Pemba haina Uwakilishi Bunge la Katiba.

Pemba haina Uwakilishi Bunge la Katiba.

Nchompa

Member
Joined
Jun 22, 2014
Posts
34
Reaction score
8
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,
Ali Omar Juma, amesema hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza kuridhishwa na utendaji wa Bunge hilo wakati hakuna mwakilishi aliyechaguliwa kwa kura na wananchi wa Pemba, ni kubariki Pemba kuwa nchi inayojitegemea.

Juma ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), alisema hatua hiyo ya CCM inatafsiriwa sawa na kuunga mkono ombi lililowahi kuwasilishwa na Pemba kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon, Mei 2009. Akizungumza na NIPASHE jana, Juma alisema kupitia watu 12 wakiongozwa
na Ahmad Ali Musa,Pemba ilitaka kujitenga na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maombi yaliyoshughulikiwa na UN kupitia aliyekuwa Balozi wa Tanzania, ambaye sasa ni Balozi nchini Somalia Agustine Mahiga.

Kwa mujibu wa Juma Mahiga alikiri kuwapo mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar na kwamba, suala hilo ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha kupatikana Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, mwaka 2010.

Alitaja sababu zilizotolewa na Musa ambaye kwa sasa ni mkazi wa Ole kisiwani Pemba wakati wakidai kutengwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni kisiwa hicho kutengwa kisiasa na kiuchumi.

Alisema miongoni mwa ushahidi wa madai yao, ulikuwa mfumo wa uongozi wa kitaifa, uliodhihirisha kuwapo upendeleo wa wazi kwa Unguja. “Mussa alimueleza Ban Ki-Moon kuwahata Baraza la Mawaziri asilimia 95 lilikuwa likiundwa na viongozi kutoka Unguja,” alisema Juma.

Alisema wao (wajumbe wateule wa Rais Jakaya Kikwete) waliobaki bungeni hawawezi kubeba jukumu la wawakilisha 18 na wabunge 18 waliochaguliwa kwa kura na wananchi wa Pemba. Alimtaka Rais Kikwete kutokubali kuzongwa na itikadi za kisiasa, badala yake, alimshauri kubaki na msimamo wake wa awali uliomfanya aungane na wananchi kuandika historia, akisema ni hilo pekee litakalosababisha Tanzania kutogawanyika na heshima yake (JK) kutukuka ndani na nje ya nchi.

KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA
Alisema kwa sasa ndani ya kamati hawachambui wala kuboresha rasimu ya katiba kama inavyoelekezwa kwenye sheria, sura ya 83 ya mwaka 2014 badala yake wanachokifanya ni kuweka viraka katiba ya sasa iliyoandikwa mwaka 1977.

Juma ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema badala ya kurekebisha na kubadilisha, watu wanafuta na kuweka vipengele kutoka kwenye katiba ya sasa au wanakojua wao, bila kujali kuwa wanabadili
maudhui yaliyomo kwenye maoni ya wananchi ndani ya rasimu ya katiba “Mfano halisi ni Ibara ya 64 ya katiba
ya sasa imehamishiwa kwenye rasimu
kama ilivyo. Kinachoendelea sasa ni uchakachuaji siyo uandishi wa katiba,”
alisema Juma.

Aliongeza: “Hii inakosesha mchakato uhalali wa kisheria kwa sababu sheria husika inaendelea kuvunjwa kwa watu kuja na ajenda zao mifukoni, kufuta
mwongozo halali wa kisheria na kuyaingiza ya kwao.” Alisema hata uhalali wa kisiasa na
kijamii umekosekana kwenye mchakato huo, jambo ambalo halihitaji mtu kusomea sheria kulibaini kwa sababu tayari vyama karibu vyote vya upinzani vya kisiasa vipo nje ya mchakato huo. Alisema Chaumma inaunga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) waliosusia Bunge hilo, lakini haitatoka bungeni kwa sababu ina haki ya kufahamu kinachofanyika humo. “Ukawa wana haki ni halali walivyosusia
vikao hivi na tunawaunga mkono kwa
asilimia mia moja. Lakini hatutatoka kwenye vikao, maana ni lazima tufahamu kwa hakika kinachofanywa. Tusingekuwapo, nani angeeleza Watanzania haya? Hatukutoka, hatutatoka na hakuna atakayetutoa,” alisema Juma. Aliwasifia Ukawa kwa msimamo wao kuwa una maslahi mapana kwa taifa zaidi ya itikadi za kisiasa na kutaka Watanzania wenye nia nzuri na Tanzania kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema katiba ya sasa na ile ya Zanzibar, zinatambua uwapo wa mamlaka kuu tatu; inayosimamia mambo ya Jamhuri ya Muungano, inayosimamia mambo yasiyokuwa ya muungano ya Zanzibar na
inayosimamia mambo yasiyo ya muungano kwa Tanzania Bara na hivyo haelewi maana ya wanaopinga mfumo wa serikali tatu.

Juma alisema kiini cha tatizo linaloukabili mchakato huo, ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwamba bila kueleza sababu za kutotekeleza Azimio la Bunge hilo, lililoelekeza kuwa Agosti 5 wangeanza
kazi kwa kupiga kura kuamua juu ya sura ya kwanza na sita ya rasimu zilizojadiliwa awali, alisimamia waanze kwa kubadilisha kanuni. Alimshutumu Sitta kuwa wala
hakutengua azimio hilo halali la Bunge kabla ya kuingiza aliyoita mambo yake, hali iliyosababisha mpaka sasa wajumbe wengi kutoelewa wanachofanya, zaidi ya kupokea posho na kushuhudia sarakasi za aina yake zikifanyika.

HALI ILIVYO KWENYE KAMATI
Alisema hata kama kanuni zinazuia wajumbe kuzungumzia yanayojiri ndani ya kamati zao, hakuwa na budi kuyazungumzia kwa maslahi ya taifa.

Juma alisema mpaka jana hawakuwa
wamefanya maamuzi yoyote katika mambo waliyojadili, hali aliyoihusisha na kutokuwapo uwezekano wowote wa kupata theluthi mbili kutokana na wajumbe wa Ukawa waliosusia vikao hivyo.

Alisema kamati namba nne ina wajumbe 19 kutoka Zanzibar, lakini waliomo ni 12 na ili theluthi mbili ipatikane zinahitajika kura 14 kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar.

Alimuomba Rais Kikwete na CCM kulegeza msimamo wao wa kutokubali mabadiliko kwa kuridhia Bunge hilo lisitishwe, ili muafaka wa kweli upatikane na hatimaye katiba halali kisiasa na kisheria ipatikane.

Source: ipp media
 
Back
Top Bottom