Paradox of the church Ministry

Paradox of the church Ministry

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Wasalaam wakuu.

Nikijite kwenye mada.

Nimekua mhumini kwa muda mrefu kwa makanisa mbalimbali ila kwa msingi wa hoja yangu sitayataja.

Makanisa mengi idadi kubwa ni masikini na wale wenye madhira mbalimbali ya maisha kama wagonjwa, waliotalakiwa, waliofiwa na wapendwa wao etc.

Tashishwi niliyonayo ambayo natamani platform hii itazame kwa critical approach ni ktk mambo yafuatayo :

1: Kanisa lina hubiri usawa lakini maisha ya watumishi na waumini yapo katika mfumo wa ubwana na utwana.
Hili kumepelekea tofauti kubwa ya kipato kati ya wch/mapadree na waumini.

2: kanisa linahubili upendo na amani
Lakini idadi kubwa ya ndoa kuvunjika zinaongezeka kila uchao. Je hali hii inatoa taswira ipi kwa mafundisho ya kanisa katika kutoa mfano wa maisha kwa jamii?

3: kanisa limeaswa kuwatunza wajane na mayatima. Ila ni nadra sana kuziona huduma kama hizi kwenye Ministry nyingi..... Kama tunavyoona msisitizo katika kujenga masinagogi na kuhudumia maisha ya anasa ya watumishi kama vile:

1.Kuwa na mabordigad
2.Usafiri wa gharama
3. Majumba ya gharama ikiwa role model wao (Jesus) hakua hata na gheto.

Tafakuri yangu nataka kumulika uhalali wa watu kuona kanisa kama msingi wa maisha ya adiri na mwongozo wa njia ya maisha ya paradiso.

Nitngulize shukrani.

Karibuni wote.
 
(role model wao YESU?!) ndugu yangu YESU wewe unamtafsiri na kumuelewa katika dhana ipi? hivi unafikiri YESU alikuwa kama wanadamu wengine wa kawaida. yaani MUWEZA WA YOTE, MWENYE MAMLAKA YA MBINGUNI NA DUNIANI, MWENYE NEEMA YA UWOKOVU NA MWENYE KUREHEMU eti ndio hawe role model wa wachumia tumbo wa kanisa hawa. swali na hoja yako yaweza kuwa nzuri lakini kabla ya kutaka kuyajua yote pambana sana kumjua YESU ni nani then utajua utendaji wake wa kazi na baada ya hapo utapata majibu ya maswali yako yote wewe mwenyewe.
 
41ce551e7cacd19b0f07e8e3855da15e.jpg
 
Umeegemea subject Jesus, umesahau object dhana ya kanisa, kuwa role Model hainashida kwani kama wana hubili injili ya Yesu hawana budi kumfuata bila ya kujali kuwa hakuwa binadamu wa kawaida. Jibu swali acha kuongeza maswali
 
MUNGU NI ROHO, WAMUABUDUO IMEWAPASA KUMUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI hili fumbo wakristo wengi makanisani hawajafafanuliwa na kufunuliwa wakalielewa na ndio maana yanatokea hayo yote yanayokutatiza. majadala huu ni mpana sana siwezi kuuendeleza ndani sana hapa wasije wakainuka wapumbavu wakaleta dhiaka juu ya MUNGU maana ile roho chafu ya mpinga kristo iko kazini, imemeza wachungaji hata waumini ili watu wa MUNGU wasiijue kweli ambayo itawaweka huru.
 
(role model wao YESU?!) ndugu yangu YESU wewe unamtafsiri na kumuelewa katika dhana ipi? hivi unafikiri YESU alikuwa kama wanadamu wengine wa kawaida. yaani MUWEZA WA YOTE, MWENYE MAMLAKA YA MBINGUNI NA DUNIANI, MWENYE NEEMA YA UWOKOVU NA MWENYE KUREHEMU eti ndio hawe role model wa wachumia tumbo wa kanisa hawa. swali na hoja yako yaweza kuwa nzuri lakini kabla ya kutaka kuyajua yote pambana sana kumjua YESU ni nani then utajua utendaji wake wa kazi na baada ya hapo utapata majibu ya maswali yako yote wewe mwenyewe.
Kihistoria Yesu alizaliwa kwenye familia masikini sana, tena alikua akiishi galilaya, karne ya kwanza wakaazi wa galilaya walikua wanaonekana kama daraja la tatu baada ya waroma (watawala) na wayahudi wa jerusalem (jijini). Pia walikua hata wakiongea rafudhi yao ilikua tofauti hivyo ilikua rahisi kuwatambua. Movement/ injili ya Yesu iliwavutia wengi kwakua alionekana kua ni mmoja wao na ni kutoka familia masikini kama wengi wao. Ndio maana mara kadhaa walijaribu kumfanya awe mfalme wao, ujasiri wake dhidi ya watawala wakandamizaji uliwagusa wengi. Hata hivyo wanahistoria wanasema mwishowe waroma walichoka kumvumilia na wakaanza kumwona kua kitisho hivyo wakamuua.
 
Back
Top Bottom