Paza sauti masheihk wa uamsho kesi yao isikilizwe sitakaa kimya

Vladimirr

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
546
565
6cbf35e6c111826f94141904a2d8f930.jpg
Kuna kimya kinachonishangaza. Nacho ni cha ‘wanaharakati’ wa Kizanzibari walioziba midomo yao kuhusu madhila yanayowakuta wale waliokuwa wakiwaita “mashekhe wetu wa Uamsho”.
Tangu mashekhe hao 10 waanze kukamatwa Oktoba 16, 2012 mpaka leo kesi yao haijatajwa mahakamani. Hadi sasa wamesomewa tu mashtaka dhidi yao, mashtaka ambayo yanahusika na vurugu zilizotokea Zanzibar Mei mwaka jana.

Washtakiwa hao walifikishwa mara ya mwisho mahakamani Julai 3 mwaka huu na wanatarajiwa kupandishwa tena mahakamani

Washtakiwa wenyewe ni Farid Hadi Ahmed, Msellem Ali Msellem, Mussa Juma Issa, Azan Khalid Hamdani, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakari Suleiman, Ghalib Ahmada Omar, Abdalla Said Ali na Fikirini Majaliwa Fikirini.

Mashtaka yanayowakabili ni kuchochea vurugu, kuharibu mali za umma na za watu binafsi zenye thamani ya shilingi milioni 500, kufanya vurugu katika eneo la Magogoni na kuhatarisha usalama wa taifa la Zanzibar.

Wanashtakiwa pia kuhusu kadhia ya Farid Hadi Ahmed aliyetoweka Oktoba 16, 2012.

Shekhe huyo aliibuka siku nne baadaye akidai kwamba alitekwa nyara na watu waliovaa barkoa waliojitambulisha kuwa ni polisi. Serikali imelikanusha dai hilo.

Mashekhe hao wamefungiwa kwenye gereza la Kiinua Miguu wakiwa chini ya ulinzi mkali. Kama wiki mbili za mwanzo baada ya kutiwa nguvuni wakidhalilishwa kwa kunyimwa hata nafasi ya kubadili nguo au ya kuonana na familia zao.

Tena kila mtuhumiwa alikuwa akiwekwa katika chumba cha peke yake. Tunavyosikia ni kwamba siku hizi wameondoshewa madhila hayo ingawa bado mazingira yao si ya kuridhisha.

Cha kushangaza ni kwamba hatusikii sauti zozote zenye kuwatetea. Labda kwa sababu wao ni mashekhe na si wanasiasa. Labda wangekuwa wanasiasa tungewaona wanaharakati, kwa mfano, wakiwasiliana na jumuiya za kimataifa za haki za binadamu na kuzizindua kuhusu janga lililowafika mashekhe hao.

Labda madevu ya hao mashekhe yanawatia hofu wanaharakati, wanachelea wasije wakashtumiwa kuwa wanawatetea ‘magaidi’ maana siku hizi kwa wakubwa wa dunia hii madevu, Uislamu na utetezi wa haki ni mchanganyiko wa hatari.

Na si kwa hao wakubwa tu bali hatakwa baadhi ya taasisi, magazeti, na wanasiasa wa Tanzania Bara ambao bila ya ushahidi wowote wameihusisha Uamsho na vitendo vya kigaidi.
Juu ya yote hayo, kuna sababu halali za kuwatetea. Sababu kubwa ni kazi walioifanya ya ‘kuwaamsha’ Wazanzibariwenzao wautambue utaifa wao na waachane na chuki na uhasama uliokuwepo baina yao kwa muda mrefu.

Jengine jema walilolifanya ni kuwahimiza vijana wa Kizanzibari warudi kwenye maadili ya Kiislamu badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoleta madhara katika jamii kama vile vya kubugia mihadarati na uasherati.

Pengine kuna wanaharakati wenye kujuta, wenye kuona kwamba walipoteza nguvu zao walipokuwa wakiwaunga mkono hao mashekhe. Wale waliokuwa na majazba waliokuwa wakiota kwamba siku moja nchi yao itaamka ghafla ionekane na sura nyingine sasa itawabidi waote ndotonyingine.
Sina dhamira ya kuingilia kesi inayowakabili washtakiwa hao. Hiyo ni kazi ya mahakama na ya mawakili.

Dhamiri yangu ni kukizungumzia hiki kimya kilichotanda kama wingu juu ya kesi hii.Na zaidi nataka kugusiahaki wanayonyimwa washtakiwa ya kuachiwakwa dhamana huku kesi ikiwa inaendelea. Kucheleweshwa kusikilizwa kwa kesi hiyoni adha kubwa kwa washtakiwa.
Inavyoonyesha nikama serikali imeamua kuwatia adabu ingawa hawakupatikana na hatia.

Ikiwa dhana hiyo ni sahihi basi serikali itakuwa imeamua hivyo kwa sababu za kisiasa. Serikali inazidi kujifaragua ikiamini kwamba kuwatia adabu viongozi wenye muelekeo wa Kiislamu hakutowakera wakubwa wa dunia hii.

Labda serikali inaamini kwamba balozi za Marekani na Uingereza zitayafumbia macho wanayotendewa mashekhe hao kwa sababu zimekwishatiwa sumu ya Uamsho kusingiziwa ugaidi.

Ndio maana kesi hiyo ikawa inaakhirishwa na kuakhirishwa kwa lengo la kuwaweka ndani tu mashekhe hao. Mara ya mwisho Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar alisema wanasubiri waletewe daftari la kesi kutoka Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam.

Nijualo ni kwamba ingawa uamuzi ni wa mahakama wengi wenye kuifuatilia kesi hii wanaamini washtakiwa hao wanaendelea kuwekwa ndani kwa sababu hivyo ndivyo watakavyo viongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar.

Mara mbili tatu hivi Rais Ali Mohamed Shein mwenyewe amesema hadharani kuwa atawashughulikia wanaochochea fujo.Wakati mwingine huwataja Uamsho.

Zanzibar ya leo ni nchi yenye kuhuzunisha; haisikitishi tu bali inahuzunisha. Ni nchi yenye kutatanisha, wakati mwingine hujikanganya yenyewe.Na viongozi wake? Naona hata haina haja ya kuwaeleza walivyo; bora tulifunike kombe…
0ec91e738448f17e53c92f766a64d044.jpg
 
Kuna kesi nyingi sana nchini ziko fabricated ili kuwanyoosha waislam. Uislam unapitia kipindi kigumu sana though Mungu kaahidi kuulinda

Mkuu;
Usiwazibie wenzio sauti kwa kuleta mambo ya ubaguzi wa dini hapa. Tunaomba, watu hawa wanaojulikana hata katika mashitaka kama; Mashekhe wa uamsho. Wapewe haki yao. Hatuwaombei kama waislam hapana tunawaombea kama watu wenye nafsi hai wapewe haki. Siungi mkono udini wa aina yeyote. Ka unataka hilo, anzisha uzi mwengine. Huu usiutie doa.
 
Hao unaowazungumzia kwa nini usiwaite Uamsho? Usitumie masheikh kuwaficha Uamsho
 
Kusema ukweli kama sio JWTZ kuwepo Zanzibar, nahisi kingekuwa kishanuka, ndio maana ccm znz wameung'ang'ania muungano.

Nchi haina haki kabisa, kila kitu kinaendeshwa kisiasa
 
Lumumba buku 7 kuna waislamu majina tu watachomwa moto kiama hawa wanashindwa kutamka hata neno tu kuwalaani hawa makafir huyu FaizaFoxy anakitetea Ccm badara ya uislam na waislam wenzake
 
hapa siwaelewi kwan hawa mashekh wamefungwa kwa sabab ya dini yao!?, je ni lazima mtu yeyote ambaye ni wa dini yao awatetee!?
hebu tuwe great thinkers tujadili tatizo bila kuingiza u dini
 
Hao mashekh ni bora wanyongwe tu wao kila kukicha wanaponda ukristo badala ya kuhubiri habari njema wao ni uchochezi tu mi naona wachomwe hata sindano ya sumu wafie mbali
 
Huwa siwaonei huruma hawa mashehe hata kidogo, huwa wanatafuta sympathy kwa wananchi,ila wakiachiwa tunaanza kusikia fulani kamwagiwa mafuta ya betri,kwa maslai ya visiwani wawekwe ndani maisha yote.
 
Ccm inavyowafanya wanazuoni wetu vp mkuu.au kwako chama ni bora kuliko pepo ukumbuke kuna kiama

Mkuu;
Huwa simtetei FaizaFoxy, lakini leo namuunga mkono 100%. CCM ni chama tu ka kingine. Wanaokiongoza ni watu. Zenj ni 99% waislam. Hao Mashekhe walikamatiwa Zenj. Nchi ya kiislam. Iweje uilaumu CCM kuwa inaonea huku ukitaka FF awatetee ati kwa kuwa yeye ni ccm!! Acheni kuelekeza mitutu kwingine ielekezeni kunako stahili. Laumu Wazenj wenyewe
 
Mkuu;
Huwa simtetei FaizaFoxy, lakini leo namuunga mkono 100%. CCM ni chama tu ka kingine. Wanaokiongoza ni watu. Zenj ni 99% waislam. Hao Mashekhe walikamatiwa Zenj. Nchi ya kiislam. Iweje uilaumu CCM kuwa inaonea huku ukitaka FF awatetee ati kwa kuwa yeye ni ccm!! Acheni kuelekeza mitutu kwingine ielekezeni kunako stahili. Laumu Wazenj wenyewe
Sasa ndio umeongea nini mkuu Zanzibar hawana sauti Ccm ndio watawara wa bara na kwa namna yoyote wale waliletwa huku kwa kuwa ndio kuna watesaji wazuri Ccm ndio inatawala bara na Zanzibar sema Waislamu wanaoitetea Ccm humu njaa imewazidi kiasi wanashindwa kutetea haki
 
Kama unawapenda uamsho, kunja vidole vyako vya kulia, kisha nyosha juu mkono wako wakulia, tamka kwa nguvu "CUF ngangariiiiiiiiiii"
 
Viongozi wa Serikali wameapa kulinda Katiba

Hawewezi kuona kikundi cha watu kinahamasisha wanainchi kuvunja Muungano then wakakuchekea tu never.

Kuna ushahidi wa mihadhara zaidi ya 50 walioifanya uamsho kuhamasisha wazanzibar kuukataa Muungano.

Kuvunja Muungano huu huwezi kubaki salama kwasababu Zanzibar haina Jeshi unategemea kesi yako itakuwaje hapo.
 
Hapa ndipo utakapoona chuki za watu, kesi zao zisikilizwe na hukumu ifanyike ili mtu ajue kabisa anatumikia kifungo kuliko na kuwekwa ndani yenye sintofahamu
 
Back
Top Bottom