Pavlova, Kwa wapenda vitam tam

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,666
Mahitaji
Ute wa Mayai 6
Sukari 4 dl
Unga wa maizena(corn flour)vijiko viwili vya chai
Siki vijiko viwili vya chai
Vanilla(harufu) kijiko kimoja cha chai
Dobble cream boksi moja
Matunda ya aina tofauti haswa magwadu ili kubalansi sukari mfano kama blueberries,raspberries,kiwi,strawberries na zabibu kiasi.

Jinsi ya kutayarisha

  1. Washa jiko 250 degrees centigrade

  1. Tayarisha matunda yaoshe na kiwi limenye ulikate vipande,strawberries usigawe na hata zabibu.
  2. Tenganisha viini vya mayai na ute wa mayai,Yapige na mashine ya keki mpaka mapovu yakazane ukijaribu kuligeuza bakuli juu chini vilivyomo ndani ya bakuli havianguki.
  3. Changanya sukari na unga wa maizena mimina kidogokidogo kwenye ute wa mayai uloupiga mpaka upate mchanganyiko mweupe mlaini unaongaaa.
  4. Mimina siki na vanilla na piga kwa dakika kadhaa.
  5. Punguza oven moto na uweke 125 degrees centigrade.
  6. Weka baking paper kwenye trey na ule mchanganiko wa mayai uweke kwenye trey na usambaze utengeneze mduara.
  7. Weka Marengs kwenye oven na uchome kwa lisaa limoja na dakika 25.
  8. Toa mchanganyiko wako na uwache upoe.
  9. Piga dobble cream na cake mixer mpaka ikazane,kuwa makini usipige muda mrefu itakatika.
  10. Weka cream juu ya mchanganyiko ulouchoma isambaze na mwagilia matunda juu.
  11. Pavlova tayari kwa kuliwa..
attachment.php
attachment.php
 

Attachments

  • pavlova.jpeg
    pavlova.jpeg
    7.5 KB · Views: 638
  • Pavlova 2.jpeg
    Pavlova 2.jpeg
    5.3 KB · Views: 628
Back
Top Bottom