Paulo Dybala, Mchawi wa soka asiyezungumziwa na wazandiki wa soka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Habari wadau,
dybala.jpeg

Mimi ni shabiki wa soka. Huwa naangalia mechi zote za mataifa makubwa Ulaya na soka la Bongo nikiwa naishabikia Kagera Sugar.

Sasa katika soka la Ulaya kuna mchezaji matata anaitwa Paulo Dybala. Huyu ni mchawi wa soka ambaye yupo katika ubora wake kwa sasa kuliko mchezaji yeyote duniani. Bahati mbaya kafichwa na vyombo vya habari ambavyo vipo kibiashara kwa Messi,Neymar,Ronaldo,Suarez na Pogba.

Kwa wasiofuatilia soka nje ya mipaka ya Uingereza na Spain sio rahisi kumjua huyu kijana.

Ana uwezo binafsi wa kubadilisha matokeo. Anajua anataka nini, anamiliki mpira kwa umahiri,anakokota vyema,anapiga mashuti ya mbali, penati zake ni uhakika 100% kutinga nyavuni.

Akiwa na miaka 23 tu namtabiria makubwa sana kutawala soka la dunia na kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.

Sina mengi ya kumzungumzia, unaweza kumtizama
 
Namuelewa pia

Ila vizuri zaidi ungetuwekea takwimu zake hapa

Amecheza mech ngap
Udadi ya goals alizofunga

Assist na vitu vinginevyo

Hapo ndio tujue anaingia katka iyo level unayoisema

But kwa sasa Juve ni HIGUAN tu
 
Dogo yupo vizuri. Ila amechelewa kidogo. Angefanikiwa kucheza na maestro Pillo, Arturo Vidal na Marchisio angetisha sana.
 
Leroy Sane...
Huyu ana umri wa miaka 21,ni winga wa Manchester City.
Uwezo wake wa kumiliki mpira,kukokota mpira na kutengeneza magoli ni wa hali ya juu.
Huyu atakuja kutisha sana siku za baadae..!
3DFC7AB900000578-0-image-a-50_1488758603067.jpg

Wiki hii Man City anacheza na Monaco kwenye UEFA.
Kwa watakaoangalia hiyo mechi watakubaliana na mimi.
 
Habari wadau,
View attachment 480846
Mimi ni shabiki wa soka. Huwa naangalia mechi zote za mataifa makubwa Ulaya na soka la Bongo nikiwa naishabikia Kagera Sugar.

Sasa katika soka la Ulaya kuna mchezaji matata anaitwa Paulo Dybala. Huyu ni mchawi wa soka ambaye yupo katika ubora wake kwa sasa kuliko mchezaji yeyote duniani. Bahati mbaya kafichwa na vyombo vya habari ambavyo vipo kibiashara kwa Messi,Neymar,Ronaldo,Suarez na Pogba.

Kwa wasiofuatilia soka nje ya mipaka ya Uingereza na Spain sio rahisi kumjua huyu kijana.

Ana uwezo binafsi wa kubadilisha matokeo. Anajua anataka nini, anamiliki mpira kwa umahiri,anakokota vyema,anapiga mashuti ya mbali, penati zake ni uhakika 100% kutinga nyavuni.

Akiwa na miaka 23 tu namtabiria makubwa sana kutawala soka la dunia na kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.

Sina mengi ya kumzungumzia, unaweza kumtizama

Mkuu nimekuelewa dogo yupo sawa sina uhakika kama atadumu kwenye soka la Italy ataenda Spain kati ya barca au real
 
Huyu dogo kailetea Juve balaa huko Serie a,penati yake ya dk ya 97 juzi iliiua Milan 2-1,Donnaruma aliwasumbua sana maforward wa Juve throughout tthe match anadaka hadi milingoti kuhakikisha Juve hawashindi ile mechi.
Kuona vile wakamuundia zenngwe,Higuain kalenga shuti mkononi mwa beki,penati wakapata Juve,mjomba Dybala akamwambia Donnaruma hapa bwamdogo nakutia adabu siku nyingiine usijifanye wewe ni Buffon,na nakupelekea huko huko kulia unakoruka tuone kama utaidaka!Donnaruma kajinyoosha hadi kucha lakini wapi,.nyavu ndogo zinatikisika na mpira umeisha!akapigapiga nyasi za Juventus stadium hakuridhika,akataka kumtwanga refa,kocha wake Montela akamzuia,hasira zake akawaambia wachezaji wenzie kule locker room wakachanachana banners zote za Milan zilizobandikwa ukutani,wakaona haitoshi wakang'oa na viti vya locker room,Hivi Juve hawajamaliza kutengeneza viti vyao leo zamu ya Casillas nae kanyooshwa na Dybala huyu huyu!sijui viti vimesalimika huko.Waache kumpa penati huyu dogo anautia hasara uwanja wa Juve!
 
Namuelewa pia

Ila vizuri zaidi ungetuwekea takwimu zake hapa

Amecheza mech ngap
Udadi ya goals alizofunga

Assist na vitu vinginevyo

Hapo ndio tujue anaingia katka iyo level unayoisema

But kwa sasa Juve ni HIGUAN tu
top scorer kule Italia nadhan n yeye.. magol 22 michezo 25
 
Back
Top Bottom