Panya road na hatima ya Tanzania

Panya road na hatima ya Tanzania

nyelesa

Member
Joined
Apr 18, 2010
Posts
63
Reaction score
18
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni kundi hili lilileta sintofahamu juu ya usalama wa raia na mali zaoi jijini Dar es Salaam.Kama kawaida Polisi walichukua jukumu lao la kuhakikisha usalama unakuwepo kwa kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari wakidai kuwa ni wahuni wachache tu na kwamba wamedhibitiwa na Polisi.Taarifa hizo zilitolewa na Kamanda Polisi Kanda maalamu ya Dar es Salaam.Ukifuatilia taarifa zake zinaonyesha kuwa kundi hilo aidha lilikuzwa kupitia mitandao,lakini pia utaona haikuwa uzushi kama ilivyodaiwa na Kamanda Kova.

Ni ukweli usiopingika kundi hilo la Panya Road limevuta hisia kubwa katika jamii,na kwamba limeweza kuteka jamii kwa muda mrefu tangu lilipoanza uharifu hadi hali ilipotulia.Kwa nchi kama yetu haingii akilini kwa kundi hili kushika kasi kwa muda mfupi kama huo,ukizingatia kuwa kila raia anawajibika kuhakikisha amani inakuwapo nchini.Ni kwa nini dhana hii ya ulinzi inatoweka kwa mtanzania?

Jibu ni wazi kwamba,Tanzania ya sasa si ya zamani.Matabaka kati ya walionacho na wasiokuwa nacho limeongezeka mno kiasi cha kuona maskini hawana haki tena.Kiashiria hiki ni hatari mno kwa usalama wa nchi yetu.

Wapi tulikosea?Tulipoua Azimio la Arusha kila kila kitu kikaanza kupanganyika(fall apart).Viongozi wakaanza kuwa wenye sauti zaidi kuliko waaajiri wao(yaani wananchi). Miiko ya viongozi iliondolewa kinyemela.Hapa ndipo tulianza kuona kuota kwa shule zinaitwa English Medium Schools/English Academy Schools.Shule hizi zinawapeleka na kuwarudisha majumbani watoto kwa magari.Watoto hawabebi tena mfagio na dumu la maji.Watoto hawadeki madarasa yao nk.Hawa ni watoto wa wenye nacho.

Ni swali la kujiuliza,katika jamii iliyojengwa kwa misingi ya haki na usawa,iweje kuwepo na matabaka haya?Bila shaka jibu liko wazi kuwa ni ubibafsi wa viongozi wetu baada ya kuona Azimio la arusha linawabana wakaamua kuliua.Ikumbukwe,hata baada ya juhudi za kurejesha usawa huo kupitia Tume Ya KATIBA(Tume ya Warioba),bado watawala kupitia Bunge la Katiba wameamua kuitupilia mbali miiko ya viongozi ili waendeleza dhana ya matabaka.
Zipo hotuba za viongozi wa kisiasa waliodiriki kusema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka kama hatua madhubutu hazitachukuliwa na serikali.Viongozi hao walibezwa kwa kejeli na mawaziri wenye dhamana za ajira hivi majuzi.Sasa tunaona kilichojiri hivi punde kuhusu Panya Road!

Miaka ya 2004 ilitokea mivutano kati ya mgambo wa jiji la Dar ambapo wamachinga walimuua mgambo.Hizo zilikuwa dalili tosha za kutafuta ufumbuzi.lakini aidha kwa makusudi au kutokudhamiria serikali ilichukua au haikuchukua hatua.Hii ni ishara kuwa VICIOUS CYCLE OF POVERTY imeshika kasi.Natoa rai kwa serikali ichukue hatua kupambana na hali hii,sababu kama hakutakuwa na ulinganisho wa maisha katika jamii,amani ya nchi yetu itatoweka haraka sana.Vijana hao watakapochoka kusubiri unafuu wa maisha,hawatajali wewe nyumba yako inalindwa na mitambo maalumu, au una silaha gani wataingia na kuchukua wanachotaka sababu wana njaa.Vijana wasio na kazi ni wengi mno.Wanamaliza shule au vyuo mbali mbali wanabaki mtaani bila ajira.

Ni kwa nini wasijiite majina kama PANYA ROAD ili waweze kusikika haraka.Polisi wafanye tafiti za kina ni kwa nini kundi limeibuka kwa nguvu kubwa.Aidha serikali itafute suruhu ya kudumu kwa tatizo ajira kwa vijana.Leo Panya Road wako Dar,kesho Arusha,Mwanza,Mbeya na hatimaye nchi nzima na mwisho kabisa kundi la kigaidi.Tuchukue hatua kwa kujenga jamii inayopendana na kuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali za nchi.

Nawasilisha.
 
wewe wenzio wanaona hizo ni longo longo tu wanataka kushinda uchaguzi tu kwa gharama yoyote ile, bora liende.Hakuna anayefikiria Tanzania ya kesho kila mtu anajali tumbo lake na familia yake.
Kila gari linakimbia kufika.Tunafikiria waliopigana vita labda sio Waafrika kama sisi
 
Mbona umeongea ukweli sana, serikali isipochukua hatua lolote linaweza kutokea.
 
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni kundi hili lilileta sintofahamu juu ya usalama wa raia na mali zaoi jijini Dar es Salaam.Kama kawaida Polisi walichukua jukumu lao la kuhakikisha usalama unakuwepo kwa kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari wakidai kuwa ni wahuni wachache tu na kwamba wamedhibitiwa na Polisi.Taarifa hizo zilitolewa na Kamanda Polisi Kanda maalamu ya Dar es Salaam.Ukifuatilia taarifa zake zinaonyesha kuwa kundi hilo aidha lilikuzwa kupitia mitandao,lakini pia utaona haikuwa uzushi kama ilivyodaiwa na Kamanda Kova.
Ni ukweli usiopingika kundi hilo la Panya Road limevuta hisia kubwa katika jamii,na kwamba limeweza kuteka jamii kwa muda mrefu tangu lilipoanza uharifu hadi hali ilipotulia.Kwa nchi kama yetu haingii akilini kwa kundi hili kushika kasi kwa muda mfupi kama huo,ukizingatia kuwa kila raia anawajibika kuhakikisha amani inakuwapo nchini.Ni kwa nini dhana hii ya ulinzi inatoweka kwa mtanzania?
Jibu ni wazi kwamba,Tanzania ya sasa si ya zamani.Matabaka kati ya walionacho na wasiokuwa nacho limeongezeka mno kiasi cha kuona maskini hawana haki tena.Kiashiria hiki ni hatari mno kwa usalama wa nchi yetu.
Wapi tulikosea?Tulipoua Azimio la Arusha kila kila kitu kikaanza kupanganyika(fall apart).Viongozi wakaanza kuwa wenye sauti zaidi kuliko waaajiri wao(yaani wananchi). Miiko ya viongozi iliondolewa kinyemela.Hapa ndipo tulianza kuona kuota kwa shule zinaitwa English Medium Schools/English Academy Schools.Shule hizi zinawapeleka na kuwarudisha majumbani watoto kwa magari.Watoto hawabebi tena mfagio na dumu la maji.Watoto hawadeki madarasa yao nk.Hawa ni watoto wa wenye nacho.
Ni swali la kujiuliza,katika jamii iliyojengwa kwa misingi ya haki na usawa,iweje kuwepo na matabaka haya?Bila shaka jibu liko wazi kuwa ni ubibafsi wa viongozi wetu baada ya kuona Azimio la arusha linawabana wakaamua kuliua.Ikumbukwe,hata baada ya juhudi za kurejesha usawa huo kupitia Tume Ya KATIBA(Tume ya Warioba),bado watawala kupitia Bunge la Katiba wameamua kuitupilia mbali miiko ya viongozi ili waendeleza dhana ya matabaka.
Zipo hotuba za viongozi wa kisiasa waliodiriki kusema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka kama hatua madhubutu hazitachukuliwa na serikali.Viongozi hao walibezwa kwa kejeli na mawaziri wenye dhamana za ajira hivi majuzi.Sasa tunaona kilichojiri hivi punde kuhusu Panya Road!
Miaka ya 2004 ilitokea mivutano kati ya mgambo wa jiji la Dar ambapo wamachinga walimuua mgambo.Hizo zilikuwa dalili tosha za kutafuta ufumbuzi.lakini aidha kwa makusudi au kutokudhamiria serikali ilichukua au haikuchukua hatua.Hii ni ishara kuwa VICIOUS CYCLE OF POVERTY imeshika kasi.Natoa rai kwa serikali ichukue hatua kupambana na hali hii,sababu kama hakutakuwa na ulinganisho wa maisha katika jamii,amani ya nchi yetu itatoweka haraka sana.Vijana hao watakapochoka kusubiri unafuu wa maisha,hawatajali wewe nyumba yako inalindwa na mitambo maalumu, au una silaha gani wataingia na kuchukua wanachotaka sababu wana njaa.Vijana wasio na kazi ni wengi mno.Wanamaliza shule au vyuo mbali mbali wanabaki mtaani bila ajira.Ni kwa nini wasijiite majina kama PANYA ROAD ili waweze kusikika haraka.Polisi wafanye tafiti za kina ni kwa nini kundi limeibuka kwa nguvu kubwa.Aidha serikali itafute suruhu ya kudumu kwa tatizo ajira kwa vijana.Leo Panya Road wako Dar,kesho Arusha,Mwanza,Mbeya na hatimaye nchi nzima na mwisho kabisa kundi la kigaidi.Tuchukue hatua kwa kujenga jamii inayopendana na kuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali za nchi.
Nawasilisha.

Uonavyo Wewe TANZANIA Sasa Hivi Kuna TISS na MI Strong? TISS na MI Imara Ameondoka Nayo Hayati Baba Wa Taifa, Hayati Mzee Mzena, Hayati Mzee Walingozi Na Wastaafu Wengine Waliokuwa Chini Ya Mwalimu Kama Akina Mzee Kuyomba, Mzee Butiku, Mzee Kamalamo, Mzee Nzagi Na Wengine Wengi Tu Ambao Bahati Mbaya Sana Wote ni Wastaafu Sasa.

Hivi Unaingiza au Unaajiri Watu Kwa Undugunization na Ngononization Haswa Kwa TISS na MI Je Hapo Unategemea Nini? Zamani Palikuwa Na a Very Thorough Vetting Ya Recruits Wote Na Pia Kila Baada Ya Muda Fulani Hata Wakuu Nao Walikuwa Wanafanyiwa Vetting Ili Kujua Uadilifu Wao au Kama Wamebadilika Je Leo Yanafanyika Hayo? Idara Kama Za TISS na MI Si Za Kufanyiwa Mchezo Na Ni Za Kuchungwa Na Kutunzwa Kama Mboni Ya Jicho Lakini Leo Hii Big Dady Ameiharibu Na Kuingiza USWAHILI Huku UTARATIBU Mwingi Tu UKIBADILISHWA, Watendaji Nao Hawana Morale na Wapo Wapo Tu...Ukimpa Ofa Tu Kidogo Ya Biere au Gongo Anabwatuka Yote...Nina Mengi Ila Naishia Tu Hapa Kwa Today.
 
ISIS... !! wa tanzania muwe macho kama hamuataki hao Panya-rodi na mbwa mwitu, Basi ISIS watawapitia na kuwabeba !!
TISS lichukulie serious action makundi ya aina hii... kwani Mwanzo wa moto ni cheche !! halafu VIRUSI ndo mwanzo wa majanga!!
 
Uonavyo Wewe TANZANIA Sasa Hivi Kuna TISS na MI Strong? TISS na MI Imara Ameondoka Nayo Hayati Baba Wa Taifa, Hayati Mzee Mzena, Hayati Mzee Walingozi Na Wastaafu Wengine Waliokuwa Chini Ya Mwalimu Kama Akina Mzee Kuyomba, Mzee Butiku, Mzee Kamalamo, Mzee Nzagi Na Wengine Wengi Tu Ambao Bahati Mbaya Sana Wote ni Wastaafu Sasa.

Hivi Unaingiza au Unaajiri Watu Kwa Undugunization na Ngononization Haswa Kwa TISS na MI Je Hapo Unategemea Nini? Zamani Palikuwa Na a Very Thorough Vetting Ya Recruits Wote Na Pia Kila Baada Ya Muda Fulani Hata Wakuu Nao Walikuwa Wanafanyiwa Vetting Ili Kujua Uadilifu Wao au Kama Wamebadilika Je Leo Yanafanyika Hayo? Idara Kama Za TISS na MI Si Za Kufanyiwa Mchezo Na Ni Za Kuchungwa Na Kutunzwa Kama Mboni Ya Jicho Lakini Leo Hii Big Dady Ameiharibu Na Kuingiza USWAHILI Huku UTARATIBU Mwingi Tu UKIBADILISHWA, Watendaji Nao Hawana Morale na Wapo Wapo Tu...Ukimpa Ofa Tu Kidogo Ya Biere au Gongo Anabwatuka Yote...Nina Mengi Ila Naishia Tu Hapa Kwa Today.
Nashukuru kwa kuona hoja zangu,lakini kikubwa zaidi tuangalie Tanzania ya kesho,kushibisha matumbo haina faida kwani kesho lazima njaa itauma tu.Katika Ukanda wa Afrika na maziwa makuu,ni Tanzania pekee imebaki kuwa na amani.Sasa tusijione tuko salama sana,serikali ichukue hatua za haraka,kati na muda mrefu kutafuta suruhu ya kundi hili la vijana.Amani haitunzwi kwa mtutu wa bunduki, ila ni mkakati unaojengwa kwa mgawanyo sahihi wa keki ya Taifa.Vijana hawa wanahitaji washirikishwe au wathaminiwe tu.Kukamata vijana nakutangazi umma eti tumekamata mia tisa (900) siyo deterrent kwa vijana.Ningeshauri Polisi wajitathimini kwa nini wanafanya hivyo!
 
rat_2404143524.jpg
 
Back
Top Bottom