Paul Makonda watetee lost generation kwa vitendo

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Marehemu Mama yangu alikuwa anapenda kutumia maneno "lost generation" kumaanisha vijana waliozaliwa kuanzia miaka ya 70, yaani wale wenye miaka ya 40 mwanzoni na wadogo zao kwa sasa. Hiyo ilikuwa ni miaka ya 90 mwanzoni.

Alikuwa akitazama mienendo na kutowajibika kwa vijana wengi, enzi hizo za miaka ya 90 mwanzoni, ndipo alipofikia hitimisho la kukipa jina la kizazi kilichopotea, kile kizazi cha vijana ambao kwa sasa wanaingia kwenye uzee pamoja na wadogo zao.

Lakini miaka imepita na wanaibuka vijana kati ya wale wale walio ndani ya "lost generation" na wanafanya mambo makubwa pengine yenye kufanana na wale wa kizazi cha zamani ambao wanajichukulia kama hawakuwa ni kizazi kilichopotea.

Wapo mameneja wengi kwenye mabenki makubwa na mashirika mengi, ambao ni vijana walio kwenye kundi la "arobaini ya mwanzoni kushuka", ambao wanafanya kweli na tija inaonekana kwa kila mwenye upeo mkubwa wa kutazama mambo jinsi yanavyokwenda.

Wapo wanasiasa katika rika hilo hilo, wanaochipukia ambao wanaongea na kutenda kama watu wenye kustahili kupewa heshima mbele ya jamii

Paul Makonda yupo kwenye kundi hili, na kwa kweli anazidi kuonyesha uwezo wake, anakitetea vizuri sana kile kizazi ambacho watu wazima wanakichukulia kama kimepotea.

Dar ni jiji lenye kila aina ya watu, wapo wenye nia nzuri kweli, wapo wengine wamejaliwa sura za tabasamu lakini mioyoni ni wabaya kuliko chatu wa Amazon. Na yeye sio kama Mheshimiwa JPM, ambaye anazungukwa na rundo kubwa la walinzi wanaojulikana na wasiojulikana kirahisi. Paul Makonda ni reachable, anafikika kirahisi. Sasa huko kufikika kwake kiurahisi kunaweza kuwa tatizo kwake iwapo ameamua kuyavulia nguo maji ili ayaoge. Nadhani nimeeleweka.

Namtakia utumishi mwema wenye kutanguliza maslahi ya watu wa hali ya chini kwanza, kabla ya kunaswa na wenye fedha ambao siku zote wanataka matakwa yao kwanza ndio yapewe kipaumbele.

Paul Makonda kitetee kwa nguvu zako zote kile kizazi ambacho wazee wetu walikibatiza jina la "lost generation".
 
Kwenye hitimisho Lako hapo..... Sema wazee wako, na sio wazee wetu, wazee wangu hawajawahi kutumia Hilo neno la lost generation
 
Back
Top Bottom