Paul Makonda: Ukimchukia Rais Samia unamkosea Mungu

Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa hapo jana huko babati Mkoani Manyara ametoa hotuba ya mwaka,hotuba iliyoteka na kugusa hisia za watu,hotuba iliyowafanya watu washindwe kujizuia machozi na hivyo kujikuta wakibubujikwa na kutiririka machozi kutoka katika macho yao,hotuba iliyoacha historia na kuwatia moyo wana babati.

Ni baada ya kusema kuwa Ukimchukia Rais Samia unakuwa Unamkosea Mungu Mwenyewe,kwa kuwa Rais Samia alijipangia kuishi maisha ya kawaida kabisa na wala hakuwahi kupanga wala kuwaza kuwa makamu wa Rais wala Rais wa Tanzania.lakini Mungu na mipango yake alipanga iwe hivyo kwa kumuinua na kumpa umakamu wa Rais na baadaye Urais.

Mheshimiwa Makonda aliendelea kusema kuwa hata yeye hapo alipo kwa sasa ni mipango ya Mungu Mwenyewe aliye juu na wala siyo mipango yake,maana alikuwa tayari yupo nje ya msitari. Aliendelea kuzungumza huku wananchi wakitekwa na hotuba hiyo iliyojaa hisia kali sana na mguso wa aina yake kwa kusema kuwa hata wao wasikate tamaa na wajipe moyo na wala wasiumie wanapodharauliwa na mtu.

Kwa hakika Mheshimiwa Makonda ni mtu ambae ukisikiliza hotuba zake lazima uguswe sana ndani ya moyo wako, ni mtu anayezungumza toka ndani kabisa ya moyo wake, ni mtu anayeongea na kuzungumza kwa kugusa hisia za watu,anaongea uhalisia wa maisha, anazungumza kile kinachogusa yale yaliyopo kwa watu na wananchi.ndio maana watu wanafurika na kumiminika sana kwenye mikutano yake.

Ni mtu ambae ukimsikiliza unapata matumaini na nguvu kubwa sana ya kusonga mbele kimapambano,anatia moyo na faraja sana.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Kwahiyo Makonda anataka kutuambua kwamba Samia ni MTAKATIFU!
 
Attachments

  • FB_IMG_1706032626462.jpg
    FB_IMG_1706032626462.jpg
    44 KB · Views: 1
Damu za nani? Acha kuropoka ujinga usio na ushahidi nao. ukiambiwa ulete ushahidi utaleta?
Ushahidi nilete kwenye vyombo hivi hivi vinavyotumika kulinda wahalifu? Ni hivi, ni muhalifu aliyehusika kumwaga damu za watu, hitaki jinyonge.
 
Ushahidi nilete kwenye vyombo hivi hivi vinavyotumika kulinda wahalifu? Ni hivi, ni muhalifu aliyehusika kumwaga damu za watu, hitaki jinyonge.
Nenda mahakamani kafungue mashitaka na siyo kuchafua watu hapa na kuandika uzushi wako hapa.
 
Nenda mahakamani kafungue mashitaka na siyo kuchafua watu hapa na kuandika uzushi wako hapa.
Mahakama zipo, hizi zilizokaa na kesi ya kina Mdee miaka zaidi ya mitatu huku vielelezo vyote vikiwepo? Labda ya mahakama za nje. Mahakama ziko Kenya, sio hii taasisi ya ccm.
 
Mahakama zipo, hizi zilizokaa na kesi ya kina Mdee miaka zaidi ya mitatu huku vielelezo vyote vikiwepo? Labda ya mahakama za nje. Mahakama ziko Kenya, sio hii taasisi ya ccm.
Nenda na hivyo vielelezo vyako mahakamani maana wenzio walishakwenda na vielelezo wakaishia kudondokea pua baada ya kukosa hoja zenye mashiko.
 
Huyu Mwasambwa. Basha wake atakuwa amesafiri maana ana ashki kwenye Tigo yake.
 
Mmeanza kumdhiaki tena Mungu, bado mjaridhika alipowatwalia jiwe wenu! Makonda na wenzake ni mashetani, Makonda alitaka kumtanguliza T.Lissu yy na washilika wake lakini ALLAH aliepusha hilo ingawa Mh: L, hadi leo tukimuona tunabubujikwa na machozi, Leo hii nami nikimshuhudia Makonda na washirika wake ni lazima nitatokwa na machozi kwa kukutwa na kumbukumbu ya maovu yao.
 
Nenda na hivyo vielelezo vyako mahakamani maana wenzio walishakwenda na vielelezo wakaishia kudondokea pua baada ya kukosa hoja zenye mashiko.
Kwa mahakama hizi ulitegemea tofauti na hukumu hizo? Huwa nawaelewa sana wazungu kwa kutumia mahakama za nje , vinginevyo wangekuwa wanashindwa Kila kesi kwenye hizi mahakama za kimagumashi.
 
Mmeanza kumdhiaki tena Mungu, bado mjaridhika alipowatwalia jiwe wenu! Makonda na wenzake ni mashetani, Makonda alitaka kumtanguliza T.Lissu yy na washilika wake lakini ALLAH aliepusha hilo ingawa Mh: L, hadi leo tukimuona tunabubujikwa na machozi, Leo hii nami nikimshuhudia Makonda na washirika wake ni lazima nitatokwa na machozi kwa kukutwa na kumbukumbu ya maovu yao.
Acha kuandalia vitu usivyo na ushahidi navyo.
 
Kwa mahakama hizi ulitegemea tofauti na hukumu hizo? Huwa nawaelewa sana wazungu kwa kutumia mahakama za nje , vinginevyo wangekuwa wanashindwa Kila kesi kwenye hizi mahakama za kimagumashi.
Nenda popote pale kafungue kesi unaapoona una imani napo
 
Back
Top Bottom