pierre buyoya
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 476
- 163
Na Pierre Buyoya
Instagram: @pierrebuyoya
Kama kuna jambo la msingi zaid Tanzania ni kupata Rais ambaye anaweza kutikisa serikali yake kwa namna ya aina yake kama anavyofanya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli . . .
Rais ambaye hana urafiki na mafisadi wala wapiga dili, Rais ambaye anaweza kusema bila uoga na kutoa msimamo wake pale pale anapoona jambo haliendi sawa, Rais ambaye anakiu ya kuona Tanzania inaenda kwenye nchi ya kipato cha kati kwa haraka zaidi na baadae kuwa Taifa la mfano Africa nzima . . .
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ameonesha ukomavu mkubwa wa siasa na uzalendo wa hali ya juu katika kipindi chote nilichomfahamu kama kiongozi wa UVCCM mpaka sasa mkuu wa jiji kubwa kabisa nchini . . .
Tukumbuke akiwa UVCCM aliweza kutamka wazi kuwa Edward Lowassa hafai kuwa Rais wa nchi hii na aliamini kamati kuu ya CCM isingeweza pitisha jina la waziri mkuu huyo mstaafu, kitu ambacho hata wakubwa zake kiumri na kisiasa walishindwa kukisema wazi kama yeye, Kipindi hicho Lowassa alikuwa Untoachable ndani ya CCM, Nakumbuka hadi waziri mkuu wa zamani Mzee Malecela alimsifu na kuwashangaa wakubwa wanaoshindwa kuwa straight kama Makonda . . .
Juzi kwenye uzinduzi wa daraja la Kigamboni Mhe. Paul Makonda alieleza wazi maovu ya aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar Mhe. Wilson Kabwe mbele ya Rais Magufuli kitu ambacho kilisababisha kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo . . .
Kwa haya machache na mengine mengi naweza kusema kama Paul Makonda ataendelea na Spirit hii ya kazi basi anafaa kabisa kuwa Rais wa Tanzania Mara baada ya Rais Magufuli kumaliza muda wake kwa mujibu wa sheria . . .
Narudia tena kusema kama "Paul Makonda ataendelea na Spirit hii" ya kazi basi anafaa kabisa kuwa Rais wa Tanzania Mara baada ya Rais Magufuli kumaliza muda wake kwa mujibu wa sheria . . .