Party caucus zisitengue majukumu ya wabunge

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Tunasubiri taarifa ya kikao cha kamati ya maadili na madaraka ya bunge dhidi ya mtuhumiwa aliyelikashifu bunge,mheshimiwa Paul Christian Makonda mkuu wa mkoa Dar es salaam. Taarifa hii ni muhimu sana kwa wananchi hususani katika kuheshimu mgawanyo wa madaraka kimhimili na kuzingatia mipaka ya kiuongozi katika ya mhimili mmoja kwenda mhimili mwingine.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977,bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi ambacho kazi yake mbali na kutunga sheria ni pamoja na kuisimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa shughuli za kila siku. Inapotokea mhimili huu mkubwa ambao ndicho chombo cha uwakilishiwa wananchi kinapoingiliwa na mihimili mingine hususani mhimili unaosimamiwa na bunge(serikali),na bunge hilo kukaa kimya kwa hofu ya kuiogopa serikali moja kwa moja uwakilishi wa maslahi ya wananchi unakuwa mashakani.

Kwa mujibu wa katiba hii,rais ni sehemu ya bunge, kuwa mkuu wa mhimili mmoja na kuwa sehemu ya bunge hakumfanyi rais kuwa na nguvu zaidi ya bunge japokuwa anaweza kulivunja bunge ikiwa kuna sababu za msingi kama zilivyoanishwa kwa mujibu wa katiba. Hivyo rais kuwatisha wabunge watokanao na chama kilichomuweka madarakani ni kuvunja sheria na kanuni za bunge ikiwa ni pamoja na kuingilia madaraka na wajibu wa bunge lenyewe.

Kadhia hii ndiyo inayopelekea wateule wa rais kudhani wao ni zaidi ya bunge na kujiona wana haki na kinga kulishambulia bunge kwa kejeli na dhihaka.

Kwa kitendo cha mkuu huyo wa mkoa kuitwa na kutii wito mbele ya kamati ya maadili na madaraka ya bunge kujibu mashitaka yake kunaibua dhana nzima ya misingi ya utawala bora. Lakini pia kunarudisha heshima kwa mhimili huu wa bunge ambao ulianza kupoteza mwelekeo uliosababishwa na makosa ya kiufundi.

Waingereza wana msemo wao unaosema divide and rule,wagawanye uwatawale. Moja ya makosa makubwa ya kiufundi yaliyosababisha bunge kukejeliwa na kudharauliwa na wateuliwa wa rais ni kusahau majukumu yao ya kibunge na kuligeuza bunge kuwa sehemu au chombo cha serikali kwa bunge wake kusimamia maslahi ya vyama vyao zaidi kuliko maslahi ya taifa. Hali inayosababisha serikali kudharau maazimio yanayopaswa kutekelezwa kwa amri ya bunge.

Party caucus zimekuwa na nguvu zaidi kwa wabunge watokanao na vyama vyao kuliko maslahi ya bunge ambalo ndicho chombo kikubwa cha uwakilishi wa wananchi. Hali inayosababisha serikali kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa kuwa party caucus hizo zimegeuzwa sehemu ya kuwatuhumu wabunge wenye mawazo na mitazamo inayokinzana na serikali tukufu.

Bunge kwa kuanza na wateule wa serikali wenye jeuri ya mwenye mamlaka ya uteuzi kuna rudisha hadhi na madaraka yake na pia kunatuma salamu kuwa bunge ni mhimili usioyumbishwa na kinatekeleza majukumu yake mujibu wa katiba.
 
Siku zote kikwazo ni wabunge wa ccm

Hawajawahi Kuwa wakweli

They fight for their ugali

Wangekuwa really huyo ngosha hata asingekuwa anatukaripia km wanafunz wa madrasa
 
Back
Top Bottom