Pemba haina uwakilishi bunge maalum la katiba

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
Samuel-Sitta-August22-2014.jpg

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ali Omar Juma, amesema hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza kuridhishwa na utendaji wa Bunge hilo wakati hakuna mwakilishi aliyechaguliwa kwa kura na wananchi wa Pemba, ni kubariki Pemba kuwa nchi inayojitegemea.

Juma ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), alisema hatua hiyo ya CCM inatafsiriwa sawa na kuunga mkono ombi lililowahi kuwasilishwa na Pemba kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon, Mei 2009.

Akizungumza na NIPASHE jana, Juma alisema kupitia watu 12 wakiongozwa na Ahmad Ali Musa, Pemba ilitaka kujitenga na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maombi yaliyoshughulikiwa na UN kupitia aliyekuwa Balozi wa Tanzania, ambaye sasa ni Balozi nchini Somalia Agustine Mahiga.

Kwa mujibu wa Juma Mahiga alikiri kuwapo mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar na kwamba, suala hilo ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha kupatikana Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, mwaka 2010.

Alitaja sababu zilizotolewa na Musa ambaye kwa sasa ni mkazi wa Ole kisiwani Pemba wakati wakidai kutengwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni kisiwa hicho kutengwa kisiasa na kiuchumi.

Alisema miongoni mwa ushahidi wa madai yao, ulikuwa mfumo wa uongozi wa kitaifa, uliodhihirisha kuwapo upendeleo wa wazi kwa Unguja.

"Mussa alimueleza Ban Ki-Moon kuwa hata Baraza la Mawaziri asilimia 95 lilikuwa likiundwa na viongozi kutoka Unguja," alisema Juma.
Alisema wao (wajumbe wateule wa Rais Jakaya Kikwete) waliobaki bungeni hawawezi kubeba jukumu la wawakilisha 18 na wabunge 18 waliochaguliwa kwa kura na wananchi wa Pemba.

Alimtaka Rais Kikwete kutokubali kuzongwa na itikadi za kisiasa, badala yake, alimshauri kubaki na msimamo wake wa awali uliomfanya aungane na wananchi kuandika historia, akisema ni hilo pekee litakalosababisha Tanzania kutogawanyika na heshima yake (JK) kutukuka ndani na nje ya nchi.

KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA
Alisema kwa sasa ndani ya kamati hawachambui wala kuboresha rasimu ya katiba kama inavyoelekezwa kwenye sheria, sura ya 83 ya mwaka 2014 badala yake wanachokifanya ni kuweka viraka katiba ya sasa iliyoandikwa mwaka 1977.

Juma ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema badala ya kurekebisha na kubadilisha, watu wanafuta na kuweka vipengele kutoka kwenye katiba ya sasa au wanakojua wao, bila kujali kuwa wanabadili maudhui yaliyomo kwenye maoni ya wananchi ndani ya rasimu ya katiba.

"Mfano halisi ni Ibara ya 64 ya katiba ya sasa imehamishiwa kwenye rasimu kama ilivyo. Kinachoendelea sasa ni uchakachuaji siyo uandishi wa katiba," alisema Juma.

Aliongeza: "Hii inakosesha mchakato uhalali wa kisheria kwa sababu sheria husika inaendelea kuvunjwa kwa watu kuja na ajenda zao mifukoni, kufuta mwongozo halali wa kisheria na kuyaingiza ya kwao."

Alisema hata uhalali wa kisiasa na kijamii umekosekana kwenye mchakato huo, jambo ambalo halihitaji mtu kusomea sheria kulibaini kwa sababu tayari vyama karibu vyote vya upinzani vya kisiasa vipo nje ya mchakato huo.

Alisema Chaumma inaunga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) waliosusia Bunge hilo, lakini haitatoka bungeni kwa sababu ina haki ya kufahamu kinachofanyika humo.

"Ukawa wana haki ni halali walivyosusia vikao hivi na tunawaunga mkono kwa asilimia mia moja. Lakini hatutatoka kwenye vikao, maana ni lazima tufahamu kwa hakika kinachofanywa. Tusingekuwapo, nani angeeleza Watanzania haya? Hatukutoka, hatutatoka na hakuna atakayetutoa," alisema Juma.

Aliwasifia Ukawa kwa msimamo wao kuwa una maslahi mapana kwa taifa zaidi ya itikadi za kisiasa na kutaka Watanzania wenye nia nzuri na Tanzania kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema katiba ya sasa na ile ya Zanzibar, zinatambua uwapo wa mamlaka kuu tatu; inayosimamia mambo ya Jamhuri ya Muungano, inayosimamia mambo yasiyokuwa ya muungano ya Zanzibar na inayosimamia mambo yasiyo ya muungano kwa Tanzania Bara na hivyo haelewi maana ya wanaopinga mfumo wa serikali tatu.

Juma alisema kiini cha tatizo linaloukabili mchakato huo, ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwamba bila kueleza sababu za kutotekeleza Azimio la Bunge hilo, lililoelekeza kuwa Agosti 5 wangeanza kazi kwa kupiga kura kuamua juu ya sura ya kwanza na sita ya rasimu zilizojadiliwa awali, alisimamia waanze kwa kubadilisha kanuni.

Alimshutumu Sitta kuwa wala hakutengua azimio hilo halali la Bunge kabla ya kuingiza aliyoita mambo yake, hali iliyosababisha mpaka sasa wajumbe wengi kutoelewa wanachofanya, zaidi ya kupokea posho na kushuhudia sarakasi za aina yake zikifanyika.

HALI ILIVYO KWENYE KAMATI
Alisema hata kama kanuni zinazuia wajumbe kuzungumzia yanayojiri ndani ya kamati zao, hakuwa na budi kuyazungumzia kwa maslahi ya taifa.

Juma alisema mpaka jana hawakuwa wamefanya maamuzi yoyote katika mambo waliyojadili, hali aliyoihusisha na kutokuwapo uwezekano wowote wa kupata theluthi mbili kutokana na wajumbe wa Ukawa waliosusia vikao hivyo.

Alisema kamati namba nne ina wajumbe 19 kutoka Zanzibar, lakini waliomo ni 12 na ili theluthi mbili ipatikane zinahitajika kura 14 kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar.

Alimuomba Rais Kikwete na CCM kulegeza msimamo wao wa kutokubali mabadiliko kwa kuridhia Bunge hilo lisitishwe, ili muafaka wa kweli upatikane na hatimaye katiba halali kisiasa na kisheria ipatikane.

Chanzo: Nipashe
 
Rasimu ya Katiba inayojadiliwa ni ya tanzania bara (tanganyika) na unguja kwishine.na 2kmbuke waziri wa sheria na katiba naye hayupo kwny BMK
 
Ccm imeparaganyika,tumebaki na wachumia tumbo na si scientifical politicians.
 
images.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma)Zanzibar Ali Omar Juma

Na Waandishi wetu
22nd August 2014

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ali Omar Juma, amesema hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza kuridhishwa na utendaji wa Bunge hilo wakati hakuna mwakilishi aliyechaguliwa kwa kura na wananchi wa Pemba, ni kubariki Pemba kuwa nchi inayojitegemea.

Juma ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), alisema hatua hiyo ya CCM inatafsiriwa sawa na kuunga mkono ombi lililowahi kuwasilishwa na Pemba kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon, Mei 2009.

Akizungumza na NIPASHE jana, Juma alisema kupitia watu 12 wakiongozwa na Ahmad Ali Musa, Pemba ilitaka kujitenga na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maombi yaliyoshughulikiwa na UN kupitia aliyekuwa Balozi wa Tanzania, ambaye sasa ni Balozi nchini Somalia Agustine Mahiga.

Kwa mujibu wa Juma Mahiga alikiri kuwapo mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar na kwamba, suala hilo ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha kupatikana Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, mwaka 2010.
Alitaja sababu zilizotolewa na Musa ambaye kwa sasa ni mkazi wa Ole kisiwani Pemba wakati wakidai kutengwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni kisiwa hicho kutengwa kisiasa na kiuchumi.

Alisema miongoni mwa ushahidi wa madai yao, ulikuwa mfumo wa uongozi wa kitaifa, uliodhihirisha kuwapo upendeleo wa wazi kwa Unguja.
“Mussa alimueleza Ban Ki-Moon kuwa hata Baraza la Mawaziri asilimia 95 lilikuwa likiundwa na viongozi kutoka Unguja,” alisema Juma.

Alisema wao (wajumbe wateule wa Rais Jakaya Kikwete) waliobaki bungeni hawawezi kubeba jukumu la wawakilisha 18 na wabunge 18 waliochaguliwa kwa kura na wananchi wa Pemba.

Alimtaka Rais Kikwete kutokubali kuzongwa na itikadi za kisiasa, badala yake, alimshauri kubaki na msimamo wake wa awali uliomfanya aungane na wananchi kuandika historia, akisema ni hilo pekee litakalosababisha Tanzania kutogawanyika na heshima yake (JK) kutukuka ndani na nje ya nchi.

KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA

Alisema kwa sasa ndani ya kamati hawachambui wala kuboresha rasimu ya katiba kama inavyoelekezwa kwenye sheria, sura ya 83 ya mwaka 2014 badala yake wanachokifanya ni kuweka viraka katiba ya sasa iliyoandikwa mwaka 1977.

Juma ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema badala ya kurekebisha na kubadilisha, watu wanafuta na kuweka vipengele kutoka kwenye katiba ya sasa au wanakojua wao, bila kujali kuwa wanabadili maudhui yaliyomo kwenye maoni ya wananchi ndani ya rasimu ya katiba.

“Mfano halisi ni Ibara ya 64 ya katiba ya sasa imehamishiwa kwenye rasimu kama ilivyo. Kinachoendelea sasa ni uchakachuaji siyo uandishi wa katiba,” alisema Juma.
Aliongeza: “Hii inakosesha mchakato uhalali wa kisheria kwa sababu sheria husika inaendelea kuvunjwa kwa watu kuja na ajenda zao mifukoni, kufuta mwongozo halali wa kisheria na kuyaingiza ya kwao.”

Alisema hata uhalali wa kisiasa na kijamii umekosekana kwenye mchakato huo, jambo ambalo halihitaji mtu kusomea sheria kulibaini kwa sababu tayari vyama karibu vyote vya upinzani vya kisiasa vipo nje ya mchakato huo.
Alisema Chaumma inaunga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) waliosusia Bunge hilo, lakini haitatoka bungeni kwa sababu ina haki ya kufahamu kinachofanyika humo.

“Ukawa wana haki ni halali walivyosusia vikao hivi na tunawaunga mkono kwa asilimia mia moja. Lakini hatutatoka kwenye vikao, maana ni lazima tufahamu kwa hakika kinachofanywa. Tusingekuwapo, nani angeeleza Watanzania haya? Hatukutoka, hatutatoka na hakuna atakayetutoa,” alisema Juma.

Aliwasifia Ukawa kwa msimamo wao kuwa una maslahi mapana kwa taifa zaidi ya itikadi za kisiasa na kutaka Watanzania wenye nia nzuri na Tanzania kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema katiba ya sasa na ile ya Zanzibar, zinatambua uwapo wa mamlaka kuu tatu; inayosimamia mambo ya Jamhuri ya Muungano, inayosimamia mambo yasiyokuwa ya muungano ya Zanzibar na inayosimamia mambo yasiyo ya muungano kwa Tanzania Bara na hivyo haelewi maana ya wanaopinga mfumo wa serikali tatu.

Juma alisema kiini cha tatizo linaloukabili mchakato huo, ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwamba bila kueleza sababu za kutotekeleza Azimio la Bunge hilo, lililoelekeza kuwa Agosti 5 wangeanza kazi kwa kupiga kura kuamua juu ya sura ya kwanza na sita ya rasimu zilizojadiliwa awali, alisimamia waanze kwa kubadilisha kanuni.

Alimshutumu Sitta kuwa wala hakutengua azimio hilo halali la Bunge kabla ya kuingiza aliyoita mambo yake, hali iliyosababisha mpaka sasa wajumbe wengi kutoelewa wanachofanya, zaidi ya kupokea posho na kushuhudia sarakasi za aina yake zikifanyika.

HALI ILIVYO KWENYE KAMATI

Alisema hata kama kanuni zinazuia wajumbe kuzungumzia yanayojiri ndani ya kamati zao, hakuwa na budi kuyazungumzia kwa maslahi ya taifa.

Juma alisema mpaka jana hawakuwa wamefanya maamuzi yoyote katika mambo waliyojadili, hali aliyoihusisha na kutokuwapo uwezekano wowote wa kupata theluthi mbili kutokana na wajumbe wa Ukawa waliosusia vikao hivyo.
Alisema kamati namba nne ina wajumbe 19 kutoka Zanzibar, lakini waliomo ni 12 na ili theluthi mbili ipatikane zinahitajika kura 14 kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar.

Alimuomba Rais Kikwete na CCM kulegeza msimamo wao wa kutokubali mabadiliko kwa kuridhia Bunge hilo lisitishwe, ili muafaka wa kweli upatikane na hatimaye katiba halali kisiasa na kisheria ipatikane.

CHANZO: NIPASHE
 
Leo hii -niseme wiki hii- haiwezi kuwa nzuri kwa ccm hii ya Kikwete, Kinana na Nape. Vijana wao Lumumba buku 7 FC nao lazima wamechanganyikiwa maana wanasubiri kupewa mwongozo wakati watoa miongozo nao wamechanganyikiwa hali kadhalika.

The knives are well and truly out now!
 
Ccm imeparaganyika,tumebaki na wachumia tumbo na si scientifical politicians.
Huwezi kuamini kuwa hiki ndicho chama cha Mwalimu Nyerere na Mzee Kawawa. Wengi tuliamini kuwa jina 'J.K' kwa vile limeshabihiana JK basi ingelikuwa chachu lakini....;

Sidhani kama huyu mzee sita kama ana akili timamu?? Unafumua maoni ya wananchi kwa mjibu wa sheria ya kupata katiba yao halafu unaweka ya kwako na chama chake!! sidhani kama huyu mzee yuko sawa!
 
hivi JK huwa anasoma magazeti au anasomewa? na ansoma magazeti gani? Uhuru na udaku au na mengine. hata motto wa chekechea anaweza kuona kuwa hakuna kitu Dodoma zaidi ya posho
 
Huyu Katibu wa Chaumma Ali Omar Juma ni mchumia mtumbo!

Wakati anawasifu na kuwaunga amkono UKAWA kususia vikao vya BMK, lakini wakati huo huo anasisitiza kwamba Chaumma hakitasusia vikao vya BMK! He is not walking the talk.

Halafu nime-check record zangu na kukuta kwamba Hamad Rashid ni Mbunge wa WAWI PEMBA na anahudhuria vikao vya BMK.
 
Bobuk
vipi huku waona wengine kwenye hiyo record zake ?

kwa taarifa zako hamad rashid ni mbunge wa mahakama hapo upo?
 
Last edited by a moderator:
Bobuk

Hamad rashid anajiandaa kwenda kugombea mbozi kwa shemegi zake wachuna ngozi.
Pemba walisha mkataa siku nyingi amebaki bungeni kwa nguvu ya mahakama tu.
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni counter attack za UKAWA ,mbona ndani ya BMK mna UKAWA wengi tu .hapo ndipo CCM anapopigwa chenga ya mwili waliona wale waliotoka ndio wamepata nafasi nzuri na nyeti kufanya madudu yao ,kwa taarifa kuna vigogo wa CCM hawakubaliani na serikali mbili nao wamo ila manyanga yatabwagwa moja moja ,kuna G55 nao wapo dili lao lipo palepale ,hoja ni kuikwamisha CCM tu +
 
Kama tunavyojua Pemba ilikuwa nchi kabla ya kuungana na Zanzibar. Hivyo basi Pemba kwenye bunge hili ina masirahi kama ilivyo Tanganyika au Zanzibar, na katika nchi zinzojali demokrasia tungebidi kuwauliza wananchi wa zilizokuwa nchi hizi kama wanataka kuendelea kuwa kwenye muungano.

Sasa kama mnavyojua Pemba kuanzia Sheha mpaka mbunge au mwakilishi wote ni CUF na CUF wamesusia bunge hilo. Kwa mameno machache ni kwamba iliyokuwa nchi ya Pemba haiwakilishwi. Katiba itakayopatikana haina mawazo wala mchango wa mtu toka Pemba. Hatari inayokuja ni kwamba wapemba wataongoza mapambano ya kudai katiba mpya na hata nchi yao.

Tafakari!
 
Back
Top Bottom