Nyamemba
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 845
- 447
Kikundi hatari cha uharifu, uporaji kimeibuka wilayani Serengeti katika kijiji cha Rung'abure na kuzua hofu kwa wakaazi wa eneo hilo kutokana na vitendo vinavyoambatana na kundi hilo.
Vijana hao ambao awali inaelezwa walikuwa wakipora na kufanya uhalifu katika mgodi wa dhahabu wa ACACIA NORTH MARA NYAMONGO wamekuwa tishio Kwani hufunga mitaa saa moja na kuanza kupiga watu hovyo na kuwapora mali na vitu wanavyokutana navyo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Rung'abure wilayani Serengeti wameelezea adha wanayokutana nayo na kuulaumu uongozi wa kijiji na polisi Mugumu kwa kulea kikundi hicho na kushangaa Kwanini watu hao ambao ni vijana wadogo wanaogopwa kiasi hicho, mkazi mmoja anasema ukitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji au kata na hata polisi usiku wanakufata na kukukata mapanga na kuhoji iwapo wanapataje taarifa.
Hawa vijana awali walikuwa mgodini wakifanya uharifu, kule mambo yamekuwa magumu wamerudi kufanya uharifu kijijini, wanabeba mapanga marefu mfano wa jambia lililonolewa pande zote, wanapita saa moja na kuamrisha watu wafunge maduka, hoteli na mabaa saa moja jioni baadae huanza kushusha kichapo kwa kila wanayekutana nao.
Wapo 8 lakini kila siku wanaongezeka na idadi, kiongozi wao anaitwa Ketentani au Bubuya, msaidizi wake ni Nyarugembe Benard Mbuluna na Chacha Bubuya. Wanabeba mapanga mawili mawili, wameeleza baadhi ya wananchi hao.