Paul Christian Makonda (PCM) hawa vipi?

Paul Christian Makonda (PCM) hawa vipi?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,619
Uteuzi wa Kada Paul Christian Makonda PCM kwenye wadhifa wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM umeendelea kutengeneza vichwa vya habari vinavyouza media mbalimbali (social na mainstream).

Uteuzi huu ambao umebadili kabisa ladha na mwelekeo wa siasa ndani na nje ya CCM umezua maswali mengi ambayo wengi hawana majibu yake.

PCM amekuja na ladha kama ya Magufuli ambaye zimwi lake limedhihiri kuwa na nguvu kwenye grassroots hususan katika wakati huu nyeti wa chaguzi.

Zimwi ambalo linapewa nguvu na changamoto mbalimbali zinazokabili jamii bila utatuzi wa kudumu wakati fulani hata wa muda mfupi.

Kiongozi huyu Mwanamapinduzi na chapa-ya-moto (Firebrand) amekuwa akihoji viongozi wa chama na serikali (wakiwemo Mawaziri) kwenye mikutano ya hadhara inayoitishwa na chama kumtambulisha na pia kutathmini uhai wa chama kwa mikoa yote.

Swali langu ni hili:
Katika kuhoji hao viongozi waandamizi na wafawidhi je, PCM anaweza kuwahoji wafuatao kama kutakuwa na kero kwenye wizara zao?

1. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

2. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

3. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ameanza na TAMISEMI ambaye ni mkwe wa mkuu wa kaya. Kamhoji wa Afya ambaye ijapokuwa wakati akiulizwa alikuwa akijibu kwa dharau na kiburi fulani hivi lakini meseji ameipata na mteuzi wake alikuwa akisikia.

Hao uliowataja watahojiwa subiri ifikie hatua hiyo kwananza Komredi PCM atazuru Lushoto Bumbuli kufuatilia utekelezaji wa miradi, ataenda Mtama kufuatilia utekelezaji wa miradi kisha ataenda Chalinze kufuatilia utekelezaji wa miradi atamhoji mbunge huyo kwanini walitumia kiasi kikubwa cha fedha kujenga stendi ndogo ya mabasi halafu baadae wameivunja tena kuiboresha kwa kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni za walipa kodi. Atahoji pia kwanini pori kuanzia Ruvu juu darajani mpaka Chalinze takribani kilomita 50 kupita msitu kuna vituo vingi vya mafuta kila baada ya mita chache je mji wa Chalinze unanufaikaje nao?
 
Uteuzi wa Kada Paul Christian Makonda PCM kwenye wadhifa wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM umeendelea kutengeneza vichwa vya habari vinavyouza media mbalimbali (social na mainstream)...

Hao watu watatu, bado hawana nguvu binafsi, kwa ufupi ndio wanajifunza na kujijenga kiutu uzima. Hapo makonda amepewa kazi ya kudili na kuwatetemesha vianganishi vya hao wanaowabeba hao.

Kuna wazee hapo ambao ni tishio kwa 2025. Na hawawezi kua tishio bila kuangalia vivuli vyao vilivyopo humo. Maana ukidhibiti vivuli hao wazee watabadili msimamo na kijifanya wana busara na watatulia.njia ya kuelekea 2025 itakua salama kwa mama.

Naamini huyu aliepelekwa nje ni aset ya 2030 huko, hivyo hatakua na madhara 2025.
 
Hao watu watatu, bado hawana nguvu binafsi, kwa ufupi ndio wanajifunza na kujijenga kiutu uzima. Hapo makonda amepewa kazi ya kudili na kuwatetemesha vianganishi vya...
Asipopata 2025 huko 2030 ni mbali Sana Mambo yatabadilika Sana hapo katikati kabla ya kufikia 2030
 
Asipopata 2025 huko 2030 ni mbali Sana Mambo yatabadilika Sana hapo katikati kabla ya kufikia 2030
Samia akipita 2025 tu. Atawaacha huru kuweka mifumo yao.hivyo sio lahisi kubadilika kiviile. Hao vijana wanaobweka hakuna mwenye uwezo wa kuweka mikakati.
 
Kamkaripia Hadi Waziri Mkuu, na kumpa miezi sita apeleke ripoti ofisi kwake mapema.
 
Back
Top Bottom