Patient Charter na ARV fake

peace2007

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
212
81
Nimekuwa nikifuatilia mambo mbalimbali yanayohusu afya zetu lakini mojawapo ya jambo linalonitia hofu ni kuibuka kwa watu wengi wanaodai wao ni mabingwa wa kutibu magonjwa mbalimbali na ambao wanajitangaza bila kuogopa.

Vilevile hata huduma katika hospitali zetu na wataalamu wa afya katika vitua vya afya nao wakati mwingine wanaweza kufanya makosa ya makusudi wakati wanapokuwa wanafanya kazi zao, lakini kinachotokea mgonjwa anakubaliana na yote kwani hana pa kwenda na kubwa hajui haki yake.

Katika nchi za wenzetu kuna kitu kinaitwa Patient Charter ambayo inaelezea kinagaubaga mahusiano na haki ya mgonjwa na wale wanaompa huduma hiyo,na haki zake na endapo kosa litafanywa na mtoa huduma kwa maana ya kutoa huduma ambayo immemleta madhara mgonjwa badala ya kumsaidia mgonjwa anaweza kuchukua hatua ikiwemo kutoa malalamiko yake kwa mamlaka husika na kwenda kwenye vyombo vya sheria na sheria kuchukua mkondo wake.

Kwa Mfano wagonjwa wote waliotumia dawa feki za ARV wana haki ya kulipwa fidia (Kwa nchi za wenzetu)Sijui hapa TZ! Je hapa Tanzania tuna Patient Charter? Kama ipo wananchi wanaifahamu na ina address vipi matatizo yao katika sector hii? Nimeweka Patient charter ya EU ili kwa wale wasifahamu waione na kujua yaliyomo. Ninaamini Patient Charter ikiwa inafanya kazi hata uzembeuzembe unaoendelea kwenye afya zetu utapungua na Serikali itawasimamia vizuri watumishi wake ili iondokane na kulipa fidia na aibu nyingine. Vilevile itawasimamia hawa waganga wa jadi amabo kila kukicha wanakuja na tiba mpya amabo nyingine ni utapeli tu na mbaya zaidi zinahatarisha maisha ya mgonjwa.
 

Attachments

  • Patient Charter EU.pdf
    354 KB · Views: 36
Back
Top Bottom