Panya Road muwasikie tu, usiombee

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
aise jana usiku wa siku kuu ya Xmas mtaani kwetu tumevamiwa na kundi la vijana wadogo, walikuwa takribani mia hivi wana mabegi mapanga mashoka marungu nk...walikuwa hawaibi bali wanafanya uharibifu na kujeruhi kila wanayemkuta kiukweli kila mmoja alinusuru roho yake .....wachache tuliobaki tulipata majeraha, hatukuwa na kwa kukimbilia tulibaki kwenye biashara zetu ila mtaa mzima ulijifungia ndani, walianza kuiba maeneo ya mabibo makuburi wamezunguka mitaa yote, wamevunja magari wametamba mpaka kunakucha. mimi niliyejifanya wa kanda ya ziwa nimevunjika mkono wanaume wa Dar es salaam wananicheka ..kweli kazi za ulinzi tuwaachie polisi....usiombe yakukute
 
Wanatamba usiku kucha unatoa taharifa asubuhi..mara sentensi ya juu hawajaiba sentensi za chini unasema walianza kuiba..kundi la watu mia unalihesabu vipi usiku umeme umekatika kama kawaida..
 
Dawa ya hao panya road ni kutundika risasi ya Kichwa na kila panya atakayekaa mbele ya Gari ni kukanyanga tu,ni washenzi sana wakishakula bangi zao kila Gari watakayoiona wanaipiga mawe.
 
Nikweli mkuu huku kinondon Mkwajun jana watu walikimbizana kila mtu kakimbia nilfunga office fasta nikaingia ndan kulala,,kisa panya road,,,week km 2 hiv zilzopita walipita na mapanga visu,,wakawa wqnapora njian na kujeruh watu live dada mmoja alikwapuliwa simu mbele yangu walikuwa km 10 hv ni vijana wadogo sana. Lkn shuhuli yao sio mchezo wakivamia afu hamkujiandaa,,walianzia bonde la mkwajun kule palipo pomolewa,, mosco,,mkwajun wakakimbia mpaka studio huko hawakuonekana tena mpaka jana saa nne hv
 
Unamuamini Kova???

kova anakamataga mibaba
miteja kariakoo na wapiga debe mbezi mwisho!
Anasema amekamata vibopa wa panya road!
Asubiri tuu lungu la magufuli maana siasa hakuna tena! ataisoma namba
 
"walikuwa hawaibi bali wanafanya uharibifu na kujeruhi"...."walianza kuiba maeneo ya makuburi mabibo" sasa hapo tuamini kipi??
 
Wanatamba usiku kucha unatoa taharifa asubuhi..mara sentensi ya juu hawajaiba sentensi za chini unasema walianza kuiba..kundi la watu mia unalihesabu vipi usiku umeme umekatika kama kawaida..

Na si hilo tu mkuu kama angekuwa amevunjika mkono angewezaje kuingia jf
 
gari la diwani kata ya makuburi limevunjwa kuna wasssssseshenzi wanapinga kila kitu, binafsi sio mwandishi wa habari kwa hiyo umahiri wa kupangilia habari usifanye mada yangu ionekane ya uongo
 
asante Polisi kwa kufanikisha ukamataji..,kuna defender kama mbili tatu zinasomba vijana wanaoshangaa shangaa wanakutambua kwa unyoaji, kama una umri wa kwenda shule na umenyoa kiduka au una rasta halafu umelewa unakamatwa safi sana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom