๐—ฃ๐—ฒ๐—ด๐—ฎ๐˜€๐˜‚๐˜€ ๐˜€๐—ฝ๐˜†๐˜„๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ๐—ฝ๐—ฟ๐—ผ๐—ด๐—ฟ๐—ฎ๐—บ ๐—ต๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—ท๐—ฎ๐˜€๐˜‚๐˜€๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฎ ๐—œ๐˜€๐—ฟ๐—ฎ๐—ฒ๐—น๐—ถ

๐—ฃ๐—ฒ๐—ด๐—ฎ๐˜€๐˜‚๐˜€ ๐˜€๐—ฝ๐˜†๐˜„๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ๐—ฝ๐—ฟ๐—ผ๐—ด๐—ฟ๐—ฎ๐—บ ๐—ต๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—ท๐—ฎ๐˜€๐˜‚๐˜€๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฎ ๐—œ๐˜€๐—ฟ๐—ฎ๐—ฒ๐—น๐—ถ

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
1_20250606_114010_0000.png


Nchi ya Israel inasifika kwa kuwa na Teknolojia ya hali ya juu kabisa, Pegasus spyware ni app za kijasusi zilizoundwa na Israel na Kampuni ya NSO Group ya Cyber Arms imeundwa maalum kwa ajili ya kutoa siri mbalimbali toka kwenye simu za smartphone.

Kampuni hiyo ina software ambayo inaweza rekodi simu zako , ku copy message zilizopo Kwenye simu yako na kukufuatilia kimya kimya bila Muhusika kujua. Ina uwezo wa kukufuatilia masaa 24 bila kugunduliwa kirahisi.

5000 (1).jpg


Program hii ya udukuzi ambayo imetengenezwa kuuzwa na kupewa leseni kwa serikali duniani kote na kampuni ya NSO Group ya Israeli yenye uwezo wa kudukua simu zaidi ya milioni 20 kwa wakati mmoja.

Toleo la mwanzo liligunduliwa mwaka 2016 ambalo lilinaswa na watafiti, simu ziliweza kuambukizwa kupitia mfumo wa spear phishing (jumbe za maandishi au barua pepe) zilizowaraghai walengwa.

images (1).jpeg


Tangu wakati huo mpaka leo hii Teknolojia yao imezidi kuwa juu , kwani maambukizi ya Pegasus yanaweza kupatikana kupitia mashambulizi ya "zero click" ambayo hayahitaji mwingiliano wowote kutoka kwa mmiliki wa simu ili kufanikiwa.

images (4).jpeg


Mfano kwenye Whatsapp wanaweza tumia mfumo wa Whatsapp call kuweza kushambulia kifaa wanachotaka kirusi cha pegasus code kinaweza kuingia kwenye simu yako hata kama Muhusika hajapokea simu.

Kwenye iphone mara nyingi wanatumia app ya iMessage kuweza kudukua taarifa za watu mbalimbali wanaotumia mfumo wa iOS hivyo Apple mara nyingi wanawaomba Watumiaji wa iphone kuweza kufanya update kila mara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom