Pasaka Njema Watanzania wenzangu

Pasaka Njema Watanzania wenzangu

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
1,984
Reaction score
1,409
Nichukue fursa hii kuwatakia watanzania wote Heri ya Sikukuu ya Pasaka.
Pasaka ni sikukuu ya ufufuko wa Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.
Mnamo miaka zaidi ya 2000 iliyopita nyakati Kama hizi Bwana wetu Yesu Kristo alisulubishwa kwa shinikizo la makuhani (Maaskofu) na wapambe wao waliyotumia slogan ya Nguvu ya Umma ( People's Power).
Makuhani wa nyakati zile ( Maaskofu wa Leo) walishinikiza Bwana Yesu asulubiwe kwakuwa walidai anawanyang'anya wafuasi wao.
Wanazuoni wa Elimu Mungu (theology) wanasema kuwa wakati wa Bwana Yesu watu walikosekana kwenye mahekalu mapato yakapungua kwa Makuhani sadaka na Zaka zikapungua sana jambo lililowaudhi Makuhani na wakuu wa masinagogi.
Katika matengenezo yale ya kiroho malaika na mapepo Shetani yaliwaingia makuhani na wakuu wa masinagogi wakaanza kuwashawishi wafuasi wao kwa People's Power wakapiga mayowe asulubiwe tena kwa dhiaka kubwa.
Kuanzia pale Msalabani ndipo neno people's power kilipoanza kutumika rasmi hadi nyakati hizi.
Ndugu zangu Watanzania mtakapokuwa katika nyumba za Ibada mkianza kuwasikia Hawa makuhani wetu wa Leo (Maaskofu) wakianza kuhubiri maisha ya hapa Duniani Kama maisha magumu,ukosefu wa ajira katiba mpya basi mjue Makuhani wetu wa leo hawana Roho wa Mungu bali wana roho ya mapepo ya Ibilisi, naomba muwakemee kwa nguvu tena kwa sauti Kuu ya malaika wa Mungu muumbaji.
Maaskofu wetu wanapaswa kutuhubiria maisha ng'mbo ya Kaburi maisha ya matumaini baada ya kifo.
Mwenyezi Mungu mwenyewe alisema kwa jasho letu tutakula hakusema kwa jasho la Wafalme mtakula hapana alijua Mfalme hana chakula .
Hivi karibuni wamejitokeza baadhi ya makuhani(Maaskofu) kulaani Rais wetu Mpendwa lakini tukumbuke kazi kubwa ya kurejesha nchi katika mstari wa maendeleo imeawathiri hata Hawa ndugu zetu Maaskofu siku hizi hakuna sikukuu za mavuno.
Sadaka za Mavuno zimeshuka sana hasa makanisa ya mikoani, wanaotegemea mazao. Sadaka za majengo nazo hazipo na Zaka na sadaka haya yote zimehathiri mapato ya Maaskofu wetu na wameingiwa na roho za Ibilisi na kupewa sapoti na kile chama kinachotumia slogan ya Nguvu ya Umma(people's Power) Kama nyakati za kusulubishwa bwana wetu Yesu Kristo.
Tuwaombee Hawa ndugu zetu Maaskofu mapepo ya chuki na Husda dhidi ya Rais wetu Mpendwa ambaye Mungu ametupa Kama zawadi Kama mfalme Daudi Mwana wa Jese.
Tusipowakemea Hawa Maaskofu watatuingiza mkenge kwa maslahi yao huku wakidai kuwatetea Watanzania.
Tukumbuke wakati Bwana Yesu alipokamatwa na maaskari wa kirumi Mtume Petro alichomoa Kisu chake na kumkata askari sikio kma kumtetea bwana wake Yesu Kristo lakini Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai alisema Vita yake siyo ya hapa Duniani bali ya ufalme wa Mbinguni.
Ukiona maaskofu wanasema wanasema wanawatetea kwa maisha ya hapa Duniani mjue kabisa hao ni mawakala wa malaika wa shetani . Yesu hakutoa uhai wake ili tuwe na maisha mazuri hapa Duniani bali alitoa Uhai wake ili twende kwa Baba mwenye Enzi Mungu Muumbaji wetu ilo ndiyo Tumaini letu Kuu.
Askofu anayehubiri Katiba Mpya badala ya kuhubiri Biblia Takatifu tambua huyo ni mtumishi wa Ibilisi aliyeingiwa na Pepo wa People's Power malaika wa shetani waliyomsulubisha Bwana Wetu Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye Hai.
Huu ndiyo Ujumbe wangu wa Pasaka 2018.
Pasaka Njema Wana na Binti wa Mungu.
Na Frey Cosseny
 
giphy.gif
 
Naomba kuwatakia Pasaka njema wanachama na wageni wote wa JF.
Ombi langu tuitumie vizuri siku hii, tuepuke matumizi ya lugha za kuuzi na matusi, ili hatimaye tusisababishe majibizano mabaya kwa leo.
Its a breaktime day!!
Karibuni tutakiane salam za pasaka
 
Naomba kuwatakia Pasaka njema wanachama na wageni wote wa JF.
Ombi langu tuitumie vizuri siku hii, tuepuke matumizi ya lugha za kuuzi na matusi, ili hatimaye tusisababishe majibizano mabaya kwa leo.
Its a breaktime day!!
Karibuni tutakiane salam za pasaka
msalimie shemeji yetu....mwambie a take care asije akaunguzs pilau
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Back
Top Bottom