Paul Makonda anafaa kuigwa !

Paul Makonda anafaa kuigwa !

Alipoteuliwa kuiongoza kinondoni wengi tulishtuka,tukajua atachemka muda si mrefu.

Wengi walihoji kiwango chake cha maadili hasa walipohusisha na sakata la Mzee Warioba.

Lakini bila shaka wote tumeona jinsi kijana mwenzetu alivyombunifu na kujitahidi kushughulikia mambo kwa njia za kiungwana.Ameitisha mkutano kusuruhisha migogoro ya ardhi,amekemea na kuwasaka wezi wa maji,ameanzisha mchakato wa kuvitambua na kuvikuza vipaji vya vijana kule Kinondoni.

Najua bado hajafanya mengi ya kutosha,ila huu mwanzo wake unaweza kutusaidia kuujua mwisho wake.Tumtie moyo na kumshauri njia bora zaidi za kuzidi kuondoa kero za wananchi,kwani hilo hasa ndilo tunalihitaji kwa kiongozi anayeonesha nia ya kulisimamia.

Kukaa kimya na kusubiri ashindwe ili tujekumdhihaki na kumbeza,si uungwana.Tumkosoe na kumuunga mkono inapofaa

Nina reservations zangu; hata hivyo hili la Gwajima awachane nalo kwa sababu Gwajima swala lake bado liko PoliCCM; sio sahihi mtu mmoja kushitakiwa au kuhojiwa sehemu mbili tofauti kwa kosa lile lile! (kama lipo!!); haki za msingi za Askofu JG ziheshimike! duplicating roles sio utawala bora! vinginevyo Makonda risks kuonekana anajitafutia umaarufu kupitia a very unfortunate public altercation baina ya cardinal na Askofu; sio vema.
 
kila mtu ana mapungufu na mazuri yake,tusijikite kutoa hukumu kwa kuangalia upande mmoja
 
Back
Top Bottom