kusema takribani bilioni 50 zitakusanywa kama ushuru wa boda boda kwa mwaka...
Zaidi ya watu 5 hufa kila siku kutokana na ajali zitokanazo na pikipiki. Hapo haujaongelea ulemavu, maumivu na hasara zitokanazo na ajali hizo.
Kiuhalisia ukifanya sensa leo, ni familia chache sana ambazo hazina ndugu, jama au rafiki aliyewahi kuathirika kwa namna moja au nyingine na ajali ya pikipiki.
Sehemu kubwa ya ajali za pikipiki hutokea mijini
Na pia inafahamika sehemu kubwa ya ajali za pikipiki (na magari) hutokea kwenye makutano ya barabara
Ingawa sio mwarubaini pekee, nina uhakika kuimarishwa usalama kwenye makutano ya barabara inaweza kupunguza hadi 30% ya ajali zinazotokea nchini, na hiyo pengine ni kusema itaokoa maisha ya mtu mmoja kila siku au zaidi ya watu 365 kwa mwaka
Sina ujuzi sana kwenye gharama za installation ya taa za kuongozea magari, lakini naamini kwa wastani haitazidi Tsh milioni 10 kwa taa za eneo moja.
Serikali "ikizimwaga" Tsh bilioni 50 kwenye taa ina maana makutano 5000 yatapata taa nchi nzima.
Sehemu zinazohitaji taa kwa sasa nchi nzima naamini hazipungui 10,000 lakini ukifanikiwa kuweka kwenye sehemu 5,000 hakika utakuwa umepiga hatua kubwa sana.
Please please, sijui plan ya wizara ya ujenzi na mambo ya ndani kwa huu, lakini naomba special consideration kwenye hili suala kupunguza vifo, ulemavu na maumivu na maumivu haya yanayozuilika.