Penda usikodhania

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini mabestitoooooooo

Jamani wanajamvi hebu tujifunze kitu kutoka katika majadiliano kati ya MKAKA NA MDADA
walipokutana mara ya kwanza na kuanzisha mahusiano ya uchumba wa awali ili waje wawe
wanandoa kamili, oneni vituko vioja na visanga hapa chini. Utakapomaliza kusoma mjadala huu
utaniambia umejifunza nini na umepata nini au umepiga hatua gani katika mahusiano yako na
yule mwandani wako wa karibu ambaye unamsaka uwe nawe maishani

PITIA MJADALA HUU HAPA JINSI WALIVYOKUTANA NA WALIVYOANZA KUCHUMBIANA KIAINA

Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi?

Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake,
nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."

Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo."

Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."

Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe."

Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu? Wasichana mbona wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote."

Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila."

Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa."

Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,
nao watakuwa mwili mmoja."

Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,
upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,
kisha ndipo utakapositawi sana."

Binti: Wowwww! Naona unampenda sana Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini."

Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki,
yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri
yo yote, yatafakarini hayo."

Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"

Binti: lakini sasa ndoa yenyewe tutafungia wapi?
Jamaa: Kwa Mkuu wa wilaya maana mimi ni MPAGANI

Marafiki zangu natumai hapa mmepata kitu kwa ambao wanatafuta mwenzi wa maisha yao, waanze mapema na sio
kukurupuka na mwishoe mtavamia na majanga bure msijesema Mama PAROKO sijawaambia na kuwashauri juu ya
kupata ndoa bora. Kama umejifunza kitu nitwangie chini. Nawapenda


copy: 24hrs, Mamndenyi, Bujibuji, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi, Heaven on Earth, measkron, watu8, Lady doctor, stevoh, Kaizer, Mwanyasi, Himidini, Simplicity, Mentor, Passion Lady, charminglady, mwallu, Mwali, kabanga, Young Master, Erickb52, Mr Rocky, Bishanga, Ruttashobolwa, nitonye, Mokoyo, sokwe, Smile, Nivea, shansarie, kiwatengu, Judgement, figganigga, lady gaga, sweetlady, FirstLady, Pasco, BAK, @Tutpr B, Madame B, madame X, amu, MziziMkavu, na marafiki zangu wote ambao nimewasahau kuwataja hapa karibuni tushare pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Usingeboreka bestito si ndo anajifunza kumwambia mdada wewe hujui wanaume wanavyojifaragua mbele ya wanawake utadhani wanamwagiwa maji baridi yenye barafu ndani wanakuwa na kigugumizi cha mdomo
nimekupata ila hizo swaga za jamaa daa mi ningeboreka asee
 
Wanaume wengi siku hiz ni wadanganyifu sana anakuja na gia ya kuwa me nilioa mke lakin kwa ss tumeachana ukichunguza kwa undani zaid utakuta hajamwacha mkewe ila anataka tu mtu wa part time na mwingine anaingia na mwamvuli wa dini ili afanane na msichana aliye nae kwa wakati huo mim ushauri wangu na ungana mam paroko
 
Duuh! nimeikubali mbwembwe nyingi kumbe hata mlango wa kanisa haufaamu kazi kwelikweli
 
Usingeboreka bestito si ndo anajifunza kumwambia mdada wewe hujui wanaume wanavyojifaragua mbele ya wanawake utadhani wanamwagiwa maji baridi yenye barafu ndani wanakuwa na kigugumizi cha mdomo

afu akishakuzoea anakuwa mjuajii
 
^^
Ni njia nzuri ya kupata mwenza ingawa hadhari inapaswa ichukuliwe. Maana si ajabu kuwaona vijana wanakariri mistari ya vitabu vitakatifu au kujibanza maeneo ya kuabudu ili wawanase wawatakao, wakiwapata tu wanaondoka.. Wote tu hata machangudoa wanahama mahali wanaenda kuimba mpaka kwaya kuficha makucha yao!
Ukweli unabaki palepale Muda wa kujiridhisha juu ya mtu mpya unahitajika.
^^
 
Nimeyapenda
Nimeipenda mistari
Mistari imesimama
Kinachotafutwa ni mbunye tu
Mistari inatafsiriwa ndivyo sivyo
Mbunye nomaaaaaaaaaaaaah

Bazazi
​
 
Mbon a unanishangaza bestito ina maana hujui kunako fani hizo? Hebu twanga chini uone furaha yake jinsi mahindi yanavyojikoboa yenyewe

ngoja na mimi nikatunge mistari wallah hutoki safarii hii, mara ya kwanza nilikuja kikurya ukaniponyoka..

huko kutwanga chini hata mimi nimepotea maboya kinu hakionekani
 
Nzuri bestito nilifikiri nawe ulikesha jana?
Nashkuru kwa mistari yako ngoja niisome kkidogo

mwanzo 51:2 - 4 na mithali 32: 7 vyote vinaelezea jambo hilo.

Habari ya asubuhi mpendwa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…